Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, August 23, 2012

Kama viongozi wa Tanzania wa Leo na wa kesho, Tunajifunza nini kwa Hayati Meles Zenawi na Ethiopia kwa ujumla?Ni kweli kuwa leo tarehe 23 August 2012 ni siku ambayo si njema sana kwa wananchi wa nchini Ethiopia kwani yule aliyekuwa kiongozi tegemezi kwa sasa hayupo tena na itabaki historia tu na yale aliyoyafanya yatazidi kubaki tu kama kumbukumbu ya yake.

Nimekaa na kutafakari sana nikaona kuwa, japo si kitu chema sana kimewatokea wenzetu lakini hatuna budi kusema "Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe". Pamoja na yote, tunakitu cha kujifunza kama watanzania kutokana na hali halisi ya nchi ya Ethiopia ikilinganishwa na Tanzania hasa katika nyanja za kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla.

Historia yake kwa ufupi ni kwamba, Meles Zenawi Asres alikuwa waziri mkuu wa Ethiopia tangu 1995 hadi alipofariki 2012. Tangu mwaka 1985,alikuwa mwenyekiti wa Tigrayan Peoples' Liberation Front, chama cha Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front alizaliwa May 8 1955 huko Adwa, na kufariki 20th August 2012 huko Brussels. Alimuoa Azeb Mesfin na walifanikiwa kupata watoto Senay Meles Zenawi, Marda Zenawi, Semhal Zenawi, alisoma Addis Ababa University (1974), Erasmus University, Open University. 
Ethiopia ni nchi ambayo ipo katika changamoto kubwa sana kutokana na kwamba hali ya hewa ambayo inaathiriwa sana na hali ya jangwa tofauti sana na nchi ya Tanzania ambayo kila uchwao tunaimba wimbo wa kwamba "hali yetu ya hewa, mali ya asili na amani tuliyonayo ni sababu tosha ya kutufanya tuwe na maendeleo ya hali ya juu zaidi ya tulipo". Kumbe nadhani tatizo hasa si "location" bali "how best do we use the location?", na hasa "who can make a good plan for this location?". 

Kwa aya hiyo tunagundua kuwa, Hayati Meles Zenawi licha ya changmoto za dini na za kimazingira zilizoko Ethiopia, alisimama kidete kama kiongozi wa nchi kuhakikisha kuwa nchi yake inasimama imara kiuchumi. Kwa taarifa tu ni kwamba mwaka 1990 Meles Zenawi alikuwa kiungo muhimu sana cha kuondoa udikteta na kuleta demokrasia ya kweli kwa viongozi wa kizazi kipya wa afrika, hii ilimpandisha chati sana katika nyanja ya uongozi.

Ethiopia ni chini ya utawala wa Hayati Meles Zenawi wamefanikiwa sana kuwekeza katika miundo mbinu na katika ushindani wa kibiashara kama vile kilimo cha maua licha ya hali ya jangwa ambayo ipo katika pembe ya Afrika, lakini sis bado kilimo kwanza hakijaleta matumani kama ambayo tuliyategemea. Mbali na hapo licha ya kwamba uchumi wa Etihiopia hautegemei mafuta licha ya kwamba sisi inasemekana kwamba tunayo lakini hakuna uchumi wake ulipanda hadi kufikia asilimia saba (7%) mwaka jana. Japo uchumi wake uliathiriwa sana na ukame wa kutisha mwaka 2002/3 lakini kwa miaka sita mfululizo uchumi wake umekuwa ukipanda kwa wastani wa asilimia kumi na moja (11%) na mipango mingi waliyonayo ili kukidhi mahitaji ya watu milioni 84.

Hata kama ni kidogo lakini ni mara chache sana utapata kusikia kashfa za ufisadi wa viongozi, na hata kama kuna migogoro hasa ya wakulima, walimu na wengineo lakini bado kuna njia sahii zinazotumika katika kutatua matatizo yao tofauti ya njia ambao Tanzania tunazitumia, kiukweli zinasikitisha sana.

Kwa viongozi waliopo na kwa wale ambao tunakuja kwaajili ya kulikomboa hili taifa, hatuna budi kutoa kipaumbele kwnza kwa kuwa wazalendo, na kutanguliza maslahi ya nchi mbele, pia ikibidi basi tufunge mkanda japo kwa miaka miwili na haya ni maamuzi magumu ambayo serikali itabidi kuyafikiria kwani kwa hali ilivyo ni kama vile uchumi unahamia kwenye asasi binafsi kiasi kwamba, Serikali inakosa meno katika kuwakemea. Tukumbuke sakata la mafuta jinsi ambavyo serikali yetu ilikuwa nyonge dhidi ya makampuni yanayo simamia mafuta. Kwa hali hii ya uchumi tutabaki tukisema kuwa, "it is only the strongest shall survive" na hapa tunamlenga mtu mmoja mmoja ambapo asilimia kubwa ya watanzania itaendelea kuwa masikini. Tutaimba sana kuwa sisi ni masikini lakini bila viongozi imara, wenye hofu ya Mungu na wenye mapenzi mema na nchi yao, tutabaki kulaumiana na kuonana kama vile kila mtu ni kisirani kwa maendeleo taifa hili ndio maana tutaanza kutafutana badala ya kutafuta maendeleo.

Ni vizuri kuwa wapo viongozi ambao wanajitahidi kweli kutimiza majukumu yao lakini kwa kweli bado safari ni ndefu kwani bado idadi ya viongozi ambao hawafanyi kwaajili ya taifa na wala hatujui wanafanya kwaajili ya nani. Sisi tunaotarajia kuingia ikulu, tuanze kwa kujifunza kwa ndugu yetu Meles Zenawi alipoitoa Ethiopia hadi hapa ilipo japo si sana lakini tuna mahali pa kujifunza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda