Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, August 31, 2012

Kuelekea Haydom Cultural Festivals: Waandishi wa Habari na Wanafunzi watembelea Haydom Cultural Center

Zikiwa zimebaki siku chache kufikia Tamasha la kwanza kabisa la utamaduni kufanyika katika mkoa wa Manyara na mikoa ya Jirani, Waandishi wa Habari kutoka ITV, Habari leo, Jambo Leo, Majira na Business Times walitembelea Kituo kujionea maandalizi kwa ajili ya tamasha na pia wanafunzi zaidi ya 100 kutoka shule mbalimbali hapa Haydom nao walitembelea kituo na kupata fursa ya kujionea mambo mbalimbali. Tamasha hili litakalozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Elaston Mbwilo litaambatana na Uzinduzi wa Filamu inayoelezea Historia, maisha na Hatma ya makabila manne yanayopatikana katika eneo la Haydom, zoezi la uchangiaji damu, mashindano ya riadha na ngoma za asili. Tamasha hili si la Kukosa kama upo maeneo ya Haydom na jirani 
"Banner" la Tamasha likiwa tayari kwa matangazo, bango hili litaonekana Haydom, Mbulu, Babati, Karatu, Katesh na Kiomboi
Waandishi wa Habari Julieth Peter (kushoto) na Mary Margwe (wa tatu kushoto) wakipata maelekezo kutoka kwa Herman malleyeck (wa tatu kulia) huku Febronia, Janeth na Timotheo wakisikilizaInterview na waandishi wa Habari mbele ya kamera ya ITV na Charles Masayanyika


Usipimie hilo pozi ndani ya "Hanang'wenda", utamtaka Febro


Mbele ya nyumba ya wadatooga, waandishi wakiwa makini kupata maelezo kuhusu Habisyanda na Habardanga
Curator wa 4CCP Elifadhili Noah Genda akitoa maelezo kuhusu 4CCP kwa wanafunzi


Walimu waliokuja na wanafunzi, Hapa ni kwenye pavilion ya 4CCP

Sehemu ya wanafunzi kutok shule mbalimbali hapa Haydom wakipata maelezo kutoka kwa elifadhili (hayupo pichani). Hawa watakwepo kwa wingi kwenye Tamasha

Mwalimu Pastor Justo Madangi akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo ya wanafunzi


Sijui alikuwa "ameconcentrate" peke yake pembeni wakati wa ziara hiyo.


Haya ni baadhi ya matukio yanayojiri katika viwanja vya 4CCP Haydom tayari kwa ajili ya Tamasha hili kubwa zaidi katika mkoa wa Manyara litakalowashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yetu. Ohayoda inawakaribisha wadau wote kuwa sehemu ya Historia hii muhimu katika jamii yetu.

"INUKA, MAANA SHUGHULI HII YAKUHUSU WEWE, NA SISI TU PAMOJA NAWE; UWE NA MOYO MKUU, UKAITENDE"  Ezra 10:4

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda