Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, July 2, 2012

IJUE HAIBA YAKO SEHEMU YA KWANZA: SANGWINI


 Na Nelson Faustin.
 Meku Mtanzania.


SANGWINI.

Sangwini ni mtu wa haiba gani?
Kwa jina la utani awaweza kufahamika kama watu wasiojali sana makuu, hawa ni wanadamu wa pekee sana kwani ni watu wenye furaha, anayependa kuchekesha, mtu wa watu wa kada zote, ni mtu anayependa kuburudisha sana na mara Ni mtu wa kuwa na uwezo wa kufanya jambo bila maandalizi na hii huwapa kujiamini kusikokuwa sawa.

Kwa nini sangwini ni sangwini? 
Kwa asili sangwine anasemekana kuwa na tabia njema sifuatazo
(The strength of sanguine) 

·        -Hapendi ubishi.
·        -Ni muwazi sana (super extrovert).
·        -Hajui kununa na mara nyingi haishiwi na maneno ya kuweka hali ya amani.
·        -Hapendelei kujitenga hasa katika kufanya kazi.
·        -Kwa asili si mtu wa kujiamini sana ila kutokana na hali yake ya uchangamfu huwafanya wengi kumwamini na kumpa nafasi katika utendaji.
·        -Ni mtu wa kupenda hafla na tafrija, kwao ni kusema maisha yawe ni hafla bila vipindi vya huzuni.
·        -Ni mtaalamu wa kuanzisha na kuendeleza mazungumzo na kuwafanya wengi washiriki.
·        -Anapenda sana kukaa na watu, kwa ufupi ni mtu wa watu.
·        -Ana nafasi kubwa sana katika jamii kwani hupokelewa kwa urahisi sana hasa na watoto.
·        -Ni mburudishaji mzuri sana, akiwepo furaha ni lazima iwepo.
·        -Akisimamiwa, huwa na utendaji wenye ufanisi sana.
·        -Anakasirika haraka sana ila ni wepesi katika kuacha hasira na kuachilia mambo.
·        -Ni mzuri katika kutawala mazungumzo.
·        -Anapenda kutumia sauti kubwa ili kila mtu asikie na kuwaamini.
·        -Anapenda sana urafiki na watu wengi.
·        -Anavutia watu  wengine kumwangalia na kumsikiliza.
·        -Ni mwepesi sana kujiinga na vikundi mbali mbali.ano 
·       -- Ni mwepesi katika kuwachochea watu wengine kufanya kazi au jambo Fulani mahali popote.
·        -Anapenda kufanya kazi za kujitolea hata bila malipo.
·        -Wanapenda kuwa maarufu.
·        -Kwa kawaida hana uchoyo.

Mpenzi msomaji wa OHAYODA naamini umepata kitu……kama wewe ni sangwini mshukuru Mungu, tutaendelea kipindi kijacho siku ya Jumatano katika kuangalia sifa njema za huyu mwanadamu aitwaye sangwini……Mungu akubariki sana…………….endelea kuifurahia blog yako pendwa…Mbiu ya haki.

Rai ya mwandishi: Kwa asili Mungu ametufanya tofauti kwa ajili ya sifa na utukufu wa Jina lake, Hivyo kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda