Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, July 25, 2012

Melankoli, Watu wenye Tabia hizi wengi ni ma Geneous.Na Nelson wa Ohayoda

Bila shaka  Mungu wa kil kitu anakulinda na unaendelea na shughuli zako, kama ni mwanafunzi basi unapata time ya kupitia blog lakini baada ya hapa unarudi kupiga msuli tembo uli upate matokeo tembo na si msuli tembo matokeo sisimizi au msuli sisimizi matokeo sisimizi, kama wewe umeajiriwa ujue basi kuna wakati wa kupitia blog ya ohayoda ila kazi zinaendelea, na wasomaji wetu woote popote pale mlipo….asalaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam, aleikhum……..

Ninaomba nitumie nafasi hii kutoa ufafanuzi katika somo letu la IJUE HAIBA YAKO linaloendelea katika blog yetu . Nimekuwa nikipata comments na simu nyingi sana na wengi wanasema hawaelewi haya ni makitu gani, Jamani nawasihi sana kwakuwa wengi mnalifurahia sana somo hili, basi jitahidi kuingia kwenye search engine yetu na uandike, “IJUE HAIBA YAKO SEHEMU YA KWANZA”, hapo utapata mwongozo utakao kupa muunganisho na hapa tulipo leo.

Na kwa kuwasaidia zaidi, Haiba ni tabia za asili ambazo kila mwanadamu aliumbiwa na Mungu katika mapungufu yake na katika ukamilifu wake, OHAYODA inakusaidia kuzifahamu tabia kwa kuzichambua na kuziweka kaitika KATIKA MAKUNDI makuu MANNE yenye majina ya KISAIKOLOJIA NA tunayafanya yawe ya Kiswahili ili angalau kila Mtu afaidike na kujitambua. Ifahamike kuwa kwa kila kundi kuna tabaia mahususi zinazolipa kundi husika heshima ya kuwa lilivyo, makundi yenyewe ni SANGWINI, MELANKOLI, FLEGMATIKI NA KOLERIKI na ukifanikiwa kuyaelewa na kulifahamu kundi lako vyema itakusaidia uweze kuishi na kila mtu bila kuwa na migogoro ya kila aina. Kazi ya OHAYODA ni kukusaidia kidogokidogo katika kujitambua na kuwatambua wengine, hii ni nzuri sana kwani inakuweka salama.

NB: KAMA NDO KWANZA UNAJIUNGA NASI, TAFADHALI FUATILIA SOMO HILI TANGU MWANZO KWENYE SURA YA KWANZA NA SEHEMU ZAKE ZOTE NDIPO SA UENDELEE KWENYE SURA HII YA PILI NA SEHEMU ZAKE ZOTE,HII ITAKUSAIDIA UWEZE KUELEWA SOMO HILI VIZURI.

Baada ya kuangalia utangulizi huo wa somo hili La IJUE HAIBA YAKO (Know your Personality) Katika sehemu hii tumalizie sehemu yetu ya kwanza kwa kuziangalia sifa njema za Mwanadamu mwenye tabia katika kundi la MELANKOLI.

*Wewe kama Melankoli una tabia ya kung’ana’ania jambo hadi likamilike, si warahisi sana kuacha kufanya jambo Fulani bila ya kuona kuwa umemaliza. Kwa mfano kufanya swali gumu la masomo kama hesabu.
*Ana uwezo wa kuwa kiongozi mzuri japo hali yao ya kuwa na maswali huwa ni ngumu kidogo ila ni viongozi wazuri
*Melankoli kama akiwa ni mzazi au mlezi au kiongozi ni wepesi sana wa kuwawekea watu matarajio ya hali ya juu sana na huwasababisha wakati mwingine kushindwa kufikikia viwango ambavyo melankoli anawekea.
*Ni wa simamizi wazuri sana katika kazi Fulani.
*Huona matatizo na kuyafanyia kazi kikamilifu.
*Hutiwa moyo sana pale ambapo viwango vya kazi zao vinazingatiwa.
*Melankoli ni mtu wa maelekezo kwani maelekezo ni njia mojawapo ya kufikia malengo.
*Ana tabia ya NDANI yenye usiri mkubwa. (Introvert).
*Ni mpembuzi sana wa mambo, kwake kila kitu lazima kichambuliwe kwa undani wake.
*Kwa kuwa ni watu wa ubora, wanategemewa sana katika jamii, na kutokana na tabia yake ya uchambuzi ni rahisi kwa yeye kuwa na nafasi ya kuviona vikwazo na matatizo kabla ya kufanya lolote.
*Melankoli ni mwanadamu asiyependa sana mabadiliko na hii humfaya asimamie mambo yake ipasavyo.
*Tabia yake ya kujiuliza maswali sana huwa anachelewa sana kufanya maamuzi.
*Ni wasikilizaji wazuri sana.
*Ni wanadamu wenye kujizatiti na ni watu kuepusha gharama.
*Na mwisho ni kuwa, walichonacho katika maisha ni sawa na kusema, “Tafadhali  Nielewe”.


Embu sasa tuulizane, Je, Umeelewa? Kama ndiyo….usiache kutushirikisha mawazo yako, kaa tayari sasa kuyafahamu mapungufu ya MELANKOLI kwani ni mengi na kwa bahati mbaya hajatokewa kupendwa sana kwani huwa wanaonekana wenye dharau sana na kwamba wengine hawawezi isipokuwa kwa kupitia kwao………………….tafakari……………Jitambue….Kama kawa, Mungu akutunze.
tuonane ijumaa....................................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda