Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, August 2, 2012

HANANG WATUMIA "DRIPU" KUKABILIANA NA UKAME.

Na Mary Margwe,Hanang
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa Kapteni Honest Mwanossa amefurahishwa na ubunifu wa ustawishaji wa miti kwa kutumia matone ya maji  kwa chupa maarufu kama (dripu)  mradi unaoendelea katika Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara.

Mradi huo ulibuniwa  katika shule ya sekondari Bassodesh  kutokana na mazingira ya hali ya ukame ,ili kuwezesha miti kustawi  kikamilifu,ambapo kapteni Mwanossa alisema mradi huo unatakiwa kuigwa hasa katika sehemu zenye mazingira ya ukame kama hayo.

Kapteni Mwanossa alisema Tanzani kuna sehemu mbalimbali ambazo wananchi wanashindwa kupanda miti   ama maua kutokana na mazingira ya ukame,hivyo kutokana na ubunifu uliofanywa na shule hiyo utakua ni mkombozi kwa maeneo mengi ya Tanzania.

 “Hadi hivi sasa kuna watu wanashindwa kupanda miti ya matunda hata kupanda maua kutokana na hali ya mazingira ya ukame,kwa hiyo sasa tumepata ufumbuzi,kwani huu utakua ni mradi wa kwanza toka nianze mbio za mwenge Mei 11,mwaka huu hadi sasa hivi”alisema Kapteni Mwanossa.

Aidha  kufuatia tukio hilo alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya HanangBi.Christina Mndeme na kumtaka kuhakikisha elimu hiyo inasambaa katika maeneo yote ya Wilaya yake ili kupata mazingira mazuri na endelevu kwa jamii.

Alisema elimu hiyo sio tu kuishia katika mashule bali itolewe kwa jamii nzima ili kuweza nao kuboresha mazingira yao.

Kwa mijibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi.Mndeme alisema aina ya miti iliyopandwa katika eneo hilo la sekondari ya Bassodesh kuwa ni pamoja na mjohoro mwekundu ,mjohoro mweupe,jacaranda,mfurufuru,
msederela ,mipera ,Bouganvilea na “Teminalia”

Aidha Bi.Mndeme alifafanua kuwa jumla ya sh.mil.  3,260,000 ,zimetumika kama gharama ya kuipanda na kuitunza ,ambapo kati ya fedha hizo hhalmashauri iliweza kuchangia sh.60,000 ,huku michango ya wananchi ikiwa ni sh.mil3.2.

Hata hivyo mkuu huyo alikili kutoa elimu hiyo kwa wananchi wanaowazunguka  shule hiyo na nje ya shule hiyo,ambapo jumla ya miti 400 imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang tayari  imepandwa, mara baada ya shule hiyo kuonyesha nia ya kulinda mazingira ya shule.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda