Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 26, 2012

Serikali Yetu, Tunaomba Mtukumbuke........Wasema Wazee Mashujaa...


NYUMBA YA BABU&BIBI
Samahani serikali,sikuingilii ila naomba tu kuuliza……………
Eti, hawa wazee mashujaa mnapaswa kuwatunza? Na Je, na wao Wanakudai? 

Nimejikuta nauliza haya kwani, jana tarehe 25 July 2012 ilikuwa siku ya mashujaa na tuliisherekea kwa amani huku tukitafakari kwa undani jinsi ya kuwa mashujaa katika jamii yetu kama njia ya kuwaenzi mashujaa wetu.

Katika pitapita zangu mjini nikapata taarifa iliyotoka kinywani mwa mashujaa wawili watatu akiwemo mzee Michael Mgasa na mzee Issa Nyamgosa ambao wamepaaza sauti zao toka Mara alikozaliwa Baba Wa Taifa kuomba kuiomba serikali iwalipe na taarifa kuwa watalipwa na serikali ya Uingereza imekuwa ni danadana tu.

Kama ni kweli, nainatoa rai yangu kwa serikali yangu tukufu kuwa, hawa wazee kilio chao kwa Mungu ni kikubwa sana na nadhani kwa imani yangu, razi yam zee ni laana na taifa linaweza kuingia katika mabalaa tukashindwa kujua chanzo, kumbe labda ni mambo kama haya ya hawa wazee, na hao ni wachache walioweza kutoa sauti zao na kwa muda mfupi zikasikika, naamini wapo wengi sana ambao bado wapo hai, Japo uwezo wa serikali ni mdogo lakini wanaweza KUKUMBUKWA.

SERIKALI INA MAJUKUMU HIVI.
Najua SERIKALI KAMA BABA, unamajukumu mengi sana kwani bado madaktari wanakushika shati, ajira kwa vijana ni bomu kwako, mafisadi nao hawaachi kukuandama, Rushwa, ajali za mara kwa mara, changamoto za baadhi ya viongozi wasiojali maslahi ya watoto wako, migogoro ya chini chini mengine usiyoijua na unayoijua, kuporomoka kwa thamani ya shilingi, changamoto za kisiasa, bodi ya mikopo ya elimu ya juu inakutazama, kesi za walimu na mengineyo mengi, unashindwa kujua namna ya kuwajibu.

RAI YA OHAYODA KWA SERIKALI.
Kama inawezekana, wapeni haki yao kwani siku zinavyo zidi kwenda wanazidi kupungua kutokana na umri. Ni rahisi sana kama serikali itaamua na kuacha kulimbikiza matatizo.

Ni hilo tu…………Samahani kama nakuingilia mheshimiwa serikali kwa sababu hata kama kuna mpango mahususi wa kuwasaidia labda hamjatuweka wazi….NAAMINI mtaifanyia kazi japo bajeti ya wizara ya mambo ya jamii, jinsia wanawake na watoto sidhani kama ilikumbuka…kama walikumbuka…NITAFURAHI SANA……….

Mbali na hoja hii kubwa, wazee pia walitoa rai kwa watanzania wote kuitunza wote kuitunza kwa hali na mali ambayo kwa nchi nyingine zinazotuzunguka ni kitu adimu sana. 

Wenu katika ujenzi wa Taifa…OHAYODA….


Baba samani kama nimekukosea, mi bado mdogo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda