Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, August 13, 2012

Mapungufu ya Mtu mwenye tabia za kundi la Koleriki - Sehemu ya Kwanza (You become a Blessing by Exactly knowing who YOU are)


Na Nelson Faustin Nderemo.
Baada  ya kufahamu kwa undani juu ya sifa njema za Makoleriki, yani watu wenye tabia za kundi la Koleriki.
Leo tujifunze juu ya mapungufu ya Koleriki. Katiaka makala iliyopita tulijifunza kuhusu uhalisia wa namna ambavyo koleriki anaishi na watu kwa kuyatazama sifa njema za koleriki. Leo japo kwa ufupi, tutajifunza juu ya mapungufu ya koleriki kwani kwa uhalisia anaonekana kuwa na mapungufu mengi kuliko ubora wake.


 Dondoo za mapungufu ya Mtu mwenye tabia za kundi la Koleriki ni kama ifuatavyo.

 • Ni wepesi sana kuwaburuza wengine kutokana na tabia zao na hii humfanya awe na uadui mkubwa sana na Masangwini pamoja na Mamelankoli.
 • Mara nyingine wanafikiri kuwa wao wanahaki ya kusahihisha makosa ya wengine kama vile wao huwa hawakosei.
 • Madhaifu ya wengine hupewa sana kipaumbele kuliko ya kwao wenyewe japo wanayo mengi sana.
 • Ni wepesi sana kuwa na kiherehere na kuwa nafasi za mbele hata kama hawahusiki au kustahili. Mara nyingi hii huwafanya watoe kauli kama, "Fulani hawezi afadhali mnipe mimi................".
 • NI warahisi sana kusababisha machungu kwa wale wanaowazunguka kama vile, familiya na mahali pao pa kazi kutokana na kauli kandamizi nk.
 • Uwezo wa Koleriki kushirikiana na wengine ni mdogo sana kwani mara nyingi huona kuwa wengine hawana uwezo wa kufanya kama wao.
 • Hapendi kusimamiwa na hii husababisha ugomvi mkubwa sana popote pale alipo.
 • Hitaji lake la kujali sana kazi kuliko watu, humsababisha kusahau ubinadamu ulioko ndani ya wanadamu wengine kwani hudhani kuwa watu ni sawa sawa na mashine.
 • Si wavumilivu na hii huwafanya wawe walalamishi sana.
 • Ni watu wenye amri sana.
 •  Wanamaringo na Kiburi.
 • Wanapenda kuelezwa na si kuelekezwa kwasababu wao ni "much know".
 • Ni wakali sana na wenye hasira nyingi.
 • Koleriki ana majibu ya mkao na ya kukatisha sana, usipokuwa mvumilivu unaweza kumtukana au hata kumpiga.
 • Ni wepesi kuwatumia watu katika kujinufaisha wenyewe/wabinafsi sana.
 • Ni wazuri sana katika kuonesha upendo mwingi kwa watu wa nnje wakati watu wake wa ndani wakiangamia.
 • Koleriki ni mwanadamu ambaye anaweza kufanya maamuzi kwa niaba ya kundi fulani bila hata kuwashirikisha.
 • Ni wepesi sana kusaidia mambo ya nnje lakini ya ndani kwa mfano nyumbani kwao ni jambo ambalo hawalipatii kipaumbele.
 • Ni wagumu sana kuwa na marafiki na pia hata wakiwa nao hujikuta wakiwa na marafiki wachache kutokana na kwamba huwabagua sana marafiki wa kuwa nao katika maisha.
 • Ni maboss kwa asili. Ni watu ambao kwa asili ni watu wakujiona wenye hadhi ya juu na kutakiwa kuwatumikia wengine kuliko wanavyoweza kuwatumikia wao hata kama kiumri na kielimu wapo chini.                                                                                  
Koleriki dhidi ya Watu wa Haiba nyingine.
                                                                                                                                                  Itaendelea..................................

Usisahau
Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo leo, tumeshajifunza HAIBA kuu mbili.

Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
Unajitambua? Au Unaishi tu kwa sababu siku zinaenda?
               
(Unadhani Huyo Mbwa Kapenda kulala alipo? Ukimuuliza Koleriki atakujibu)
(We remain little Beings, trying to give You the little we have, Receive it Please.)


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda