Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 12, 2012

Vurugu za Uchaguzi CCM-HAYDOM KATIKA PICHA.....

Wiki kadhaa zilizopita, zoezi la haguzi wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi tawi la Haydom liliingia dosari baada ya kukiukwa taratibu nyingi za uchaguzi hivyo kupelekea "vurugu" na kusababisha zoezi hilo kuahirishwa.
Katika uchaguzi huo, ushindani mkubwa ulikuwa kati ya mwenyekiti anayemaliza muda wake ndugu Diyamet na Yekonia Deles ambaye anakubalika zaidi na vijana ambapo kila upande ulikuwa unaushutumu upande mwingine kwa kuvuruga uchaguzi. Kati ya taratibu ambazo zilikiukwa ni kutokuwepo kwa orodha kamili ya wapiga kura na wapiga kura kuandikishwa hadi siku ya uchaguzi na baadaye zoezi hilo kusitishwa na kuelezwa kuwa ni wale tu wenye kadi za CCM ndio watakaopiga kura jambo lililozua tafrani kubwa sana hasa kwa kambi ya Yekoni Deles ikidai ni hujuma za Diyamet na kambi yake kwani utaratibu huo umekuwa ukitumiaka tawini hapo ikiwa ni moja ya njia ya kuwakaribisha wanachama wapya na kambi ya Diyamet wakidai kuwa kambi ya Yekonia imejaza mamluki.
Aidha katibu wa CCM wilaya ya Mbulu ambaye alikuwa mwangalizi wa uchaguzi huo naye alizua tafrani baada ya kusoma kanuni ya uchaguzi na kutangaza kuahirisha uchaguzi kuwa ulitakiwa uwe umeanza kabla ya saa 4 asubuhi na muda aliokuwa anaahirisha tayari ni saa 10 jioni.
"Kwa nini hakusema toka mapema kama kanuni inasema kabla ya saa 4?" alihoji mwanachama moja aliyekuwa na jazba ambaye hakutaka jina lake kuandikwa.
Katika hatua nyingine viongozi wa CCM walishindwa kutoa maelezo ya nani atakiongoza chama katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mwingine kwani uongozi uliopita ulikwisha kujiuzulu ili kupisha uchaguzi huo ambao haujafanyika.
"Mimi bado ni mwenyekiti na nitaendelea na kazi mpaka uchaguzi utakapofanyika" alisema Diyamet alipohojiwa na Ohayoda.
Naye ndugu Emmanuel Mighay ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Haydom alieleza kuwa "tawi litaongozwa na sekretarieti ya kata" mpaka uchaguzi utakapofanyika majibu yaliyozidi kuleta mkanganyiko chamani humo.
Uchaguzi huo hatimaye uliahirishwa kwa amri ya Afisa mtendaji wa Kata ya Haydom ndugu G. Isaay ambaye ndiye mwenye dhamana ya ulinzi na usalama katika kata hiyo baada ya kubaini uwezekano wa amani kuvunjika endapo uchaguzi huo ungefanyika.
Katika hatua nyingine, taratibu za CCM zinaeleza kuwa tawi linatakiwa kuwa na wanachama wasiozidi 600 na endapo watazidi idadi hiyo tawi hilo linapaswa kugawanywa na kuwa na matawi mawili. Mpaka wakati wa uchaguzi uliovunjika tayari kulikuwa na wanachama zaidi ya 800 walioandikishwa huku wengine zaidi ya 300 wakiwa wanasubiri kuandikishwa na kuzua sintofahamu ya Je Tawi litagawanywa?
Tawi la CCM Haydom linavyanzo vingi vya mapato yanayolalamikiwa kutafunwa na viongozi huku wananchi wengi wasiowanachama wa CCM wakihoji uhalali wa CCM kumiliki vyanzo hivyo vya mapato ambavyo vilikuwa mali ya kijiji wakati wa chama kimoja. CCM inamiliki maeneo "strategic" katika mji wa Haydom ambayo yamekodishwa kwa wafanyabiashara, minara miwili ya simu na vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vinadaiwa kufisadiwa na viongozi walioko madarakani.


Kutoka kushoto ni Godlove Mushi, John Massay, Mtoto wa Msindai,
Elifadhili Noah na G. Isaay kabla ya uchaguzi


Wapiga kura wakiwa eneo la tukio kabla ya uchaguzi
Viongozi wanaomaliza muda wao wakisoma repoti ambayo haikuwa na taarifa ya mapato na matumizi ya fedha kwa kisingizio cha "muda" haukutosha. Nadhani hata makaratasi yaliwaishia kuchapisha
Vigogo wa CCM wakifuatilia mchakato mzima
Diyamet na timu yake
Watu kibao
Emmanuel Mighay akitoa utaratibu wa uchaguzi kabla ya kuvurugika. Kushoto ni diwani wa Haydom ndugu Nasaeli Sulle na Kwa nyuma namwona kada maarufu wa CCM Haydom ndugu Kibonge

Huyu dogo alikaa mbele kabisa, sijui kama naye angeweza kupiga kura. "huwezi jua"
Watu wakiwa makini kufuatilia mchakato wakiongozwa na mhando

Ayubu akiwa na mtu muhimi sana kwa maisha ya mabachela wa Haydom maarufu kwa jina la Nyau. Itabidi tujue chanzo cha kuitwa Nyau ni nini....

Katibu wa CCM wilaya ya Mbulu
Mhando akieleza kutokurishwa kwake na jinsi mambo yalivyokuwa yakienda


HATUKUBALIANIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...mambo yakaanza kuvurugika
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata akaamua kuingilia kati na kuahirisha uchaguzi
Tafrani ikaanzaSijui anamwambia nini


Mzozo wa kutokuridhwa na yaliyojiri ukaendelea, huyu ni Ayubu akimzonga Emma MighayKatibu wa CCM wa wilaya naye alikiona cha moto mbele ya wanachama waliokuwa na hasira

Mama Kwini (Queen) naye hakuwa nyuma, sijui alikuwa kambi gani hahahaaa siasa zina raha yake


Huyu mama alikuwa akijaribu kumshauri Diyamet akae kimya asijibu shutuma zilizokuwa zikielekezwa kwake na watu


Huyu bwana mwenye fulana jeupe akamvaa Duyamet n kumtaka "wapinge" kama atashinda uchaguzi utakapofanyika tena akimtuhumu laivu kwa kukifisadi chama
Postamaster Samueli naye alikwepo eneo la tukio, haikufahamika alienda kupiga kura ama kushuhudia, pengine alipeleka "barua" hahahaaa
Makundi ya watu waianza kutawanyika


Viringi vya "much Know" vikaendelea chini ya mwenyekiti Yona Tikin ambaye ni kada maarufu wa Chadema aliyekuwa shuhuda, huku wadau wengi wakidi kuwa Chadema ilipenyeza mamluki ili kukihujumu CCM.

3 comments:

 1. i'm truly proud to call Haydom "HOME"
  Muhando you impress me.. Big up :)

  ReplyDelete
 2. God Bless you all

  I Lilly want to visit there one day and to learn everything over there... Somebody assist please!!

  ReplyDelete
 3. I hope Vurugu hazikuwa kubwa Sana za kuhatarisha Amani... Nimezipenda Picha Mkuu Nitapenda kutembelea Maeneo hayo Siku Zijazo... Rangi za Kijani na Njano zinapungua Miaka hii Nchini Tanzania kweli Watu wanahitaji Change...

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda