Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, July 25, 2012

Ohayoda Tunasemaje Kuhusu USHUJAA?.....


USHUJAA………………..

Kwangu mimi Siku ya Mashujaa  inatoa maana hii ya Ushujaa.
Leo tarehe 25/7/2012 sawa na miaka mingi iliyopita hapa kwetu  Tanzania tangu uhuru, taifa limekuwa na dhamira njema ya kukumbuka kazi njema ambayo mashujaa wetu ambao wametutangulia mbele ya haki na wale walio hai bado, katika kuhakikisha kuwa hadhi ya Tanzania inakuwepo hata kama ni kwa kuyatoa sadaka maisha yao.

Nikiwataja ni wengi sana na wengine sintaweza kuwataja kwani hawajatajwa popote katika historia japo walijitoa mhanga katika harakati za ukombozi wa taifa letu la Tanzania, Hao ninawapongeza sana na nawatakia kila la kheri na Mungu awazidishie………… 

……………………..sasa………………………………

MBIU yangu ya haki ya USHUJAA leo naipiga kuwaelekea wale wanajamii tulionao leo katika taifa letu kila mmoja kwa nafasi yake katika kuliletea taifa ukombozi wa kila siku katika maisha, harakati hizi ni zile ZINAZO FANYA MAISHA YETU YA KILA SIKU KUWA NA MAANA SAHIHI NA INAYOTAZAMIWA NA WENGI kisiasa,kiuchumi na kijamii. “HOW DO YOU MAKE A DIFFERENCE”.

Ishu ya msingi si kukusanyika uwanja wa mnazi mmoja na kusherehekea bali ni kurudi nyuma na kufanya tathmini yakinifu ya ni nani ndani ya jamii nayetumia muda wake,nguvu zake,mali zake na vyote alivyonavyo katika kulikomboa taifa la Tanzania? Je ushujaa lazima uletwe na vita?

 Embu tuanza kwa kumwangalia shujaa ambaye ni mmbunge anaye “risk” maisha yake wala si kwa maslahi ya watu wa jimbo lake ili 2015 apate kura bali kwaajili ya taifa kwa kupaaza sauti yake ndani na nje ya bunge katika kuisimamia serikali ili itende yale yanayotazamiwa na wanachi.

Tumtambue shujaa ambaye ni kiongozi wa ngazi ya chini kabisa katika serikali ya mtaa anaye pambana na kero za wananchi za kuzibua mitaro na kuzoa taka katika mitaa yao huku kesi za kila aina zikibisha hodi katika meza yake kila kukicha.
 
Tumtambue shujaa, Yule mama ntilie anayehakikisha kuwa ile asilimia kubwa ya wabongo ambao ni mafundi makenika, madereva wa daladala, makondakta, wamachinga, wapiga debe na wale mabachela kama Nelson hapa ambao tunategemea sana ule msosi mtamu wa si zaidi ya sh. 1500/= na maji unakunywa bure kwani anamsaidia mtanzania aweze kuwa na matumizi yanayolingana na kipato chake halisi…Jamani huyu ni shujaa ambaye haihiitaji vita kumtambua.

Mtazame yule keshia pale benki, anayefanya kazi kwa minajili ya kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma kikamilifu. Bila ya kujali muda wa chai na chakula cha mchana, bado yupo tayari kujipinda mgongo kwaajili ya ile foleni kubwa inaoyomsubiri na anaifanya kazi hii bila majivuno kwani anajua yupo pale kwaajili hiyo japo mahela yote yanayopita mikononi mwake si yake wala hayatamani.
On top kabisa, mkumbuke Yule shujaa ambaye ni NESI pale katika hospitali Fulani na huyu pasipokujali maisha yake anajitoa kwa hali na mali katika kuokoa maisha ya watanzania wa kada zote kwani kazi wanazofanya si rahisi sana kwani wanaweka ubinafsi pembeni na kutumia utu wake kwaajili ya watu wengine.

Yupo mwalimu hasa Yule wa shule ya msingi ambaye anatumia muda wake japo kwa kipato cha chini lakini anajitahidi kufanya uumbaji upya katika eneo la elimu, kwa kweli kama walimu wakisema leo wanaacha kazi na wakajishughulisha na mambo mengine sidhani kama Tanzania tutakayokuwa nayo itakuwa ya watu wanaojitambua. Elimu inaitwa ufunguo wa maisha embu fikiria maisha bila huo ufunguo.Walimu wote wanaofanya kazi zao ipasavyo kwa kweli hao wote ni mashujaa, ualimu ni mgumu ndugu yangu..jaribu uone…
 
Sijakusahau wewe dereva na kondakta wa daladala ambaye bila ya kujali ile nauli ambayo abiria anakupa lakini ile huduma unayotoa kuanzia asubuhi hadi jioni bila kuchoka . Si kazi rahisi, lakini wewe umeifanya hii kazi takribani miaka mitano iliyopita si kwa sababu umekosa kazi nyingine bali kutokana na kuipenda kazi hii ya kutoa huduma kwa watanzania ambao bado hawajapata fursa ya kuwa na usafiri binafsi.

Tumtazame mwanafunzi wa kiwango chochote cha elimu anayejua kuwa elimu anayoitafuta ni kwaajili ya ukombozi wake na watanzania wanaomzunguka, kwa hiyo suala la msuli tembo kwa kusoma pasipo kujihurumia linapewa kipaumbele kwani kwa hili anajaua atafanikiwa na bila shaka ile kanuni ya “utavuna unachokipanda” itajidhihirisha…..huyu naye ni shujaa wa stahili yake.

Mwangalie Yule mwandishi wa habari ambaye  yeye anajitoa mhanga kwa kufanya kazi katika mazingira magumu sana ya kutoa taarifa kwa umma juu ya yale ambayo yanatokea hapa kwetu Tanzania hata kama yanahatarisha maisha yake kwani hakuna wa kusema ila yeye. Kwangu mimi huyu ndiye shujaa na mzalendo kwani bila yeye ukombozi ungeendelea kuwa historia.

Usimsahau kiongozi wa dini ambaye yeye anafanya kila linalowezekana katika kuhakikisha kuwa waumini wake wanaishi kwa kufuata misingi ya kidemokrasia, kimaendeleo, kiutu na kwa kila namna ili kuiweka Tanzania katika hali ya usalama zaidi. Na huyu ni shujaa wetu leo, embu tumtambue.

Wapo wengi sana,kama vile madaktari, polisi, mahakama, wanaharakati,wanauchumi,nakadhalika…. nikiendelea hapa sintamaliza ila kwa kumalizia tu niseme kuwa TUNAHITAHI KUTAMBUA MCHANGO waasisi wa taifa letu lakini zaidi sana kwa wale wanaolifanya taifa hili liendelee kuwa na muonekano tunaouona leo kwani isingefaa kitu kama wangeleta ukombozi na sisi tusiuenzi huo ukombozi, kwa hili lazima tuutambue mchango wa mashujaa wetu wa leo.

…………………………Ewe shujaa mwenzangu, Kaza Buti Safari bado ndefu, endelea kuisimamia dhamira ianayokusukuma kufanya unalolifanya kwaajili ya Tanzania, kwa kuwa dunia huwa haina shukrani ukiwa hai basi uamini kuwa .

LIYEKUWEKA DUNIANI ANAJUA ATAKULIPA KWA NAMNA GANI………ENDELEA KUCHAKARIKA…..WANAKUHITAJI HATA KAMA WASIPOKWAMA

chezea shujaa wewe?? Muulize Nelly wa Ohayoda.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda