Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, August 30, 2012

Matukio katika Picha: Baada ya maonesho ya Biashara yaani Sabasaba Nane Nane,,,Sasa ni "Haydom Cultural Festivals". ndani ya Haydom

"Nipo Kwa Sababu Upo"
Ni kauli mbiu ya tamasha hili la utamaduni ambalo kwa Hakika hii haijawahi kutokea. Kuanzia leo hadi tarehe kumi mwezi wa tisa, OHAYODA itakuletea matukio katika picha za namna ambavyo maandalizi yanapamba moto hadi siku na baada ya tukio lenyewe. Kwa wale wadau wa "Truly Tanzanian" usikose fursa hii ya muhimu hatua kwa hatua. Karibuni sana....................Tamasha hili litafanyika tarehe 6-8 september mwaka huu katika viwanja vya Kituo Cha Utamaduni hapa Haydom.

Lango kuu la kuingilia viwanja vya "culture" tayari kwa tamasha.


Kamati kuu ya maandalizi ikiwa "Busy" na maandalizi mpaka kieleweke

Mmoja wa wadau wa kutengeneza nyumba za asili akiwajibika tayari kwa maandalizi hayo.

Moja kati ya vivutio ambavyo tunauhakika hujawahi kuviona na hii ndo fursa pekee.Dada Janeth na Elifadhili wakipanga mikakati mbalimbali ili tu kuhakikisha kuwa tamasha hili linafana.

Ndani ya Pavilion kuna Nyota ambayo ina Pembe sita zinazowakilisha makundi ya makabila manne, hospitali na uwepo wa serikali katika mji mdogo wa Haydom.

Bloggers wa OHAYODA wakiwa kazini poriniiiiiiiiiiii.. Amani Paulo na Comrade Meku.

Blogger Amani Gaseri akiwa na Febronia wakipumzika baada ya ruti ndefu walipokkwenda kutafuta miti ya kutengenezea mabanda.

Hili si shimo bali ni nyumba ya wairaqw..sasa uje uone nyumba ambayo ni zaidi ya self container. Juu udongo wa kichuguu ndani watu na mifugo wote...
Mzee Lameck akikkumbushia enzi za namna ambavyo nyumba za wanyiramba zilivyokuwa zinatengenezwa.
Ukishangaa ya Wairaqw utayaona ya Wadatoga...sasa hapa ndo ya aina yake..Nyumba hii ilikuwa inatumiwa na wairaq, baada ya kuona kuwa wamasai wanawachomea ndo wakaamua kuezeka kwa udongo tena wa kichuguu...

"Main Entrance" na ukiagalia kwa makini unakutana na "Partition" ya ukweli, watu juu. wanyama chini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda