Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, August 3, 2012

AFYA KWANZA-USHAURI JINSI YA KUISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI


 Na Bearice Githiri-HLH 
Ndugu wasomaji wa ohayooda nina imani kila mmoja wetu anafahamu jinsi virusi vya ukimwi vinavyopatikana na hata athari zake. Kuwa na virusi vya ukimwi sio mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa maisha mapya ya uangalifu zaidi. Unapopata virusi vya ukimwi kuna kipimo vya kuchunguza   kinga ya mwili, kitaalam kinaitwa CD4 count.

Kama CD4 count ipo chini ni lazima uanzishiwe dawa za kurefusha maisha  au dawa za kudumaza virusi  (ARV).
Ni vyema wanajamii tuwasaidie waliopatwa na huu ugonjwa kwa upendo kuzingatia  ushauri ufuatao:


Ø   Jikinge na maambukizi mapya kwa kutofanya ngono zembe- tumia kinga (condom) wakati wote kaa mbali na vitu vyote hatarishi vinavyoweza kukuambukiza virusi vya ukimwi.
Ø   Fuata masharti ya dawa. Zingatia saa za kumeza dawa, fika kliniki siku za kufuata dawa bila kuchelewa na hudhuria mafundisho kila mara .
Ø   Hakikisha unahudhuria kliniki kila baada yamiezi mitatu au sita kuchunguza kinga yako –CD4.
Ø   Pata mlo kamili na lishe bora. Wanga ,protini na vitamini katika kila mlo bila kusahau maji.
Ø   Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara kabisa.
Ø   Zingatia usafi wa mwili pamoja  na mazingira ya nyumbani kwako.
Ø   Usijinyanyapae mwenyewe kwa kujiona mgonjwa na kujitenga na jamii. Unapofuta masharti unakuwa mtu wa kawaida na huna sabau yoyote kujitenga na jamii. Fika katika kazi zozote zinazohusu jamii ikuzungukayo na jiunge na makundi katika jamii.

Wote tumeadhirika na janga la ukimwi, kama sio mimi ni ndugu yangu au rafiki yangu. Tuepushe maambukizi mapya!!
Tusiwatenge wala kuwanyanyapaa walioathirika kwani inawezekana kesho ni kwako kama hutakuwa mwangalifu.

Inawezekana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda