Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, August 13, 2012

Mwanossa akabidhi ng'ombe wa JK kwa wananchi Ngorongoro

Na Mary Margwe,
Ngorongoro
Kutokana na ukame mkubwa ulioukumba Wilaya ya Ngorongoro, Mkoani Arusha  msimu uliopita,jumla ya ng’ombe wapatao 40 wenye thamani ya sh.mil.15 wamekabidhiwa kwa wananchi wa Kijiji cha Meshil Kata ya Olbalbal na Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Kapteni Honest Mwanossa.

Akikabidhi mifugo hiyo kwa wananchi hao Kapteni Mwanossa alisema  mifugo hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete  kwa lengo la kutoa mkono wa pole kwa wananchi walioathirika  kwa ukame kwa kupoteza mifugo yao.

Kufuatia  tukio hilo Kapteni Mwanossa alisema Serikali imejipanga katika   kuwasaidia kuwaletea maendeleo wananchi wake ikiwa ni pamoja  na kutoa misaada pale ambapo inahitajika,ambapo Agosti 3,mwaka huu Rais Kikwete alizindua mradi wa mifugo (Seed Stock) kwa wale wananchi waliopoteza kabisa mifugo yao , na hivyo kutolewa kama kifuta jasho.

“Wananchi wenzangu tuna kila sababu ya kuishukuru Serikali yetu ya Tanzania  bila wasiwasi wala mashaka yoyote, kwani inatekeleza ahadi zake kimya kimya  maneno madogo lakini utendaji wake ni mkubwa alisema Mwanossa.

Akisoma risala ya utii kwa mh.Jakaya Kikwete,Mkuu wa Wilaya  ya Ngorongoro Bw.Elias Wawa Lali aliisema, ukame ulioukumba Wilaya hiyo  kwa msimu uliopita ulisababisha vifo vya ng’ombe wapatao 115,422 ambapo  kwa sasa ng’ombe 40 wamekabidhiwa wananchi wa Kijiji cha Meshil kata ya Olbalbal.

Aidha Bw.Lali alifafanua kuwa shughuli kubwa za kiuchumi katika Wilaya hiyo inategemea mifugo kwa asilimia 80%, ambapo kwa sasa Wilaya hiyo inakadiliwa kuwa na ng’ombe 319,489, mbuzi 419,591,  kondoo 421,655,  na punda wapatao 23,080.

Bw.Lali alisema kutokana na mvua za vuli kunyesha ktika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo,hali ya malisho  na maji kwa mifugo ni ya kuridhisha , na hivyo kupunguza matukio ya mifugo kuhama  kwenda maeneo mengine ndani   na nje ya Wilaya kwa lengo la kufuata malisho na maji.

“Hadi sasa wafugaji wangu wametulia kwani hakuna matukio  ya mifugo  ya  kuhama hama kwa sababu ya kutafuta malisho na maji,jambo ambalo ukilinganisha na kipindi cha nyuma kwa kweli tunazidi kumshukuru mwenyezi Mungu”alisema Mkuu huyo.

Wakiongea kwa nyakato tofauti wananchi hao walimshukuru mh.Kikwete kwa uwamuzi wake wa kuhakikisha kuwa anawasaidia kutoa kifuta machozi  kwa kile walichokidai kuwa nikitendo cha uzalendo.

 Bw.Lali aliongeza kuwa  kwa mwaka 2012 jumla ya ya miradi 6  yenye thamani ya  zaidi ya mil.300 ilipitiwa na mbio za mwenge wa uhuru,ambapo miradi ilifunguliwa ,mradi mmoja ulizinduliwa,miradi 2 iliwekewa mawe ya msingi huku mradi mmoja umeendelezwa kwa kugawa ng’ombe.

Hata hivyo alifafanua kuwa kati ya fedha hizo ,wananchi walichangia kiasi y ash. Mil. 29,854,000, Serikali kuu walichangia sh.mil.133, 497,587, wafadhili nao waliunga mkono kwa kuchangia sh.mil. 216, huku Halmashauri ya Wilaya ikiwa imechangia sh.mil.7

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda