Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, August 5, 2012

Maisha Yamekosa Maana kwangu, Ninaomba Ushauri wako, Ninajua Unaweza kunishauri, Tafadhali, Nisaidie Japo kwa Neno Moja tu Nipone...


Na Nelson Faustin.
Karibu mpenzi msomaji wa blog hii ya OHAYODA, Leo ninakukarisha katika makala mpya tuliyoipa jina la:-
 "Maisha Yamekosa Maana kwangu, Ninaomba Ushauri wako, Ninajua Unaweza Kunishauri, Tafadhali Nisaidie Japo kwa Neno Moja tu Nipone... .....".
 Lengo kuu la kuwa na makala hii ni kuweza kutoa hadithi au mkasa uliomkuta mtu fulani, na katika hili tutatoa nafasi kwako wewe msomaji wetu siku ya leo Jumapili utume ujumbe wako katika "comment box" hapo chini ili tuweze kumsaidia mtu huyu kwa kumshauri ili kumpatia "moral support" kwani tunaamini kuwa si kila tatizo linahitaji pesa au msaada wa mali  bali matatizo mengi yanahitaji tu "mguso wa ushauri wako." Huu utamsaidia yeye na wengine wengi ambao wapo katika hali kama yake.

Tunaanzia hapa kwa Jumapili ya leo..................................

"Nilikukuwa nina umri wa miaka kumi pale nilipoondokewa na wazazi wangu wote wawili mwaka 1995 kwa ajali ya gari. Tulikuwa na safari ya pamoja kutoka Dar es salaam kwenda Moshi kwa bibi kwaajili ya christmas mimi, baba, na mama yangu mzazi. Baba ndiye alikuwa dereva na tulipofika maeneo ya Mto Wami tulipata ajali mbaya sana iliyopelekea wazazi wangu wote wawili kufariki dunia pale pale...........................Nilipata mshtuko na kuzimia  pale pale......................

Kwa neema ya Mungu nilijikuta hospitalini Muhimbili muda wa saa kumi jioni na nikaambiwa kuwa nililetwa na mtu aliyejitambulisha kama dereva wa lori aliyetusaidia baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Mto Wami.  Kesho yake asubuhi nikaambiwa kuwa ninatakiwa kutoa maelezo namna ambavyo nitawapata ndugu zangu wengine ili tufanye mikakati ya mazishi, sikuamini kuwa ndo mwisho wa kuwaona wazazi wangu,................niliumia sana.................ilibidi tu nikubaliane na hali hii na mwishowe tukaenda kuzika salama nikarudi Dar kuedelea na shule.

Baba yangu mkubwa aliamua kuchukua jukumu la kunilea na japo kwa bahati mbaya mke wake hakuwa anaelewana na mama yangu, katika hili aliamua kunichukia sana na hata watoto wake wote waliamua kunichukia hata kufikia hatua ya kunitesa kwa namna mbalimbali, kama  vile kuninyima chakula, kunilaza chini nakadhalika.

Katika familiya yetu, wazazi wangu walibahatika tu kuwa na mtoto mmoja wa kike ambaye ni mimi na nililelewa katika maisha ya kudekezwa sana. Sasa nina umri wa miaka 27 na katika kipindi chote cha maisha nilikutana na mambo magumu sana tena ya kukatisha tamaa lakini namshukuru Mungu nipo hapa nilipo leo, Kwani mali zote za wazazi wangu zilitwaliwa na ndugu zangu wote nikabaki na sanduku la nguo tu.

Kwa bahati mbaya sana sikufanikiwa kuendelea na masomo ila Namshukuru Mungu nilibahatika kufungua genge maeneo ya Mianzini Arusha na baadaye Soko kuu. Kinachonitesa sasa hivi, hadi nikaamua kukuandikia ili kukuomba ushauri ni kwamba, kutokana na sababu mbali mbali familiya ya baba yangu mkubwa ilitengana na wote wakasambaratika baada ya baba mkubwa kuamua kuoa mke mwingine. 

Hapa nilipo nimegundulika kuwa ninamatatizo yanayotokana na sumu niliyowekewa kwenye chakula na mmoja wa watoto wa baba yangu mkubwa kwa shinikizo la mama yake. Kwa neema ya Mungu sikufa bali nilipata matatizo makubwa mawili, kwanza iliharibu mfuko wangu wa uzazi ambao ulitolewa nikiwa na umri wa miaka 25, pili uti wangu wa mgongo hujaa maji mara kwa mara ila nina kliniki hapa Mount Meru Hospitali huwa ninapewa huduma ya kusafishwa kila baadaya ya siku nne au tano.

 • Ndugu zangu, mama yangu mkubwa (aliyekuwa mke wa baba mkubwa) amekuja Arusha ni wiki sasa na anasema hana msaada mwingine ila mimi, Je nimsaidie? Au ndo anampango wa kunimaliza kabisa Kutokana pia anasemekana kuwa na imani za kishirikina?
 • Mwanae aitwaye Alex ambaye ndo inasemekana aliniwekea sumu na mbaya zaidi alinibaka kipindi ninaishi kwao, yeye naye anaugua ugonjwa wa saratani na yupo hapa Mount Meru hoi hawana hata chakula, nimfanyeje?
 • Nilibahatika kuolewa mwaka jana na sasa ninaishi Njiro, ila hatujafanikiwa kupata mtoto na sijathubutu kumwambia mume wangu tatizo nililonalo, nimwambie au nifanyeje ili kuinusuru ndoa yangu kwani ninampenda sana mume wangu na yeye ni msaada wa pekee sana kwangu na ndugu yangu wa karibu sana kwani tulianza mahusiano nikiwa nina umri wa miaka 17 nilipofika tu Arusha nikiwa katika hali ngumu sana ya maisha.
 • Mtoto wa kike wa baba yangu mkubwa anayejua kuwa mimi ni tasa ameanza kuifuatilia ndoa yangu kwa ukaribu huku akitaka kuzaa na mume wangu na ameshaniambia kuwa ni lazima azae naye, nimfanyeje?
Nina mengi sana ndugu zangu ila ninaomba sana ushauri wenu kwani kulipiza kisasi sijajifunza na wala kuwasamehe ni kiti kigumu sana kwangu kwa sasa, ingekuwa wewe ungefanyaje?

Ninaomba ushauri wako kupitia blog hii au kupitia e-mail ya blogger ambayo ni sonnelly06@gmail.com. Nipo kwenye kipindi kigumu sana kimaisha ndugu yangu".

Mpenzi msomaji, bila shaka umeipata stori nzima, embu vaa viatu vyake uone ungefanyaje.

Tunasubiri Ushauri wako.

000000
Asante na tunakutakia jumapili njema yenye baraka na tuonane tena jumapili ijayo kwa kisa kingine..


NB..Ukiwa na kisa au taarifa ya mtu ambaye atahitaji wadau wa OHAYODA wamsaidie, tafadhali wasiliana nasi kupitia e-mail yetu sonnelly06@gmail.com au tupigie simu 0714080311 au 0784238225

1 comment:

 1. daahh sijui nianzie wapi .

  Pole nadhani utakuwa mwanzo mzuri .

  kitu cha kwanza nitakacho kushauri ni hiki jipunguzie "MAWAZO" mawazo ndio yatakayo zidi kukuathiri kila kukicha.

  Na jinsi ya kujipunguzia mawazo ni kuwa mkweli na nafsi yako.

  umepitia mengi sana, hakuna binadamu anaestahili kupitia uliyopitia. ila dunia ni shule na umesha faulu mitihani mengi sana.

  Sasa Nitakachokushauri ni hiki "ANZA UPYA"
  anza upya na mumeo. anza kumshirikisha mumeo kwenye mambo hayo . na cha kwanza kabisa kusanya nguvu zote ulizo nazo "Mwambie ukweli" kuhusu ya kwamba wewe ni tasa. Na kama unavyosema mmejuana kwa muda sana tangu ukiwa na miaka 17. na anaelewa yote uliyopitia "kupoteza wazazi" etc. anaweza kukuelewa na pia kukupa nguvu mpya.

  kwa kweli anza kumshirikisha mumeo kwenye haya mambo na unaweza kujipunguzia mzigo mkubwa sana.

  kumbuka dunia tapara bovu , ni wengi hawapendi kuona mafanikio ya wengine. wewe umejivuta uka kokomaa kuimarisha na kujenga maisha yako lakini hao ndugu wamerudi wanataka kukuvurugia.

  Na hakika ukimwambia mumeo kila ulichoandika hapa. huyo mumeo kama anakupenda haswa atakusaidia tu. mueleze kila kitu kuhusu hao ndugu wabahili.

  Mwisho ningependa kusema ni ngumu sana kwa sisi kukwabia nini cha kufanya na hao ndugu. wengi watasema kaa nao mbali "usiwa karibishe kwako" lakini kuna wengine wasamaria wangesema wapokee. sana sana tutakuchanganya.

  Ila atakaekusaidi ni yule anaejua zaidi kuhusu wewe na kwa sasa ni "mumeo".

  Pole dada kwa uliyopitia, HOngeara sana kwa ulichofanikisha maishani. hakuna kitu kigumu maishani kama kupoteza wazazi kama ulishinda hayo na haya na hakika utashinda. Mshirikishe Mungu kwa kila ufanyalo.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda