Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, August 2, 2012

MGOMO WA WALIMU WAANZA KUATHIRI RATIBA ZA TAALUMA.MBULU


WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WAKISUBIRI VITA YA SERIKALI NA WALIMU IISHE ILI WAFANYE MITIHANI (WALITAKIWA WAWE NA MTIHANI LEO LAKINI WAMESHINDWA KUFANYA  KWA SABABU ZILIZO JUU YA UWEZO WAO.


Na Nelson Faustin-Haydom.
Wakati sakata la mgomo wa walimu likiendelea kuisumbua jamii bila ya kujua hatma yake, mkoa wa Manyara ni moja kati ya mikoa ambayo mgomo huu umeanza kuonyesha athari hasa katika ratiba za kitaaluma.

Tangu mgomo huu uanze, nilipata fursa ya kutembelea shule kadhaa hapa katika tarafa ya Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara hasa zile za vijijini nikidhani kuwa angalau walimu watakuwa wanaendelea kuudumisha wito lakini cha kushangaza hali imekuwa ni tofauti kabisa na kwa taarifa tu ni kwamba huku vijijini hali ya mgomo ni mbaya sana.

Ratiba ya mtihani wa utamirifu (mock) darasa la saba kwa wilaya ya Mbulu ulitazamiwa kuanza tarehe 1/8/2012 lakini kutokana na mgomo huu imeshindikana kufanyika hadi hapo itakapo pangwa tena hii ni kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Haydom Bw. George F. Dahhmay ambaye na shule yake yenye jumla ya watihiniwa 172 mitihani hiyo imeshindikana kufanyika kutokana na sakata hili la mgomo.

WANAMACHUNGU LAKINI BADO WANAIMANI
Mbali na hilo, kwa taarifa tu ni kwamba, shule ya msingi Haydom ina jumla ya wanafunzi 1,052 na walimu 21 lakni cha kushangaza ni kwamba yupo mwalimu mkuu peke yake na ana jukumu zito la kusimamia wanafunzi wote hao kwani walimu wengine wote wapo kwenye mgomo. Hii hali inatisha sana na kama hali hii ikiendelea bila ya pande zote mbili kukaa chini na kuangalia njia bora ya kulisaidia taifa hili, tunaweza tukaishia  pabaya sana.

Mheshimiwa sana raisi wa nchi jana alitoa rai kwa kusema kuwa, "Jambo la tatu na la mwisho ni mgomo wa walimu.  Pengine ni mapema kusema kwa vile kesho Mahakama itaamua kuhusu shauri hilo.  Lakini napenda kuwahakikishia walimu kuwa tunawajali, tunawathamini na kutambua mchango wao muhimu kwa taifa letu.  Wakati wote tumekuwa tunashughulikia madai ya haki zao na malimbikizo mbalimbali.  Madai ya safari hii ni makubwa mno, yametuzidi kimo.  Athari za kuyatimiza yalivyo yataifanya bajeti ya Serikali kutumia asilimia 75 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali na kubakiza asilimia 25 kwa kuendeshea Serikali na kutimiza majukumu ya maendeleo kwa wananchi.  Haitakuwa sawa.  Ndiyo maana tumeshindwa kuelewana walipokataa rai hiyo na wao kusisitiza kugoma. Wakati tunaendelea kusubiri uamuzi wa Mahakama, nina maombi mawili kwa walimu:  Moja, wasiwalazimishe walimu wasiotaka kugoma wafanye hivyo, wawaache waendelee na kazi.  Pili, wasitumie watoto isivyostahili kujenga hoja zao.  Nawasihi warudi kwenye meza ya mazungumzo."

(OHAYODA NDANI YA OFISI YA WALIMU)
WAKATI HUO HUO
Viongozi wa CWT wilaya ya Mbulu jana walikamatwa na kuwekwa rumande kwa masaa kadhaa wakihojiwa na polisi kwa kile kinachodaiwa kuchochea mgomo huo. Ohayoda iliweza kuongea na katibu wa CWT wilaya ya Mbulu ndugu Zacharia B. Naali na alikuwa na haya ya kusema
"Ni kweli tulikamatwa na kushikiliwa na polisi kwa madai ambayo kimsingi si ya kweli. Tunashutumiwa kwa kupita mashuleni na kuchochea mgomo kwa kuwahamasisha walimu wagome lakini sisi (yeye na mwenyekiti wa CWT wilaya ndugu Wensenslaus L.Musenya) tulikuwa ofisini hatukutoka, wanamfahamu mtu aliyekuwa anapita mashuleni na kuchochea mgomo lakini hawajamkamata." Alisema bwana Naali
Aidha akizungumzia hatma ya mgomo huo na athari zake katika wilaya ya Mbulu ndugu Naali alisema kuwa walimu wote wamegoma na wanachosubiria ni matokea ya shauri kutoka katika mahakama kuu kitengo cha kazi na kauli ya viongozi wa CWT Taifa lakini viongozi hao wa CWT wilaya wanatakiwa waripoti katika kituo cha polisi cha Mbulu tarehe 6 ili kujua kama watafikishwa mahakamani na wapo nje bila masharti.


HABARI ZAIDI KATIKA PICHA


OFISI YA WALIMU IMEFUNGWA. (2-8-2012) SAA 4:15 ASUBUHI.


KUINGIA NDANI-SIKUMKUTA MWALIMU HATA MMOJA.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda