Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, August 24, 2012

AFYA KWANZA: MAUMIVU YA MGONGO


Na Beatrice Githiri-HLH
Hii huwa ni hali ambayo humfanya mtu kujisikia uchovu sana mara baada ya kufanya kazi inayohusisha mgongo. Hali hii inaweza ikatokana na kusimama kwa muda mrefu, kuinama kama vile ukifua ama kudeki nyumba, kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu kama vile makarani ofisini ama madreva wanaoendesha safari ndefu.
Maumivu ya mgongo huanza taratibu sana kiasi kwamba utahisi uchovu wa kawaida ambao utaisha mtu akisha pumzika baada ya kazi. Hali hii ya uchovu ikiendelea sana huwa inasababisha maumivu makali sana kwa eneo la chini la mgongo, maumivu ambayo huwa kwa misuli.
Mtu akipuuza haya maumivu, athari zake ni kubwa mno kiasi kwamba maumivu husambaa mpaka kwenye kisigino cha mguu mmoja na kisha mtu anashindwa kutembea ama hata kulala kwa mgongo ama kuulalia upande huo.

KINGA NA MATIBABU.
Inawezekana kuzuia hali hii isitokee kwa kuhakikisha kwamba mtu anabadilishia mtindo au mfumo wa kazi. Iwapo kazi ya mtu ya mtu inahusu kusimama kwa muda mrefu, pasiwe na kusimama kwa eneo moja tu bali kutembeatembea ili uzito wa mwili usambae kote kwenye miguu na mgongoni kwa usawa. Ikiwa kazi ni ya kuketi sana, aidha mtu asimame mara anapohisi uchovu ama ganzi ikiingia kwenye “makalio”  ama abadilishie pozi alilokaa nalo.
Kama ishatokea kwamba maumivu yapo, inahitajika mtu afuate matibabu bila kupuuza.
Matibabu yake huwa kwa ujumla ni kuchua eneo la maumivu mgongoni kwa mikono ama kwa mashine halafu kuna mazoezi yanayoambatanishwa kama matibabu ili kuimarisha misuli ya mgongo.
Kwa muda ambao matibabu yanaendelea, mhusika anashauriwa kama inawezekana kujiepusha na kazi ngumu ama apunguze ugumu wa kazi anayoifanya mpaka pale matibabu yanakamilika. Muda hasa wa matibabu unategemea ukali wa hili tatizo na muda ambao hii hali imekuwepo.
Ni hali ambao inatibika ingawaje pia inaweza kuzuilika. 

Mpenzi msomaji, kama unaswali au ushauri usisite kutuandikia au kuacha maoni yako hapa chini nasi tutayafanyia kazi. 
Ijumaa Kareem

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda