Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, August 14, 2012

Papaa On Tuesday........Hata Tukibanana Hapa Hapa Atakayepata Ni Aliyejaaliwa.

Kama ilivyoada ya kila siku ya Jumanne, Samuel Sasali aka Papaa anakuja na Papaa on Tuesday, na leo anasema Hata Tukibanana Hapa Hapa Atakayepata ni Aliyejaliwa
Katika ulimwengu wa Injili katika Jiji la Dar-es-Salaam,historia imeandikwa ambapo kwa mara ya kwanza Tamasha la Tanzania Love Festival imeandikwa katika Viwanja Vya Jangwani ambapo wanamuziki nguli wa Injili Don Moen pamoja na Nicolle Mullen walihudumu katika viwanja hivyo, Mungu awabariki wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kufanikisha Tamasha tajwa.
Mtaani kumekuwa na misemo mingi inayoonesha namna ya kung`ang`ania kile unachokiamini,mojawapo ya misemo hiyo ni kama ipo ipo tu, msemo mwingine ni Tutabanana Hapa Hapa. Wiki chache nikiwa katika matembezi yangu ya jioni nikiwa nimekaa na jamaa wa kijiweni pamoja na madereva wa taxi kikatokea kichekesho ambako kalipelekea huu msemo kuusikia. Tukiwa tumekaa akatokea mteja kwa ajili ya taxi karibu madereva 6 walimkimbilia mteja yule, dereva mmoja nilibaki nae pale maskani,yule mteja akawaacha wale wote waliokuwa wakimzonga akamfata yule dereva niliyebaki nae pale chini akamwambia nipeleke. Wakati yule dereva wa taxi akisimama akasema "Hata Wote Tukibanana Hapa Hapa, Atapata Aliyejaaliwa"neno hili likanipa tafakari ya siku baada ya kulisikia.
Katika Maisha kumekuwa na ushindani wa kila siku, Katika masomo kuna watu wanasoma weeeeeee lakini mwisho wa siku anayejitwalia namba moja ni yule ambaye pengine wala haonekani kuwa na bidii. Katika Kizazi chetu kupata ajira imekuwa ni changamoto unakwenda kwenye Interview una sifa zote na umefanya interview vizuri lakini mwisho wa siku anapata mwingine kabisa. Suala la Biashara nalo ni changamoto kuna watu tunadhani wangefanya vizuri lakini wanafanya vema ni wengine kabisa mpaka wengine wameitwa wana mkono wa biashara.Kuna Wadada kwa jinsi walivyo tulitegemea wao waolewe mapema lakini mambo yako tofauti na vile wale wanaonekana wangechelewa ndio wanao tangulia, itasikia watu wanasema kuna watu wamezaliwa na bahati kwenye maisha wana kismat.

Wenzetu Waislam wamekuwa wakiamini kila mtoto duniani ana riziki yake, kila anayekuja duniani ana share ama ana sehemu katika mgawanyo wa riziki za Mwenyezi Mungu hapa duniani, hata tukibanana namna gani basi kila mtu ana sehemu yake ya kumfanya aweze kuishi hapa duniani. Mtaani kuna maneno kama Ngekewa, Ngekewa maana yake ni kama Nyota kumaanisha kuna watu nyota zao ziko na mwanga sana kuliko wengine.
Kwenye Biblia kuna kitu kinaitwa "Kukubalika" ama "Kupata Kibali" kwa lugha ya kimakonde wanaita "Favor". Kibali kinakutofautisha na watu wengi sana kwenye maisha. Na hauhitaji jitihada kukubalika as long as ile neema iko juu yako, ni kama vile samaki asivyopata shida kuogelea ama ndege kuruka hewani ndivyo ambavyo ukiwa na kibali huitaji kuwalazimisha watu wa kukubali. Kuna watu ninawajua kwenye maisha yangu wanafanya kazi kwenye maofisi wao wanapendwa sana na wafanyakazi wenzao, na hii ni automatic hakuwahi kuwalazimisha watu wawapende basi tu inatokea kukubalika, mbaya zaidi kuna watu wanajisikia vibaya eti wewe unavyokubalika utadhani ulifanya application letter ya kukubalika ya kwake ikashindwa. Kuna Ma Mc wengi sana duniani, na kuna wengine Wanavaa sana, kwa kadri wanavyovaa ndivyo wanavyozidi kuwa kero ila kuna watu ambao wanakubalika Wakishika Microphone tu Watu wote Mioyo yao iko tayari kumpokea, huyu mtu amepata Kibali ndani ya mioyo ya watu.
Rafiki yangu John Lisu Muimbaji wa Nyimbo za Injili, Sio Kwamba anaiomba Saaaaaaana, au anapiga Ma-cord ya Muziki sanaaaa, John Lisu akishika Gitaa lake akasimama mbele za Watu akianza tu kuimba watu wote wanapokea, Kwanini??huyu Mtu anakibali ndani ya mioyo ya watu. Mwaka huu nikiwa Uwanja wa Taifa katika Tamasha la Pasaka nilishangaa sana aliposhika Microphone Rose Muhando, yaani huyu Mama anaimba nyimbo zile zile ambazo tunazisikia kila send off na harusi tukienda lakini akianza tu kuimba kuna hali ya tofauti hutokea huyu mtu ana Kibali kwenye mioyo ya watu. Haya mambo sio kuimba tu na kwenye maofisi hata kwenye kuoa na kuolewa. Hujawahi sikia watu wanasema "Maharusi Hawaendani" unakuta Mkaka Bongeee la handsome halafu mdada mtu wa kawaida sanaaaaaaa, au unakuta familia moja masikini nyingine ni tajiri kwanini haya huwa yanatokea kwenye maisha??haijalishi watu wako wangapi duniani wanafanya kile kile unachofanya ama wanashinania kile unachoshindania, kama ipo ipo tu.
Nimejifunza kuto kukata tamaa katika kile ninachokifanya zaidi ya kukiboresha, huwa siogopi wala sijisikii wivu mbaya kuona kuna mwenzangu anakubalika zaidi yangu, ukiangalia mawimbi yanayokuzunguka utazama kama Petro kwenye bahari. Sitaacha kuwa Mc sababu kuna ma Mc wengi sasa hivi Dar ama Tanzania, Kila Mtu ana Upako wake kuna event ambazo watu wakikaa kwenye vikao watasema tu, atafutwe Papaa, Sitaacha kuwa na Blog eti sababu kuna watu wengi wanafanya Blog, Kila Blog ina upako wake na Kila Mwandishi ana kibali chake, Siwezi jenga fitna kwa mtu ama kuwa na wivu kwa mtu sababu eti yeye anakubalika zaidi kuliko mimi, ninajua hakuwahi fanya application ili akubalike ila Kibali kimemfanya akubalike katika maisha yake. Nimewahi ona Wadada wazuri na warembo wakiwa na shauku ya kuolewa wanabaki king'aa macho wakati wale unaoona ni kituko ndo wanavaa mashela. Hujawahi ona Mtoto wa Masikini anapona Hospital na Mtoto wa Tajiri anakufa hospitali hiyo hiyo??
Kizazi chetu kila mtu anatafuta "Kutoka" hata watumishi wa Mungu pia Wanatafuta Kutoka, ukweli ni kwamba ukitaka Kutoka bila kibali inakula kwako, kila unachofanya kitageuka kuwa kero na kila mtu atakuwa anakaa mbali na wewe. Kibali kinawavuta watu kukusaidia na kuwa na wewe. Nimeshuhudia nimekuwa na marafiki wengi wenye kunisaidia katika mambo mengi si kwa sababu ninajua sana ila Mungu amenipa Kibali mimi na Blog yangu. Kupitia Blog hii nimekuwa na Marafiki Ulimwengu Mzima, sio Sumbawanga,, Sio Ukerewe, Sio Namtumbo, Sio Ulaya, America na hata Asia, Watu wamekuwa wakipokea katika Madhabahu hii, sasa kwanini tugombanie fiti wakati wote tunajenga nyumba moja??Hata kama tutabanana hapa hapa wote atapata aliyejaaliwa.
Mwalimu Wangu Pastor Carlos pamoja na Mwalimu Wangu Mgisa Mtebe Waliwahi nifundisha wakaniambia Kile ambacho unafanya Vizuri na hautumiii Msuli Mkubwa Kukifanya hautumii muda mrefu kukifanya na Unafanya Kwa Ustadi Mkubwa ukiambiwa kukifanya basi Kitazame hicho kwa Umakini. Mwalimu Wangu Mgisa Mtebe aliniambia "Maji hayajitahidi Kulowesha" Mwl. Wangu Carlos aliniambia "Samaki hafundishwi Kuogelea". Mwl. Mgisa aliniambia Yeye akipewa Kuwa Mc Jasho litamtoka Kutafuta Maneno, Ila Kuna watu wakipewa kuwa Ma Mc utashangaa amepata wapi hayo maneno ya kuongea. Kuna watu wako talented hata kuwaza, wakati wewe haujawaza hicho kitu yeye alishawaza kitofauti zamaniiiii. Kila mtu Mungu amempa fungu lake. Ukiona Kuna Kitu unatamani Kukifanya halafu unapata nacho sana tabu kujiandaa ili ukifanye basi jiulize mara mbili mbili. Kuna watu wanashangaa Papaa Unapata wapi Uwezo  wa Kuandika Papaa On Tuesday Kila Jumanne, Ukweli ni Kwamba Mimi Ninawashangaa wale wanaonishangaa Sababu nina Papaa On Tuesday nyingi mpaka nashindwa ipi niandike, Kwa Mwaka kuna majuma 52 ina maana Kwa Mwaka Ninaandika Papaa On Tuesday 52 na tangu nianze kuandika huu ni mwaka wa 3, Mimi nashangaa Wale wanaoshangaa. Mungu amenipa hiyo nafasi ni kazi yake kunipa cha Kuandika na sio mimi kutoka na Jasho. Nisipo kuwa na cha kuandika jumanne naumwa nakosa raha kabisa.
Hata kama tutabanana hapa hapa atapata aliyejaaliwa. Mungu yuko tayari kukupa Kibali katika eneo ambalo amekusudia kukutumia,utalazimishia mambo sana kwenye maisha "Neema" ni mafuta ya griss katika Vyuma. Mungu atusaidie.
Think Differently and Make a difference.
Papaa Ze Blogger.
0713 494110.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda