Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 12, 2012

Ujenzi mbovu wa miundombinu kwa fedha za umma

Na MM
Kuna mizani mpya na ya kisasa ya kupima uzito wa magari ukiwa unatokea chalinze kwenye Msata. Sikumbuki vizuri lakini nadhani ilifunguliwa mwaka jana na imefanya eneo lile kuvutia sana. Hivi majuzi nilisimama pale na nilishangazwa nilipoingia kwenye kile choo kilichoko pale ambacho nacho ni kipya na hakijatumia zaidi ya mwaka mmoja.

Kwenye picha nilizoambatanisha utaona kwa nje jengo la choo kile linaonekana zuri na jipya. Ila ukiingia ndani utashangaa kuona aina ya ujenzi na upigaji wa rangi ulivyofanyika. Tayari kimeoza na kinatia kinyaa utadhani kina miaka kumi au zaidi tangu kijengwe. Pamoja na uchafu wa hali ya juu, mambo ya maji yameharibika, rangi imebabuka na mfumo wa vyoo haufai kabisa

Je, haya nayo sio matumizi mabaya ya fedha za umma katika ujenzi wa miundombinu? Tanroad na wizara ya ujenzi hawajaona hili?

Ilinishangaza sana na nikavutiwa kupiga picha na kuchukua video clips

Sina hakika kama hii yaweza kuwa of interest kwa kuwekwa kwenye blogs zenu. Ikiwezekana bandikeni labda wahusika wataona na kuchukua hatu maana inatia aibu...na ujumbe umfikie Mzee Magufuli.

Ninaomba usibandike jina langu kwenye blog...yatosha kusema imetumwa na Mtanzania

Mungu awabariki

MM
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda