Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, August 8, 2012

Endelea Kuwafahamu Watu na Tabia Zao - (strengths of a Choleric)

Na Nelson Faustin Nderemo
Ni Jumatano nyingine ambayo Mungu ametupa nasi tuna kila sababu ya kufurahi na kushangilia ndani yake. Unayepata nafasi ya kufuatilia somo hili la HAIBA kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa, naamini unapata nafasi ya kujitambua ili sote kwa pamoja tupate fursa ya kujenga jamii yenye amani, tija na mafanikio kwa kila mmoja, usisahau, migogoro hurudisha nyuma juhudi za maendeleo.

Leo tushirikishane juu ya sifa njema za KOLERIKI. Baada ya kuona utangulizi katika sehemu hii, leo tujifunze juu ya sifa njema za koleriki kwani sawasawa na watu wengine yeye naye ana mazuri yake na hapa tunaangalia japo dondoo chache kumuhusu yeye.
 • Ni viongozi / watawala wazuri sana.
 • Koleriki ni mtu ambaye hana aibu.
 • Wanapenda sana kuwa katika nafasi za juu sana (High Table).
 • Wanajali kazi zaidi kuliko maneno matupu.
 • Kazi au Shughuli isiyokuwa na matunda au tija kwao ni upotezaji wa muda.
 • Tofauti na sangwini, Melankoli na Flegmatiki, Koleriki anauwezo mkubwa sana wa kupambana na Upinzani kutoka kwa wanaompinga hata kama ni kwa muda gani.
 • Ni watu wenye nguvu na hitaji kubwa la mabadilliko hata kama itawagharimu maisha yao na baadhi ya watu wengine.
 • Ni wasimamizi wazuri kwa wale wasiopenda kufanya kazi kwa ufanisi (ni kiboko ya wavivu)
 • Ni wahamasishaji wazuri sana hasa katika michango na hata katika maumivu ni watu wazuri sana katika kuhamasisha wengine nao wakamfuata.
 • Ni watu wa mabibu mkononi. Si watu wa kujiandaa ili waseme kitu fulani, tofauti na Melankoli ambaye hawezi kusema kitu bila ya kukihakikisha kwanza.
 • Koleriki ni mtu ambaye anauwezo wa kutafuta majibu ya matatizo kwa haraka sana bila ya kujiulizauliza maswali mengi (fast trucking)
 • Ni watu wa kuweka malengo na kuyasukuma hadi yakamilike.
 • Koleriki wengi wanauwezo wa ajabu wa kukabiliana na dharura za aina yoyote.
 • Ni watendaji wazuri sana wa kazi kwa kasi ya ajabu.
 • Koleriki anasifa kuu ya kuweza kubadilika kwa hali hali yake ya moyo na akili kutokana na mazingira na watu anaokutana nao katika nyakati fulani fulani. 
 • Ni wagumu sana kudhibitiwa. 
 • Koleriki ni mtu ambaye ni mwepesi sana kuchangamkia fursa anazokutana nazo, mara nyingi wanafanikiwa si kwa sababu wao ni wema sana bali ni watu wanaojua kuchangamkia ishu mbalimbali.
 • Japo koleriki pia anakosea, lakini mara nyingi huona kuwa ana jukumu la kuwasahihisha wenzake kwani hawana aibu ya kwamba mtu atawaonaje.
 • Koleriki ni kiongozi kwa vitendo na si maneno matupu tu.
 • Baada ya kufanya tathmini, Koleriki hutoa jibu la moja kwa moja na lenye uwazi. Kwa mfano Hapana, Haifai, Ni sawa, Sitaki, Haiwezekani, Inawezekana, Umependeza, Umefanya vibaya, Unanuka nk.
 
NB: Koleriki si lazima awe na umbo kubwa (bonge), tabia yake tu humfanya kisaikolojia aonekane baunsa au pande la mtu hata kama ni mdogo na mwembamba. Utamtambua kwa Maneno na matendo yake.


Nikutakie ila la kheri,

Tuonane Ijumaa katika kumalizia kujadili sifa njema za Koleriki.

Usisahau
Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo leo, tumeshajifunza HAIBA kuu mbili.

Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
Unajitambua? Au Unaishi tu kwa sababu siku zinaenda?
               
(Unadhani Huyo Mbwa Kapenda kulala alipo? Ukimuuliza Koleriki atakujibu)
(We remain little Beings, trying to give You the little we have, Receive it Please.)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda