Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, August 9, 2012

Kumbukumbu haiozi: Nyerere alipofungua Chuo Cha Uuguzi Haydom 1984

Nadhani Haydom ni moja ya maeneo ambayo baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa anapenda kuyazuru mara kwa mara wakati akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Mwaka. Mnamo tarehe 15 Septemba 1984 kabla hajang'atuka madarakani Nyerere alitembelea Haydom lakini awamu hii alifika mahasusi kwa ajili ya kukifungua Chuo Cha Uuguzi cha Haydom (Haydom School oh Nursing wakati ule Haydom Nurses Training School).

Wakati Chuo hiki ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa sana nchini na nje ya nchi kwa kutoa wauguzi makini na mahiri kikiadhimisha miaka 28 toka kufunguliwa rasmi na kikiwa kinaandaa harambee kwa ajili ya upanuzi wa chuo kwa kujenga maabara maalum ya kujifunzia wanafunzi na maktaba ya kisasa kwa ajili ya wanafunzi, Ohayoda inawaletea matukio yaliyojiri siku hiyo ambayo Nyerere alifika Haydom....endelea

Umati wa Watu ukiwa tayari kumsubiri Baba wa Taifa, hapa ni uwanja wa ndege wa Haydom

Taratiiibu ndege ikawaisili katika uwanja huo uliopo kitongoji cha Gangay

Hakukuwa na mbwembwe nyiingi za mapambo kama siku hizi, hapa ni jukwaa kuu akisomewa risala

Kwaya za shule za msingi na Chuo cha Uuguzi walikuwepo na bashasha kumpokea Nyerere kwa mara nyingine Haydom


Ilikuwa ni usawa "Mandolini" enzi hizo hakuna cha V8 wala VX, msafara ulikuwa mdogo siyo rais anakuja na msafara utadhani mashindano ya magari

Jukwaa kuu 

Hapa ni ndani ya Haydom Lutheran Hospital, mstari wa kushoto ni wanafunzi wa uuguzi na wa kulia ni wauguzi

Nyerere akitoka Ofisi ya chuo baada ya kusaini kitabu cha wageni akiambatana na Else Marie Voll aliyekuwa mkuu wa HSN


Nyerere alipata wasaa wa kuzunguka sehemu mbali mbali za HSN

Mchungaji Yotham Girgis naye alikwepo

Baada ya kumaliza zoezi hilo Baba wa taifa hakuwa na lingine zaidi bali alirejea uwanja wa ndege wa haydo tayari kuondoka, kama kawaida alikuwa mtu wa watu

Haikuwa kazi rahisi ku"host" ujio wa rais, Else Marie akiwa na hawa kina mama ambao ohayoda haijaweza kuwatambua

Ndege iliyombeba Nyerere ikiondoka katika uwanja wa haydom ikifuatwa na helikopta mbili za polisi

Helikopta si likatimu vumbi?

Hongera mama Else Marie kwa shughuli nzito

Hiki ndicho chuo cha uuguzi Haydom kwa sasa kinaitwa Haydom School of Nursing
Ndugu msomaji,  Haydom School of Nursing kinhistoria ndefu nchini, kikiwa ni moja ya vyuo bora zaidi vya uuguzi nchini na sasa kipo katika mchakato wa kubereshwa zaidi ili kiweze kutoa wauguzi bora zaidi nchini. Unaweza kutuma mchango wako kupitia accounti zifuatazo:


HAYDOM LUTHERAN HOSPITAL
HAYDOM SCHOOL OF NURSING
NBC (1997) LIMITED, ARUSHA BRANCH
USD ACCOUNT NUMBER 078105000359
SWIFT CODE: NLCBTZTX

au

HAYDOM LUTHERAN HOSPITAL
HAYDOM SCHOOL OF NURSING
NBC (1997) LIMITED, ARUSHA BRANCH
TSH-ACCOUNT NUMBER 078103000903

na
HAYDOM LUTHERAN HOSPITAL
HAYDOM SCHOOL OF NURSING
NBC (1997) LIMITED, ARUSHA BRANCH
REVOLVING FUND ACCOUNT NUMBER 014103013852
BANK SWIFT CODE NLCBTZTX
Au waweza kupata habari zaidi kwa kuwasiliana nao kupitia
HAYDOM SCHOOL OF NURING
P.O. 9001 HAYDOM
MBULU MANYARA— TANZANIA

Telephone: 027 2533322
E-mail: haydomnursing@haydom.co.tz


1 comment:

  1. Ahsante sana kwa taarifa nzuri.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda