Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, August 3, 2012

Know Your Personality, Build Your Value-Je, Melankokoli anaweza kuishi na watu Vizuri?

Na Nelson Faustin JR Psy.
.
U-hali gani mpenzi msomaji wa OHAYODA, ni matumaini yetu kuwa unaendelea vizuri na Mungu wa mbinguni anaendelea 
kukutunza kila iitwapo leo.

Niwashukuru wale wote ambao wamekuwa wakitupigia simu kutu shauri, kutupongeza na hata kutukosoa katika kuhakikisha kuwa makala hii na blog hii inafikisha ujumbe ambao tuliudhamiria.

Baada ya kujifunza mengi katika kumfahamu Melankoli, leo tumalizie sura hii ya mwisho kwa kumsaidia melankoli njia madhubuti za kumfanya awe bora zaidi kwani yeye ni mtu mwenye thamani sana licha ya mapungufu yake kwani mengine yanaweza yakapunguziwa makali kwa kumpatia huyu mtu mbinu bora za kuweza kuishi na watu.

Tuamini kuwa, Hakuna mwanadamu ambaye ni vigumu kuishi naye, bali kila mmoja ana mapungufu yake lakini kwa nia njema kabisa mtu anaweza kujifunza na kujiweka katika namna bora zaidi ya kuweza kuishi na watu.

Hii kwa wale ambao wamepata nafasi ya kujikubali kuwa wao ni Mamelankoli na kwa sababu hiyo, Dondoo zifuatazo ambazo ni za kawaida tu ni kama zifuatazo.
 
If some one gets to bear with what and who you are, 
You'll have to thank God sana.(nelly)

 • Kwanza, tambua thamani iliyopo katika utu wa watu wenye haiba au tabia  (personality) tofauti na ya kwako.
 • Ndugu, acha Ubinafsi.
 • Jitahidi kutokuweka vinyongo moyoni kwa kuwasamehe wengine punde tu ukasirishwapo bila ya kuuliza maswali mengi ambayo hayatakupa majibu.
 • Kubali mabadiliko pale inapobidi, acha kuamini kuwa wewe ndo mwenye mawazo ya mwisho na ni lazima wengine wakufuate, kwa hivi utaboa ndugu yangu.
 • Jifunze kuwa na usalama wa ndani kutokana na vipawa ambavyo Mungu amekujalia bila ya kuangalia kuwa nani atakupinga kwani kwa kufanya hivi umeacha kufanya mambo mengi sana...
 • Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo na ni bayana ya yasiyoonekana, maana hii lazima wakati mwingine uwe nayo, hii itakufanya uwe na imani kwa Mungu na zaidi sana utaweza kuepuka mashaka ya maisha yajayo hata kama changamoto zipo si zako peke yako.
 • Kubaliana na dhana kuwa, si kila mtu anaweza kutenda, kufikiri au kufanya uonavyo wewe, hii inakugharimu na itaendelea kukugharimuu tena sana usipokubali kubadilika.
 • Jifunze kuomba msamaha kwani kwa kufanya hivi si kwamba unakuwa mjinga bali unakuwa katika upande salama zaidi kwani hupotezi kitu kwa kuwa mnyenyekevu na kukubali kuwa umekosea.
 • Pa kusema sema ila pa kukaa kimya kaa kimya japo usikae kimya sana.
 • Usichoke kwa haraka hasa unapotakiwa kutumia muda wako au nguvu zako katika jambo fulani kama vile Mahusiano. Jifunze kuvumilia do not be so mechanical.
 • Usibishane sana ili watu wakukubalie, cha msingi bisha kidogo tu kama ukweli upo upo tu na utajitenga na uongo daima.
 • Usiwe na tabia ya kujitenga bali tenga muda kwaajili ya watu wengine kwani unawahitaji watu kwaajili ya maisha yako.
 • Ndugu yangu, maswala ya kisheria na mahakama ni mazuri sana ila mara nyingi huathiri mahusiano yetu kama binadamu, ukiweza kujitenga nayo, please jizuie japo najua ni ngumu.
 • Acha kusingizia wengine na kuona kuwa wewe hukosei bali wengine ndo wanaokosea tu, kaa mbali na tabia hii, kubali kuwa you are also weak.
 • Najua maswali yako matano ya ndani ambayo ni WHY, WHO, WHERE, HOW and WHEN lazima yajibiwe lakini si lazima yajibiwe kila mara, punguza maswali, hata kama ni lazima kujua kwa undani lakini kuwa na kiasi, bila hivyo unaboa ujue.
 • Tumia vipawa vyako bila kuwabania wengine.
 • Unauwezo mkubwa sana wa akili yaani personal IQ, kwa hili unapaswa kujitahidi katika taaluma yako na ufanye vitu ambavyo ni vya hali ya juu (aim High and think Big) ili usije ukapata msongo wa mawazo yani depression kutokana na kufanya vitu ambavyo ni kinyume na uwezo wako wa ndani (to avoid underperfoming which may bring you to depression)
Kwa ufupi mbinu hizi zitakusaidia, yapo mengi sana ila jitahidi kuwafahamu watu wanaokuzunguka na uishi nao kwa amani japo sijasema ukubaliane na kila kitu bali toa maamuzi fasaha na yenye tija kwako na kwa wote wanaokuzunguka.
...Juma lijalo tutajifunza Koleriki kwa sehemu zote kama ilivyokuwa kwa Sangwini na Melankoli.

NB: OHAYODA kama kioo kitatenga somo maalumu kwaajili yako la kuwagawa wanadamu katika makundi makuu mawili yaani:- BINADAMU WEMA NA WAOVU. Tukumbuke kuwa binadamu wote tunatabia za asili.


NB: Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu hapo juu kabisa ili kupata tulipoanzia hadi tulipo. 
 
Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
 
No Body Is Perfect, Who are you to Judge others?


KAMA KAWA,, MUNGU AKUTUNZE....
0753-038005
sonnelly06@gmail.com                                       (We are little Beings, trying to give you the little we have)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda