Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, July 3, 2012

Papaa On Tuesday.....Liwalo Na Liwe, Likiwa Usiliogope
Wahenga walisema Lisemwalo Lipo, kama Halipo Linakuja, haijalishi ni lini lakini kama halipo kwa sasa linakuja siku moja itakuja kuwa kweli katika maisha yetu yale yanayosemwa. Biblia inasema katika Mithali, Lile Asiye Haki analoliogopa ndilo huwa linampata kwenye Maisha yake, sehemu nyingine inasema Ulimi ni kiungo kidogo lakini Ulimi ni noumaaaaaaaaa.

Nitoe pole za dhati kwa Dr. Mwanaharakati Steven Ulimboka kwa yale yaliyompata mpaka sasa, Nimshukuru Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania JK kwa hotuba yake ya Kuwataka Madaktari kurudi kazini huku "mchakato" wa huduma bora ukiendelea. Maisha Bora kwa Kila Mtanzania Yanawezekana.

Papaa On Tuesday ya leo inatokana na neno la Kawaida sana ambalo limekuwa likitumika katika Kutishiana, kupiga mkwara, ama kwa mtu ambaye amekosa suluhisho la jambo fulani katika maisha kisha anaamua "Liwalo Na Liwe'. Kauli hii ambayo imetolewa siku moja kabla ya Kutekwa na Kuteswa kwa Dr. Ulimboka bungeni na Waziri Mkuu kuwa mgogoro wa Madaktari ulipofikia "Liwalo Na Liwe". Inawezekana  alilisema kwa nia njema sana lakini, Ulimu huumba, Ulimi Unaua. Ukimwambia Mtu Nitakufanya Kitu mbaya ikatokea yule mtu amepata kitu kibaya maishani mwake basi jua kuwa katika Ulimwengu wa roho kuna kitu ulikiachilia kupitia kinywa chako.

Maneno yetu yanaweza kutugharimu siku moja sababu tulisema kwa kudhania tu ni kawaida, Ukimuona mtu anakutishia jua tayari ana kuogopa, na Kuogopa ni zao la hofu, na hofu inatoka kwenye moyo kama sio fikra za mtu, maana kimjazacho mtu moyoni mwake ndicho anachokisema, huwezi kuwa huogopi then ukamwambia Mtu Liwalo na Liwe, Huwezi kuwa umepata Suluhu ya Jambo then Ukasema Liwalo na liwe. Ukitamka Jambo Likiwa basi usiogope unapaswa kufurahia sababu ulilisema. Ila likitokea halafu ukaogopa basi ujue ulikuwa ni Mkwara tu unautoa ambao unagharimu maisha yetu ya baadae.

Wengi tuko hivi tulivyo pengine sababu ya maneno tuliyowahi nena ama kunenewa, wengine mpaka sasa hawajaoa ama kuolewa sababu ya yale waliyowahi yatamka ama tamkiwa, wengine biashara haziendi sababu ya yale tuliyowahi tamka ama tamkiwa, wengine tumekosana na Waume ama wake zetu sababu ya yale tunayoyatamka, wazazi na watoto wana ugomvi sababu ya maneno, mgogoro wa Madaktari na Serikali ni kwa Sababu ya maneno, hakuna kitu kinasubiriwa kwa hamu kwa Sasa kama maneno atakayoyatamka Dr. Ulimboka Mungu akimjaalia uzima. Rais juzi ameongea Kuwa anayeona mshahara mdogo aache kazi, maneno haya ya Liwalo na liwe, ya waziri Mkuu nayo yanatoa utata kwa kile kilichotokea.

Kuanza kutolea ufafanuzi Kauli zako zinapunguza integrity yako pia kwenye Jamii, Ndio yako iwe ndio na Sio yako iwe Sio, ukigombana na mtu kuwa makini sana na maneno unayoyasema kwenye maisha yako unaweza mpandikizia mtu mwingine maroho ya ajabu. Ukisema neno jua litakuwa kinywa huumba, ukisema hautazaa na hautazaa kweli, ukisema sijui kama ntaolewa ama kuoa itakuwa hivyo hivyo maana jambo unaloliogopa maishani hukupata sawa sawa na Kitabu cha Mithali.

Kuwa Mwangalifu unayoyasema na unayo nenewa, Unaongea nini kila Siku kwenye maisha yako. Ukiwa na Tabia ya kuzira na Kukasirika na kuongea maneno ya ajabu kuwa makini, uko hivyo ulivyo pengine kutokana na maneno uliyowahi nenewa na wazazi wako, boy friend ama girlfriend wako, Mchumba wako, ama boss wako ama mtu fulani na kitendo cha wewe kukubalia ama kuyakubali maneno hayo ndio maana uko hivyo. Inawezekana waliwahi sema maneno mazuri juu yako, kuwa wewe ni bright wewe unaweza, wewe ni Jembe ndio maana umekuwa kweli ulivyo, na inawezekana walisema maneno mabaya ndio maana umekuwa na maisha hayo, inawezekana waliwahi sema hauta fanikiwa, hautaweza kuishi miaka mingi lakini niseme jambo moja Yuko Mungu MKuu kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kwa Kusema Rais ni Dhaifu tusitegemee kabisa kuwa atakuwa Strong, Kwa kusema Liwalo na liwe, yanakuwa, tunaposema damu itamwagika ikianza msiogope, ukisema sijui kama ntaishi, ukianza kufa usipaparike, Ukisema Sijui kama Utafanikiwa ukiendelea kuwa masikini usishangae, Ukisema sijui kama utapiga hatua kwenda mbele basi usishangae, ukisema wewe kichwa chako ni cha panzi hakiwezi kubeba mambo makubwa basi akili zako zitaishia hapo hapo, Kila ambacho unakitamka kwa kinywa chako basi ujue utakula matunda yake.

Think Differently, Make A Difference 

Papaa
0713 494110

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda