Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, August 10, 2012

AFYA KWANZA: MAZOEZI KWA AFYA YA MOYO


Na Beatrice Githiri-Haydom

Mazoezi ni jambo la muhimu ila wengi wetu wanaliipuuzia sanaIli moyo uwe na afya unahitaji lishe sahihi na mzoezi ya kutosha. Kama tayari moyo umedhurika ni muhimu kumwona daktari ili kupanga nae aina ya mazoezi pamoja. Makala ya leo inkupa namna ya kuuweka moyo katika hali ya afya kwa Kufanya mazoezi.

Anza na zoezi rahisi zaidi kwako
Jaribu kutembea kwa dakika tano na kwa mda mfupi ndani ya nyumba au barazani kwako. Ongeza mda hadi kumi na kwendelea.

Jaribu mazoezi mara kwa mara
Jitahidi dakika 30-60 mazozi laini hadi magumu.

Jaribu mazoezi aina tofauti
Changanya  mazoezi ya kujinyoosha, endurance(aerobic) na strengthening(weight training) na anza kwa warm up, workout level na cool down katika kila zoezi.

Badilisha mazoezi ili usijiumize
Unaweza jaribu kubadilisha aina ya mzoezi kwa mfano kuogelea, kuendesha baiskeli
na kutembea.

Usizidishe mazoezi
Anza taratibu na uongeze mazoezi kadri ya uwezo wako wa kustahimili ili mwili uweze kupumzika na kupata ahueni. Utakapo pata maumivu ni vizuri uache.

Ongeza shughli zako za kila siku
Jaribu Kufanya shughli za nyumbani kama kulima, kudeki na kupanda ngazi ili kupunguza lehemu(cholesterol)  na kuboresha  afya yako. Badala ya kwenda na gari hadi nje ya ofisi, egesha mbali ili upate nafasi ya Kufanya mazoezi.

Kama una swali maoni au ushauri tuandikie hapo chini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda