Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, August 10, 2012

4CCP kutoa filamu inayoelezea Historia, Maisha na Hatma ya Makabila ya Wahadzabe, Wairaqw, Wanyiramba na Wanyisanzu na Wadatooga mwezi September

Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni Haydom (Haydom Four Corners Cultural Programme-4CCP) kipo mbioni kutoa filamu inayoelezea Historia, Maisha na Hatma ya makundi manne ya lugha yanayopatikana katika eneo la Haydom mkoani manyara.

Uzinduzi wa filamu hiyo ni hatua moja mbele zaidi katika kuyafikia malengo ya kituo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2006 kikiwa na lengo la kuhifadhi utamaduni na kuurithishwa kwa vizazi vijavyo. Filamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa katika maonesho ya Utamaduni (Haydom Cultural Festivals) yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Kituo hicho kilichopo chini ya mlima Haydom nje kidogo ya mji wa Haydom.

Filamu hiyo ambayo ni muunganiko wa filamu nne ndani yake, ilianza kutengenezwa mwaka 2011 na uchukuaji wa picha umefanyika katika maeneo mbalimbali katika wilaya za Mbulu, Iramba na Hanang ambako makundi hayo manne ya lugha yanapatikana.

Akizungumza na Ohayoda mhariri mkuu wa filamu hiyo (Chief Editor) ndugu Pascal Oswald Kipenye alisema kuwa wadu wajiandae kupokea kitu kizuri kutoka kwa timu nzima ya Vantage Studios ambayo ndiyo waandaaji wa filamu hiyo iliyotengenezewa Haydom kuanzia mwanzo hadi mwisho (pre and Post Production).

Filamu hiyo imeandaliwa na Vantage Studios chini ya Executive Producer Amani Paul ambaye pia ni mmiliki wa Ohayoda, imetafsiriwa katika lugha za Kiswahili na Kiingereza pamoja na lugha za makabila husika ya Wahadzabe, Wanyiramba/wanyisanzu, Wairaqw na Wadatooga na itapatikana sehemu mbalimbali baada ya kuzinduliwa baada ya maonesho hayo.

Kukamilika kwa filamu hiyo kunatarajia kufungua milango kwa tasnia ya filamu hasa za kihistoria na za kielimishaji (documentary films) kufika vijijini na kuibua maswala mengi yaliyoko vijijini ikiwa ni pamoja na urithi mkubwa wa utamaduni na maliasili zilizoko vijijini ambazo zikipewa kipaumbele yatachangia katika kuleta maendeleo nchini na kuitangaza nchi yetu katika anga za kimataifa kupitia filamu.

Wakati huo huo wananchi mbalimbali wa Haydom na maeneo ya jirani wanakaribishwa kuhudhuria maonesho ya Utamaduni yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 6 mwezi September na kufikia kilele tarehe 8 mwezi huo huo katika viwanja vya kituo cha utamaduni Haydom. Maonesho hayo yataambatana na maonesho ya ngoma za asili kutoka kwa makabila 4, mashindano ya ngoma pamoja na mashindano ya nusu marathon ambayo yamegawanywa katika makundi 3 ambayo ni wazee wanaozidi miaka 50 ambao watakimbia umbali wa kilometa 2, watu wa rika mbalimbali km 5 na mashindano kamili ya nusu marathon ya km 21 ambapo washindi watapewa zawadi mbalimbali.

Kamati ya maandalizi inapenda kuchukua fursa hii kuwatangazia watu wote watakaopenda kushiriki katika mashindano ya marathon waandikishe majina yao katika Ofisi za kituo Cha Utamaduni zilizopo ndani ya Hospitali ya kilutheri Haydom na pia vikundi mbalimbali vya ngoma kutoka makabila ya Wanyiramba/wanyisanzu, Wairaqw, Wadatooga na Wahadzabe nao wanaombwa kujiandikisha ili kuweza kushiriki katika tukio hili la aina yake litakalofanyika kwa mara ya kwanza.

Maonesho hayo pia yataambatana na maonesho ya biashara kutoka kwa taasisi na makampuni mbalimbali yanayotoa huduma huku vijijini na yanatarajiwa kufunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara. Aidha kama wewe ni mfanyabiashara na unataka kushiriki katika maonesho haya wasiliana na kamati ya maandalizi au bofya hapa http://www.ohayoda.blogspot.com/2012/07/haydom-cultural-festivals-kufanyika.html utapata maelezo ya namna ya kushiriki.

1 comment:

  1. Kwa sisi tunaokaa mbali na Mbulu hiyo filamu tutaipataje bei ikoje. Mimi nakaa Tanga mjini.
    Reginald Tsafu.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda