Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, August 1, 2012

(Know Your Personality) Japo Melankoli ni Watu Wenye Tabia Ngumu sana, ila Unaweza Kuishi Naye vizuri.

Na Nelson Faustin JR Psy.
Nianze kwa kuwashukuru wote ambao wamekuwa wakifuatilia makala hii ya IJUE HAIBA YAKO tangu tulipoanza kwa kuchambua kundi la watu wenye tabia za SANGWINI na hata sasa tunapoingia katika sehemu hii ya mwisho ya Namna ya kuishi na Melankoli na  pia kumsaidia melankoli ili aweze kuishi katika jamii bila kero.

Kwa kuwa udhaifu si dhambi bali ni asili, katika uasili wake tunaweza sasa kujifunza njia bora za kuweza kuchukuliana na kila tabia ya mtu jinsi alivyo, "trust me It is possible" labda ukatae kuamua kuishi na watu vizuri. Nngoja nikwambie, kuna watu wanaona ufahari sana pale wanapokuwa wanaishi bila amani na watu, embu jiulize ni kwa nini????...Neno la Mungu linatualika kila mara, kuwa ,"Tafuteni kuwa na AMANI na watu wote na huo UTAKATIFU ambao mtu hawezi kumwona Munga bila kuwa nao", Sasa kwa nini wengine wako bize kutatuta fujo na vurugu na watu wengine? Kwanza hii inarudisha maendelao nyuma na pengine tunafupishiana maisha bila kufahamu.
 
If some one gets to bear with what and who you are, 
You'll have to thank God sana.(nelly)

Aliye Melankoli na asiye melankoli asome hapa kwa umakini mkubwa.
 • Ili kuweza kupata taarifa au feedback toka kwa melankoli, Jitahidi sana katika kila jambo kutoa maelezo ya kina ili usimpe nafasi ya yeye kujiuliza maswali yake ya uchambuzi ambayo ni WHY? WHO? WHERE? WHEN? and HOW? kwasababu lazima atakuuliza hata kama unachomwambia kina umaana.
 • Hata kama hukubaliani naye, usimnyenyekee sana bali heshimu nafasi yake ya utendaji au usemaji.
 • Tambua bidii na juhudi zao kwani bila ya kufanya hivyo utamfanya avunjike moyo na hata kama amefanya vibaya, Give appreciation and encoragement with smooth supervision.
 • "Mpangilio" ni hitaji lao la msingi sana, jitahidi kuheshimu mpango wao wa vitu na kazi bila kuwavuruga vuruga na pia Jitahidi kuweka kila kitu katika mpangilio wake.
 • Kama boss wako, mzazi, mlezi au mkubwa wako ni MELANKOLI na upo chini ya maongozi yake, jitahidi sana kufanya mambo kwa utaratibu na kwa ukamilifu wake kadiri ya uwezo wako wote, kumbuka hii sio nidhamu ya woga bali mbali na kufanya kazi kwa ufanisi pia inakuwezesha kuepuka migogoro, kumbuka hawa ni "Perfectionists".
 • Katika mazungumzo ya kawaida tu, usimwone kero kwa maswali yake mengi na hata mengine hayana tija, bali wewe mpe majibu kwa upole na kwa ustaarabu na hekima. ukianza ubishi tu, basi umevunja mazungumzo afu si ajabu akaweka kinyongo...hawa wajamaa bhana....
 • Ndugu yangu, chukua muda kutafakari jambo kabla ya kumshirikisha vinginevyo anaweza kukuboa japo jambo lenyewe kwako ni la maana. NB: Japo si wote lakini wengi huamini kuwa kila kitu wanakifahamu, wewe ni nani umshirikishe na si yeye kukushirikisha? Lakini ukiona atakuboa na kukukatisha tamaa, Usimwambie.
 • Kwa kuwa si wepesi kusisimka kwa haraka kutokana na jambo fulani, jaribu tu kumwelewa kwani wala si kwamba wana maringo bali kwa asili huchelewa sana kukimbilia jambo tofauti na kina sangwini.
 • Kama Melankoli ni mwenzako wa ndoa au mtu wako wa karibu, msaidie kutokuweka maumivu moyoni kwa kujenga mazingira ya Ukweli na Uwazi baina yenu.
 • Akibahatika kuyafahamu maeneo yake dhaifu basi mpe nafasi ya kuyafanyia kazi, ukimlaumu au ukimkaripia tu, Umemmaliza. Hii inawahusu sana wale ambao ni wazazi, maboss, welezi au wenzi wa melankoli.
 • Japo sometimes ni ngumu lakini jitahidi kuwasiliana naye kwa kuzingatia sababu za msingi na hoja zenye mshiko. (Communicate with facts and not empty words).
 • Usimwingilie sana au kumchimba chimba saaana, huwa ni wasemaji kwa kiasi na hawapendi sana kuweka mambo yao hadharani, kwa kumchimbachimba saaaaaana utasababisha akuweke kando, kumbuka, hii ni kwa sababu hawana usalama wa ndani (internal Peace).
 • Let them think and come up with standing decisions. Usim-buruze.
 • Kama wewe ni kaka, dada, mlezi, mzazi, na unauhakika mtoto uliyenaye ni Melankoli, basi mhimize asome hasa masomo ya sayansi na mhimize afanye vitu vya kutumia akili kwani kwa kumuanzishia hivi ataweza kumuandalia maisha mazuri yasiyo na msongo wa mawazo au migogoro.
 • Tutajadili hili wakati wa kuangalia makuzi sahihi ya mtoto sawasawa na tabia zake za asili.
Mpaka hapo tumejaribu kuona angalau mbinu chache za kuweza kuishi na melankoli, kipindi kijacho tutamwambia melankoli aishije katika jamii?

Baada ya hapo tutamjadili FLEGMATIKI kama tulivyofanya kwa Sangwini na Melankoli. Tukumbuke kuwa katika yoote ambayo tunajifunza si kwamba sisi tunajua sana bali kile kidogo tunajaribu kukushirikisha na kama unafahamu zaidi tunahitaji mchango wako. 

Somo hili ni mahususi kwa familiya, makazini, mashuleni, vyuoni, kambini na sehemu yoyote ambayo ina mkusanyiko wa watu. Tumia dakika tano hadi kumi na tano kuweza kutambua kundi la tabia ya mtu fulani ili ujue utaishi  naye kwa namna gani.

Zaidi ya yote tujitahidi kuishi kwa hekima na kwa kuheshimiana na kumpendeza Mungu, kila mtu aone UTU ndani ya mtu mwingine "regardless of who you are"  
(Kila mtu ANAPASWA KUSEMA HIVI)

Tukumbuke Kuwa...
"Kwa namna fulani unaweza kuona kuwa wewe ni MELANKOLI ila kuna baadhi ya dondoo za tabia tumeainisha hapa na wewe hauna,...KATIKA SOMO HILI LA HAIBA TUNAJARIBU KUCHAMBUA TABIA ZA ASILI ZA BINADAMU KATIKA MAKUNDI HAYA MANNE YANI SANGWINI, MELANKOLI, KOLERIKI NA FLEGMATIKI ila kutokana na mabadiliko ambayo mwanadamu anapitia katika mchakato mzima wa kukua na maisha kwa ujumla kama vile kubanwa na sheria za dini, kazi, sheria za nchi, tamaduni nk, au kutokana na majukumu, hali ya maisha, ushawishi utokanao na watu wanaokuzunguka, nafasi yako katika jamii nk..unajikuta unajenga mtu wa tabia fulani kwani kila binadamu anayetazamia mazuri hufanya mazuri ili kupata mazuri na kwa kufanya hivi hujikuta akijenga tabia za aina mbali mbali ambazo ni nzuri zinazokuweka katika hali ya kuonekana huna udhaifu wowote"

NB: OHAYODA kama kioo kitatenga somo maalumu kwaajili yako la kuwagawa wanadamu katika makundi makuu mawili yaani:- BINADAMU WEMA NA WAOVU. Tukumbuke kuwa binadamu wote tunatabia za asili.

BAADA YA SOMO HILI LA HAIBA, TUTAJIFUNZA MASOMO MENGINE KWA KUJIBU MASWALI YAFUATAYO.

 1. Kama mzazi, Kuna Ulazima wa Kufahamu Tabia/Haiba ya Mwanangu? Kama Inatofautiana na yangu Nifanyeje?
 2. Hivi kwa nini baadhi Watu Waliopendana sana huwa Maadui wakubwa sana Baada ya mahusiano yao kuvunjika? (utapata na ushuhuda wangu hapa)
 3. Kwanini Wasichana Wengi WALEO wanakuwa na mawazo ya kukataa kuolewa tangu wakati wakiwa na umri wa miaka 16+?
 4. Je, kuna Uzuri au Ubaya wowote wa mahusiano ya kimapenzi wakati wa UANZAFUNZI wa ngazi yoyote? (Tutapata kuona shuhuda za mahusiano yaliyodumu hadi ndoa na zilizovunjikana na kuleta hasara kubwa sana)
 5. Kwa nini wanaume wengi leo wana Hofu kubwa kuhusu kuoa?
 6. Je, kuna umuhimu wowote wa Msamaha katika jamii?
 7. Itakuwaje kama ndoa ni ya watu wenye haiba za tabia tofauti kwenye makundi tofauti kama vile sangwini na Melankoli, au sangwini na sangwini, au ya flegmatiki na koleriki, nk?Je wanaweza wakaishi pamoja? Na Je, zinadumu?
 8. Tutajaribu pia kuangalia mwanzo na hatma ya "life style ya Usharobaro", na Je, ina sababu zozote za kisaikolojia? Na je walio wa hulka hii Je, ni Masangwini, Makoleriki, Mamelankoli au Maflegmatiki? 
Tunaamini utanufaika sana na safu hii..........

NB: Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo. 
 
Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake yeye mwenyewe.
 
No Body Is Perfect, Who are you to Judge others?


KAMA KAWA,, MUNGU AKUTUNZE....
0753-038005
sonnelly06@gmail.com


(We are little, trying to give you the little we have)


Tuonane Ijumaa.................................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda