Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, July 23, 2012

PICHA YA HAYDOM: 1970-2012

"Haydom is a miracle"..... Haydom ni muujiza"
Haya ni maneno ya Mama Kari kila alipokuwa akipita na kuwaaga watu mbalimbali wa Hadom na vitongoji vyake mwezi Mei akirejea kwao Mandal Norway baada ya kuishi Tanzania hususan Haydom tokea tarehe 10 Disemba 1961 (siku moja tu baada ya Tanganyika kupata Uhuru)
Tofauti na makazi mengine maeneo mbalimbali nchini, waanzilishi wa Haydom yaani wamishionari kutoka Norway walijenga Hospitali katika pori ambalo hakukuwa na matumaini ya kuwepo kwa maisha. Mbung'o na wanyama wa porini ndio waliokuwa wakitawala maeneo haya na walipewa eneo na familia ya mzee Munya eneo la kuanzisha hospitali, eneo alilowapa alikuwa analitumia kwa ajili ya kupumzishia ng'ombe wakati wa mchana na ndipo ilipo Medical Ward maarufu kwa jina "Old Ward" kwa sasa.
Kilichofuata baada ya Hapo ni historia, kutoka kuwa pori lisilo na tumaini la maisha leo hii Haydom ni Hospitali tegemeo kwa mamilioni ya wakazi wa Mikoa ya Manyara, Singida, Shinyanga na Arusha
Chini ni picha inayoonesha Haydom katika miaka ya 1970, kisha miaka ya mwanzo ya 2000 na Haydom hususani Hospitali ya Kilutheri ya Haydom ilivyo sasa.
Haydom miaka ya 1970

Haydom miaka ya mwanzo ya 2000

Haydom Ilivyo sasa 2012
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda