Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, July 23, 2012

Wasemavyo wadau wa Facebook: Serikali inapoamua kwa makusudi kuwaibia Wananchi wake

Kufuatia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kubaini kuwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ipo hatika kufilisika kufuatia serikali kushindwa kurudihsha mikopo ya miradi mbalimbali iliyokopa kataika mifuko hiyo ukiwemo ule wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Wadau mbalimbali wamejitokeza kueleza hisia zao kupitia mtandao wa kijamii wa facebook, na hivi ndivo wasemavyo


When a Government deliberately plans to "rob" its own people.You ever thought this 'you don't get your nssf until you are 55' idea is by mistake??read this...

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uko hatarini kufilisika na kupoteza fedha za wanachama wake.

Hii inatokana na serikali kushindwa kurejesha katika mfuko huu, mabilioni ya shilingi iliyokopa au kudhamini katika miradi mbalimbali.
 ·  ·  · about an hour ago via mobile · 
 • Elizabeth SHe Ringo likes this.
  • Lorenzo Laigwannan 
   Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya 2010/2011, fedha za wanachama, hata katika mifuko mingine ya jamii, ziko hatarini kupotea.Mbali na NSSF, mifuko mingine inayotajwa kuwa katika hatari hiyo ni Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF); Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu (PSPF), Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).Kulingana na taarifa ya CAG, sehemu kubwa ya fedha za wanachama ambazo hazijarejeshwa, zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).Katika chuo hiki, NSSF peke yake iliingiza Sh. 234.1 bilioni. Mifuko iliyosalia ilitoa jumla ya Sh. 181.3 bilioni.Katika ujenzi wa UDOM, PPF ilitoa Sh. 39.99 bilioni, PSPF (Sh. 105.9 bilioni), LAPF (Sh. 22 bilioni) na NHIF (Sh. 13.4 bilioni). Fedha hizo na riba yake hazijarejeshwa.
   58 minutes ago via mobile · 
  • Lorenzo Laigwannan 
   Ripoti ya CAG, Ludovick Utouh, inasema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo, iliyochukuliwa au kudhaminiwa na serikali, ni kinyume cha sheria ya udhamini ya mwaka 1974.“Kutolipika kwa mikopo hii iliyodhaminiwa na serikali kunaiweka mifuko hii ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha uwezo wa mifuko kufanya uwekezaji zaidi,” anasema na kuongeza:“Kushindwa kulipa madeni taasisi hizi ambazo baadhi yake zilipata udhamini wa serikali, kunatia shaka iwapo upembuzi wa kina wa wakopaji ulifanywa na mifuko ya kijamii kabla ya kutoa mikopo hiyo.”Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau hakupatikana kwa maelezo kuwa alikuwa kwenye mkutano mkoani Mbeya.
   56 minutes ago via mobile · 
  • Fakihi Fadhili ‎@Lorenzo mimi naomba nikurudishe nyuma kidogo...hivi sheria zote si zinatungwa na Bunge? na kama jibu ni ndio hii sijaisikia ikajadiliwa bungeni au kuna exceptional? nataka ufafanuzi kabla sijaanza kuchangia mada.
   53 minutes ago · 
  • Lorenzo Laigwannan 
   Lakini Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume amesema mikopo kwa serikali imetolewa kwa uangalifu na inalipwa bila matatizo na kwa misingi ya kibiashara.“Mikataba ya kisheria imesainiwa kukidhi mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na iwapo itacheleweshwa…. Hakuna hatari yoyote ya fedha kutolipwa wala kupoteza fedha za wateja,” amesema Chiume.Lakini CAG katika taarifa yake ya kurasa 183, anasema, “Ukubwa wa kibiashara kati ya serikali na mifuko unatia shaka kutokana na kusuasua kwa serikali katika ulipaji madeni yake. Hii inahatarisha uendelevu wa mifuko hii.”Katika ukaguzi wake, CAG amebaini kuwa NSSF ilitoa Sh. 234.1 bilioni kwa mradi wa UDOM, lakini mkataba uliosainiwa ni wa Sh. 35.2 bilioni tu. Hii ni hatari kwa fedha za wafanyakazi na wastaafu.
   52 minutes ago via mobile · 
  • Mosseley Mkoba 
   Broo dc country bana ni balaa tupu!!!mlala hoi kila leo amekua ni dekio la walio madarakani.yani huwezi amini michango ya wanachama inwapa mtaji mifuko ya pensheni bila mashart, wanawekeza wanaearn na kulipana marupurupu manono.At the same...See More
   49 minutes ago · 
  • Jaffary Juma hii pia ilipita bungeni....labda kwa sababu wao haiwahusu (wanakula sijui gratuity) ndio maana hawakuitolea mijicho
   32 minutes ago · 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda