Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, August 30, 2012

Hofu kuu yatanda Haydom: Mfanyabiashara atekwa na watu wasiojulikana

Gari lake latelekezwa porini likiwa na funguo bila tatizo

Simu yake yatumika kutoa taarifa

Wananchi watishia kuchoma kituo cha Polisi

Na Amani Paul na Mary Margwe
Qorong'ayda-Haydom
Mfanyabiashara Hhando Samo wa kijiji cha Hayderer tarafa ya Haydom wilayani Mbulu usiku wa kuamkia juzi alitekwa na watu wasiojulikana na kutokomea kusikojulikana huku wakilitelekeza gari aliokuwa akiliendesha katika msitu wa Ilongero mkoani Singida.
Tukio hilo limegusa hisia za wananchi wengi wa tarafa ya Haydom hasa baada ya polisi kutuhumiwa kutokutoa ushirikiano walipopelekewa taarifa na hivyo kushindwa kufanikisha kupatikana kwa Bw. Hhando.

Wananchi wa Tarafa ya Haydom Wilayani Mbulu,Mkoani Manyara  wametishia kuchoma moto kituo cha Pilisi Haydom kwa kushindwa kuwajibika pindi wanapokelekewa taarifa mbalimbali za uharifu.
Tuhuma hizo zimeelekezwa kwa Jeshi polisi wa kituo kidogo cha mjini Haydom kwa kile walichokidai kutowajibika  kikamilifu kwa askari polisi ,ambapo walidai huenda wanashirikiana na majambazi kuteka watu na kuwaibia.
Aidha hali hiyo imejitokeza jana wakazi walipokua kwenye kikao cha kujadili namna ya kupatikana kwa mmoja wa wafanyabiashara maarufu wa mjini Haydom Bw.Petro Samo (40)  maarufu kwa jina la Hando,aliyetekwa juzi Agosti 28 ,mwaka huu,majira ya saa  5: 45 za usiku huko  katika eneo la korongo la Qorong’aida  wakati alipokuwa akielekea nyumbani kwake Haydarer.

Katika tukio hilo zaidi vijiji 11 kati ya kata 4 za Haydom, Maghang, Getarer na Maretadu, wanaokadiliwa kufikia watu wapatao 3000 walikusanyika katika makundi matatu tofauti ili kujadiliana namna ya kumpata mfanyabiashara huyo ambaye kabla ya tukio hilo alitokea Mkoani Singida akiwa na wenzie wanne, wengine ni Bw.Justine Masuja, Bw.Peter Tahani pamoja na kijana wa kazi wa Bw.Masuja.

Kwa upande wa wananchi hao walidai kuwa hadi sasa hawaoni umuhimu wa kuwa na kituo cha polisi cha hapo Haydom kwa kuwa hawana ushirikiano  na wananchi hata kidogo, huku wakisema kuwepo kwa kituo hicho kimeongeza matukio mengi ya ujambazi badala kupungua.

Aidha walimuomba Inspekta General wa Polisi Said Mwema kuhakikisha anaingilia kati tatizo hilo linalofanya na polisi wa Haydom, ambapo wamedai wabadilishwa wote isipokuwa Mkuu wa kituo Anania Mshana kuwa hana tatizo lolote bali anachafuliwa na vijana wake wa chini .

Kadhalika walimuomba Saidi mwema kuwa asipochukua hatua yoyote juu ya polisi hao watachoma moto kituo hiko ama polisi hao warudi uraiani na raia wachukue nafasi kama polisi jamii, kwani hakuna kazi wanayoifanya zaidi ya kula rushwa kwa kukamata pikipiki na magari  kwani wameshindwa kufanya doria ambayo ingeweza kupunguza hali ya uhalifu katika maeneo hatarishi mjini hapo.

Kwa upande wake mkazi Haderer Bw.Samweli Bayo alisema ni vema polisi hao wote wakabadilishwa kwa kile alichokidai kuwa wamekosa nidhamu katika kazi yao wamebakia kulala tu kituoni hapo badala ya kufanya kazi iliyowaleta pale Haydom.
“Kwa muda aliotekwa mwenzetu  na taarifa ilikwenda haraka sana kituoni hapo na iwapo wangechukua hatua za haraka wangefanikiwa kuwatia nguvuni hao majambazi waliomteka mwenzetu, lakini walisingizia mafuta  na bila kutoa ushirikiano wowote juu ya tukio hilo” alisema Bw.Bayo.

“Leo tuna siku ya tano hatujalala wala kula chakula kuna mwenzetu mmoja alikamatwa na kukatwa katwa mapanga na kulazwa juzi ndio limetokea hili la huyu mwenzetu Bw.Hhando la kutekwa na kuporwa hadi sasa hatujui kama mzima ama la, tunazidi kuomba Mungu azidi kuweka Baraka zake awe mzima” alisema Bw.Melkizede Emmanuel anayetoka Kijiji cha  Hayderer  anakotoka mfanyabiashara huyo.

 Kwa upande  wake Diwani wa kata ya Geterer Bw.Petro Lory  alisema Tarafa ya Haydom suala la majambazi kwa Haydom limekithili kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linatishia amani kwa wananchi kwa ujumla.
Bw.Lory alisema kwa kawaida mfanyabiashara huyo huwa ana chukua mazao kwa wananchi na kwenda kuuza kwa bei ya juu kidogo ukilinganisha na walanguzi wanaonunua mazao kwa wananchi, na hivyo kurudi kuwapatia wananchi fedha zao.

“Kwa mujibu wa diwani anasema, mke wa huyo mfanyabiashara alitumiwa sms kutoka kwa mume wake(huyo mfanyabiashara) inasema nimetekwa na majambazi nikiwa na sh. Mil. 84.7 na gari langu liko Ilongero Mkoani Singida” alisema Diwani huyo.

Aidha kufuatia meseji hiyo wananchi walipata mwanga wa kukodi gari na kufuatilia gari hilo na kufanikiwa kulipata mahali palepale ilipoelekeza meseji ile ana sasa liko katika kitu cha polisi cha mjini Haydom.
Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha polisi Haydom Anania Mshana alikiri kupokea taarifa hiyo  na kusema kuwa walichokieleza wananchi hao kuwa polisi haikutoa ushirikiano si kweli kabisa kwani polisi hao ndio waliongoza msafara kutoka hapo Haydom  huku gari lao likiwa limejaa wananchi na hadi kufika lilikoachwa gari hilo la mfanyabishara na kurudi nalo katika kituo cha polisi Haydom.

“Kama nyie wenyewe waandishi wa habari mlivyotukuta katika eneo hilo tupa kwa ajili ya kulinda hali ya usalama wao, wanavyolalamika juu yetu si kweli kabisa hata viongozi wa kata, Tarafa na hata Wilaya wanafahamu juu ya uwajibikaji wetu, licha ya kuwa wanadai kuwa polisi hawatoshi hili sio kwetu tu karibia kila mahali” alisema Mshana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda