Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, August 31, 2012

KAMA WEWE NI MWANADAMU MWENYE TABIA YA KOLERIKI, MAKALA HII ITAKUSAIDIA ILI UWE BORA ZAIDI.


Na Nelson Faustin JR Psy.
Katika makala hii leo tumalizie kujifunza tabia za wanadamu waliopo katika kundi la koleriki, Baada ya kujifunza kwa undani sifa njema za koleriki, mapungufu yake sasa leo tumweleze koleriki namna bora ya kuishi na watu ili aweze kuishi vizuri. Tunajua fika kuwa Koleriki ni mtu ambaye tunamhitaji sana katika jamii, lakini bila shaka una vitu ambavyo huna budi kuvifahamu katika kujua ni kwa jinsi gani unatakiwa kuongeza thamani yako katika jamii. Huna haja ya kuwa kero katika jamii bali unatakiwa kufahamu kuwa maisha yako ni kwaajili ya wengine. Inahitaji kuwa na unyenyekevu ili kufahamu fika ni njia gani utumie katika kuishi na watu vizuri.

Dondoo zenyewe ni kama ifuatavyo:-
 • Kama wewe ni Mwanamke  na unajifahamu kuwa wewe ni Koleriki, zingatia sana kuwa na nafasi ya unyofu moyoni, unyofu wako ndo utakusaidia kuishi vizuri na mume wako na zaidi sana katika kuwalea watoto.
 • Boresha sana ustadi wako wa namna ya kuishi na watu, usikubali kabisa kuishi na watu kama wanyama, zingatia sana utu uliopo ndani ya kila mtu.
 • Sifa ya kuwa Koleriki ni nzuri sana, na anahitaji zaidi kuitumia kwa mtazamo chanya ili wengine wafurahie kuwa na wewe na wanufaike na kile ambacho unakifanya.
 • Kwa kuwa wewe ni kiongozi kwa asili, fanya hima utumie nafasi yako, si kwa kuwakandamiza wengine bali kwa kuzingatia kuwa wewe kama binadamu unaongoza binadamu wengine.
 • Kuwa na mpangilio na ufanye kazi kwa kufuata hatua fulani. Kulipua kutakusababishia hasara, kumbuka kuwa, Harakaharaka haina baraka.
 • Lugha ya Koleriki ya mawasiliano ni kali sana katika hili unapaswa kufahamu kuwa kila unalolisema lina madhara kwa makubwa sana kwa wanaokuzunguka, kabla hujaongea jitahidi kuhesabu maneno yako kichwani kabla hujanena kwani unaweza ukawaweka watu mbali na wewe. 
 • Weka imani kuwa, watu wengine wanathamani kama wewe, wape nafasi na wao ya kujieleza pale wanapoona kuwa kuna jambo ambalo halijakaa sawa.
 • Elewe kuwa si kila mara unahitaji kutumia kanuni katika kufanya mambo, kuna wakati mwingine ambapo unahitaji kuangalia uhalisia na mambo jinsi yanavyotakiwa kuwa hata kama kanuni hazitapata nafasi yake.
 • Pokea changamoto na kuzifanyia kazi, acha kuwa "much know" kwani mwisho wa siku utaachiwa kila kitu ufanye peke yako na kumbuka kuwa kidole kimoja hakivunji chawa.
 • Ukitaka kuishi na kina SANGWINI AU MELANKOLI vizuri, basi hakikisha kuwa kila wakati unatambua uwepo wao na pia unafahamu mahitaji yao ya hali na mali katika maisha.
 • Usikate tamaa pale ambapo hakuna mtu wa kukushukuru au kukutia moyo kwani, fanya kwa bidii, baadaye wataona.
Mpaka hapo, tumefikia mwisho wa sehemu hii ya tatu ya "Ijue Haiba yako", kipindi kijacho tutajifunza kuhusu Flegmatiki na tabia zake.

BAADA YA SOMO HILI LA HAIBA, TUTAJIFUNZA MASOMO MENGINE KWA KUJIBU MASWALI YAFUATAYO.

 1. Kama mzazi, Kuna Ulazima wa Kufahamu Tabia/Haiba ya Mwanangu? Kama Inatofautiana na yangu Nifanyeje?
 2. Hivi kwa nini baadhi Watu Waliopendana sana huwa Maadui wakubwa sana Baada ya mahusiano yao kuvunjika? (utapata na ushuhuda wangu hapa)
 3. Kwanini Wasichana Wengi WALEO wanakuwa na mawazo ya kukataa kuolewa tangu wakati wakiwa na umri wa miaka 16+?
 4. Je, kuna Uzuri au Ubaya wowote wa mahusiano ya kimapenzi wakati wa UANZAFUNZI wa ngazi yoyote? (Tutapata kuona shuhuda za mahusiano yaliyodumu hadi ndoa na zilizovunjikana na kuleta hasara kubwa sana)
 5. Kwa nini wanaume wengi leo wana Hofu kubwa kuhusu kuoa?
 6. Je, kuna umuhimu wowote wa Msamaha katika jamii?
 7. Itakuwaje kama ndoa ni ya watu wenye haiba za tabia tofauti kwenye makundi tofauti kama vile sangwini na Melankoli, au sangwini na sangwini, au ya flegmatiki na koleriki, nk?Je wanaweza wakaishi pamoja? Na Je, zinadumu?
 8. Tutajaribu pia kuangalia mwanzo na hatma ya "life style ya Usharobaro", na Je, ina sababu zozote za kisaikolojia? Na je walio wa hulka hii Je, ni Masangwini, Makoleriki, Mamelankoli au Maflegmatiki? 
Tunaamini utanufaika sana na safu hii..........

NB: Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA au JINA LA HAIBA/TABIA FULANI kama vile Koleriki, Melankoli au Sangwini" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo. 
 

Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu, ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
Unajitambua? Au Unaishi tu kwa sababu siku zinaenda?

KAMA KAWA,, MUNGU AKUTUNZE...0753-038005
sonnelly06@gmail.com 
(We are little Beings, trying to give you the little we have)

Tuonane Jumatatu...............................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda