Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, August 6, 2012

Ijue Haiba Yako - Sura ya Tatu - KOLERIKI (Know Your Personality)

Na Nelson Faustin (Meku)

KOLERIKI - Utangulizi.
Karibu tena na tena mpenzi msomaji wa makala hii ya IJUE HAIBA YAKO (Know Your Personality) katika sura hii ya tatu tukiwachambua wanadamu wenye tabia za kundi la KOLERIKI.

Baada ya kujifunza mengi katika makundi mawili yaliyopita, yaani Sangwini na Melankoli leo tunapata fursa nyingine ya kujifunza tabia za watu waliopo kwenye kundi la KOLERIKI.
Tutatumia Mwongozo ufuatao.
 1. Utangulizi.
 2. Sifa Njema za KOLERIKI (strengths of Choleric)
 3. Mapungufu ya KOLERIKI (the weaknesses of a Choleric)
 4. Jinsi ya kuishi/kuchukuliana na KOLERIKI (how to live with a choleric)
 5. KOLERIKI anawezaje kuishi katika jamii? 
 6. Mwisho.

1. Utangulizi.

KOLERIKI NI MTU WA AINA GANI?
Kwa asili kila binadamu ana hulka na tabia ambazo Mungu alimuumbia na kutokana na hilo tunajifunza namna ambavyo wanadamu wamegawanywa katika makkundi makuuu manne. Hapa sote tunajifunza moja kati ya makundi magumu sana kuishi nayo kwa jinsi tu walivyo umbwa na Mungu.

Kwa utangulizi tu ni kwamba, kwa lugha ya wenzetu waingereza tunaweza kuwaita watu hawa "the tough Beings"/mechanical people. Maana halisi ni kuwa, watu hawa ni watendaji au watu wa kazi zaidi, hata kama ana kamwili kadogo kama cha Nelson ila ni watu wa kazi. Hii haiwafanyi kuwa wakamilifu ila inawafanya wawe watu ambao "they make things happen and they do not watch things happening".

Ready to Dare.
Kwa asili mtu yeyote ambaye ni Koleriki utamtambua kwa hitaji lao la msingi ambalo ni "matamanio ya kufanikiwa kwa gharama yoyote ile hata kama itagharimu maisha ya mtu" (by any means possible). Katika kutimiza azma yao ya kufanikiwa huwasababisha watu wengine wawaunge mkono hasa kwa kutumia ushawishi wenye vigezo tofauti na sangwini, lakini pia hata ikibidi kwa kulazimisha kwa kuwaburuza wengine ili mradi wanachokitaka kifanikiwe. (udikteta)

Kwa asili, ni vigumu sana kwa wao kuishi kwa amani na Melankoli kwani Melankoli si mtu wa kushinikizwa bali koleriki ni washinikizaji wa mambo by nature. Mtu ambaye kwao ni vigumu kuishi nao pia ni Sangwini ambaye kwa asili anaonekana kutokuwa serious na mambo. Usirious wa Koleriki ni Mateso kwa sangwini, hii humfanya Sangwini aone kama vile anaburuzwa na anafanywa kuwa mnyonge, badala yake Sangwini humkimbia mtu huyu. 


Kwa mfano wakati wa mahusiano kabla ya ndoa, mvulana ambaye ni Sangwini akiwa na mahusiano na msichana ambaye ni Koleriki utaona tu kuwa wakati wa mahusiano yao hata kama wanayafurahia ila baada ya muda kwa kuwa mwanaume anatamani kupata nafasi ya kwanza lakini msichana kutokana na Ukoleriki wake hutokea kumburuza mwenzake, mahusiano haya mengi huishia kwa mvulana kutoa kauli kama vile, "mimi siwezi kukalilwa na mwanamke", au pia unaweza kusikia, "yule mwamke ni kama bondia bwana mi siwezani naye", au "kabla ya ndoa tu ananiburuza hivi, huko ndani si ndo nitakuwa mume bwege kabisa? we better break up", au "atakaye mwoa mtu fulani lazima awe na roho ya bati sana" au pia, "siwezi kuoa mwanaume mwenzangu" (kwani wengi ni wababe kama wanaume) nakadhalika. Hii hutokana na utofauti uliopo baina ya watu hawa, ndio maana inashauriwa sana watu Makoleriki waoane wenyewe kwa wenyewe, au kama Koleriki atamwoa Flegmatiki basi waoane kwani Flegmatiki ndo wale walio wanyone kama tutakavyojifunza katika sura ya mwisho ya somo hili.

Kwa Koleriki Hii si Ajabu.
Kutokana tabia zao za asili, Makoleriki wengi huishia kuwa viongozi wa kisiasa, wanajeshi, madalali wakubwa, wanasheria, wahandisi, mafundi wa mashine ngumungumu nk, hii inatokana na kuwa, wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi ngumu ngumu tu hata kama si za kutumia akili kwani wao nguvu hutangulia akili katika utendaji wao. Kwa mfano ni mara chache sana wanaweza kuwa madaktari kwani udaktari ni kazi inayohitaji sana uangalifu wa hali ya juu. Koleriki akiwa daktari anaweza kuishia kumuumiza mgonjwa zaidi badala ya kumsaidia. Hali kadhallika, Koleriki hawezi kuwa mwalimu hasa wa shule ya Msingi au sekondari kwni ataishia kuwadunda watoto wa watu bure. Kwani wana kauli kama vile:-
 • Kama unaona huwezi acha.
 • Hapa kazi tu.
 • Liwalo na liwe.
 • Kitaeleweka tu.
 • Mtu asinibabaishe, nimeshaamua haibadiliki.
 • Ukichezea ukuta lazima uumie.
 • Haniambii mtu kitu hapa. nk
 NB: Koleriki si lazima awe na umbo kubwa (bonge), tabia yake tu humfanya kisaikolojia aonekane baunsa au pande la mtu hata kama ni mdogo na mwembamba. Utamtambua kwa Maneno na matendo yake.

Na Hawa wajamaa ni wababe sana, yani ukitamani ugomvi, mtafute Koleriki uone madhara ya kuukimbilia mzinga wa nyuki ambao asali yao imerinwa.
(Unadhani Huyo Mbwa Kapenda kukaa hapo?)

Nikutakie ila la kheri,

Tuonane Jumatano katika kujadili sifa njema za Koleriki.

Usisahau
Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo leo, tumeshajifunza HAIBA kuu mbili.
 
 
Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
Unajitambua? au Unaishi tu kwa sababu siku zinaenda?
                                                                         
                                                                     

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda