Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 12, 2012

Papaa On Tuesday…….Ingawa Twateseka Mioyoni na Kutokuridhika na Tunayoyafanya Lakini Tunang’ang’ania Hapo Hapo.

Na Samuel Sasali a.k.a Papaa

Wapenzi wasomaji wa Ohayoda tunasikitika na tunawaomba radhi kwa kutokuweza kuwaletea habari na makala mbalimbali kama ilivyokuwa ada kutokana na sababu za kiufundi ziliokuwa nje ya uwezo wetu. Lakini pamoja na kuadimika hewani kwa siku kadhaa tumeona si vyema tukawakosesha wasomaji wetu makala wanayoipenda ya PAPAA ON TUESDAY japo leo si jumanne kama ilivyo jina la mada.

Ikiwa ni Jumanne nyingine Mungu amenipa nafasi ya Kukaa na kuandika Makala nyingine ya Papaa on Tuesday ya leo. Ni matumaini yangu ya kuwa hata wewe msomaji wangu kwa Neema ya Mungu uko Salama kabisa bukheri wa Afya.
Hakuna kitu bora sana kwenye maisha kama amani ya ndani, roho yako kufurahia jambo ama maisha unayoyapata, si kweli kila aliyeridhika ana amani ya moyoni, si kweli walio na kila kitu wana amani ya moyoni, si walio vijijini wana afadhari kuliko wale wa mjini, si kwamba kila aliye Mjini ana raha ya moyoni si kila anayefanya kazi ana amani ya moyoni. Kama mioyo ingekuwa ya vioo ndipo ambapo tungeshuhudia lumbesa ya huzuni iliyobebwa na mioyo ya watu.

Mungu ashukuriwe alitupa mioyo ya nyama isiyoweza kuonekana shida zilizobebwa na watu wala majonzi na huzuni za watu hao. Amani ya moyoni ni zaidi ya Mshahara wa fedha unayoipata, Amani ya moyoni ni zaidi ya ndoa za Maigizo zilizojaa mateso, amani ya moyoni ni zaidi ya kukaa kwenye nyumba yenye geti kubwa, amani ya Moyoni ni zaidi ya kufanya biashara ya mifugo ama mazao, wengi wamejitahidi kutafuta kila kitu kwenye maisha yao, ajabu pale walipovipata havijawa jawabu la kwenye maisha yao. Kuwa na amani ni zaidi ya tabasamu la kulazimishia kuonekana uko safi kumbe una kansa ya furaha inayokukula ndani yako.

Katika kuishi miaka michache hapa duniani nimekuja kutazama wengi wetu tunateseka kwa namna moja ama nyingine katika yale tunayoyafanya ama yaishi, tumekuwa haturidhiki na aina Fulani ya maisha ama kile tunachokipata lakini “no way out” tumeamua kuchagua “kuvumilia” hata yale yasiyovumilika katika maisha. Tumekubali kupokea manyanyaso, matusi, maonezi na dhuruma lakini tumeona bora tuteseke tubaki kuliko kutafuta ustaarabu, na tumekuwa na mawazo what if kama nikitoka nisipopata kile ninachokitaka.
Kuna wafanyakazi wengi sana walioajiriwa ndani ya mioyo yao hawapendi kazi wanazozifanya, by the way wanakwenda kazini basi tu sababu hawawezi kutoka hapo walipo, nimekutana na marafiki zangu ambao wanafanya kazi katika ofisi nzuri na mshahara mzuri lakini “hawana furaha”. Ukiwatazama wana kila kitu lakini ndani yao wanajua kabisa wanafanya kazi wanazozifanya sababu hawawezi kutoka hapo na wakipata sehebu bora zaidi wataenda, lakini hata huko nako wengine waligundua “fedha sio jawabu la mambo yote” Nimewahi kutana na watu hawalipwi fedha nyingi sana lakini wanafanya kazi kwa furaha sana. Wanafanya Kitu ambacho hata kama hawatapata fedha lakini wana furaha ya kutimiza ndoto zao za kwenye maisha. Hawa watu fedha kwao si kitu ingawa wanazihitaji ila inner satisfactions.

Rafiki yangu mmoja aliwahi acha kufanya kazi Kampuni ya Kimataifa yenye mshahara mkubwa kupita maelezo kwa miaka hiyo zaidi ya dola 5000 kwa mwezi akaamua kuwa mjasiriamali. Nilipomuuliza kwanini ameacha mshahara mkubwa vile na kuchagua maisha yasiyo na uhakika wa mshahara akaniambia nimegundua kuwa na fedha nyingi bila kuwa na amani ya moyoni ni ubatili mtupu, ni bora nisipate hata shilingi lakini niwe na Inner Satisfaction yaani furaha ya ndani kuwa nimefanya jambo moja kuelekea kwenye ndoto zangu.
Wengi wetu tunandoto za kufanya mambo makubwa sana lakini bado tumeng’anga’ania mambo ambayo hayatatupeleka kufikisha ndoto zetu kwa namna yoyote ile tunaamka asubuhi kwenda kwa mwajiri huku mioyo imeinama tuna furaha ya dakika chache tunapopata mshahara, na hata wengine wakipata mshahara hawana hiyo furaha sababu wana madeni yasiyokuwa na idadi, mioyo ina makunyanzi ya huzuni na furaha kwetu ile ya ndani imekuwa ni hadithi simulizi.
Kuna baadhi ya watu wako kwenye ndoa mbali na ajira lakini lakini si kwamba wana furaha kwa sababu wako huko wengi wanatamani kutoka hawana furaha ya ndani katika maisha yao, lakini ndo wataenda wapi sasa, unaweza waona watu wanakuja kwenye sherehe Fulani wameongozana ukawatamania walivyokuwa wanaonekana kumbe Utanashati husitiri shida ya masikini. Wakirudi nyumbani ni magomvi kuna watu hawashiriki tendo wa waume zao ama wake zao sababu ya magomvi yanayoendelea kwenye ndoa zao, wameamua kubaki sababu tu pengine wana mtoto ama watoto unasikia watu wanasema “kukosa hawa watoto ningeshaondoka zangu”. Mambo sivyo yanavyoonekana barabarani.

Kinachonifurahisha kuna watu hata hawapo kwenye ndoa wapo tu kwenye mahusiano lakini wameshaanza kufanya mazoezi ya kuvumilia, ukiwaambia si umpige chini uendelee na maisha yako atakuambia “ntaenda wapi tena” watu wamechagua kuzoea shida hizo wakiamini kama wakioana watazimudu, ndio maana katika kizazi chetu watu wanaotegeshewa mimba wameongezeka kila mtu anachagua kung’ang’ana hata kama ndani kabisa anajua hapa nimepotea. Kwa taarifa yako Ndoa inaweza kukupa Baraka ndoa inaweza kukuwehusha kama unabisha kamuulize shost wako mmoja aliyeng’ang’ania kuingia yaliyomkuta ndani ya ndoa.

Amani ya ndani na furaha ya ndani ni muhimu sana katika maisha ni vema ukafanya kazi yenye mshahara mdogo lakini una amani tele, ni vema ukaolewa ama kuoa mtu ambaye hana muonekano lakini una amani tele, ni heri leo ukachagua fungu jema kwenye maisha yako. Mimi nimekwisha chagua katika maisha kuwa na furaha, nimeamua kuacha alama katika kizazi chetu, kuna watu wanaona pengine kuna watu wanajitaabisha aina Fulani ya maisha lakini huwezi jua kwa kufanya hayo yeye amechagua kuwa na furaha. Usichague furaha ya muda chagua furaha ya milele.

Kung’ang’ania kubaki hapo hapo ingawa hauridhiki wala haupati amani haitakuletea amani sababu umeamua kung’anga’nia maana hata uvumilivu una kikomo chake.
Papaa
0713 494110.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda