Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, July 23, 2012

PEOPLE IN THEIR DIFFERENT PERSONALITIES¤MELANCHOLY.

MELANKOLI
Na Nelson wa OHAYODA
MFANO WA MATUNDA YA MELANKOLI
Karibu tena mpenzi msomaji wa blog pekee ianyowika toka vijijini. Ni matumaini yetu kuwa umemiss mwendelezo wa masomo yetu katika safu hii ya watu na haiba zao, lakini kama kwa bahati mbaya ndo unajiunga nasi, hili ni somo la pili katika mfululizo wa somo linalohusu haiba na unaweza kutembelea blog yetu hii kwa kufahamu tabia za sangwini ambazo tulizianisha na namna ya kuishi naye. 

Baada ya kuona utangulizi wa mtu huyu aitwaye MELANKOLI ni dhahiri kuwa tunahitaji kumchambua ipasavyo ili kupata kufahamu huyu ni mwanadamu wa hali gani na tunawezaje kuishi naye ili hali tukijua kuwa sisi sote ni wanadamu na tunamapungufu japo tunahitajiana kila mmoja kwa nafasi yake.

Sifa njema za MELANKOLI ni kama ifuatavyo......

 • Wewe kama ni Melankoli, jifahamu kuwa una tabia ya kufikiri kuwa kila kitu kinapaswa kufanyika katika ukamilifu wake hata kama ni ngumu kiasi gani.
 • Tabia yako ya kufanya mambo katika mpangilio na kuweka vitu katika mpangilio ni sifa njema sana kwani inasaidia katika kutunza kumbukumbu vizuri.
 • Melankoli anahitaji sana maelezo ya kutosha kwani kwao la maana ni maelezo na si tu nguvu ya ushawishi. Kwa kawaida maswali matano ya msingi lazima ajiulize ambayo ni, NINI, KWA NINI, KIVIPI, NANI,  LINI ili kupata taarifa za kutosha.
 • Mara nyini si mtu wa kuendeshwa na hisia bali hufikiri kwanza.
 • Hana muda wa kupumzika kwani kila sekunde kwao ni ya kazi.
 • Una uwezo mkubwa sana wa kufikiri kwa marefu na mapana na kwa sababu hii huweza kujifunza masomo ya sayansi na yale ya kutumia sana akili tofauti na masangini wengi ambao wamesoma masomo ya sanaa-arts.
 • Ni wavumbuzi na wabunifu wa mambo hasa mashine ngumu na pia huwa na uwezo mkubwa wa kushika misamiti migumu inayotumika katika mashine hizo hata kama si wao wamezigundua.
 • Melankoli ni mtu wa kuishi kwa tahadhari na wana umakini mkubwa sana katika kufanya mambo.
 • Kiubinaadamu, ni muungwana na mkarimu sana.
 • Ana viwango vya juu sana katika utendaji kwani anapenda kila kazi ifanyike katika viwango vyao na si vinginevyo.
 • Tofauti na sangwini, Melankoli amejaliwa uwezo mkubwa sana wa kujitegemea mwenyewe bila ya mtu yeyote kumsaidia.
 • Uwezo wake wa kuchambua mambo humsaidia sana kutoingia katiak matatizo na migogoro isiyo ya lazima.
 • Ni mtu mwenye msimamo katika mipangilio aliyojiwekea kwani anaamini kuwa yeye ni kama yeye na alichonacho si rahisi kukipata kwa mtu mwingine.
 • Ni mchumi mzuri na mara nyingi hupenda vitu vya kawaida, kwake kuishi maisha ya kawaida ni suala la msingi.
 • Hawapendi sana kujionesha sana mbele za watu, japo wengine wanapenda sana sifa.
 • Ni MSEMAJI kuliko MTENDAJI.
 • Ni mtu ambaye akidhamiria jambo lazima likamilike.
 • Wanafanya kazi kwa usafi mkubwa.
 • Wanafanya mambo wakiongozwa na kusudi.
 • Ni mtu wa mawazo mapya kila siku.

Mpenzi msomaji.....yapo mengi sana lakini jifunze haya machache kwanza na kipindi kijacho tutaona tutamalizia sifa za melankoli ili tujifunze sasa mapungufu yake.

Kwa kawaida melankoli hujiona maalumu sana, si vema ila mshukuru Munu na ujue kuwa jamii inakuhitaji sana.

KILA LA KHERI,,,,TUONANE JUMATANO...........................................


1 comment:

 1. nimeipenda sana hiyo kaka Nelson.. kama inanihusu vile. nashawishika kusubiri kwa hamu sana hiyo jumatano.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda