Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, July 1, 2012

Ninachokiwaza juu ya Hotuba ya raisi wetu.......

Na Nelson Faustin,
a.k.a Meku Mtanzania
Mbali na swala la usafirishaji wa binadamu, Mheshimiwa Raisi alitolea majibu swala la madaktari…….

“Ndugu zangu madaktari, wahurumieni watanzania wenzentu wanaoteseka……………………..” Hii ni kauli ya masikitiko ya raisi Jakaya Kikwete alipokuwa akilihutubia taifa hapo jana 30 -6-2012.

Na huu ni mtazamo wangu kutokana na hotuba ya Mh. Raisi kuhusu mgomo wa madaktari……..

Je, sisi watanzania masikini tutakimbilia wapi? Ninaumia sana nikisikia msimamo wa serikali kupitia raisi wa nchi, swali langu la msingi kama mtanzania wa hali ya chini kabisa ninayeandika kwa niaba ya asilimia kubwa ya watanzania waliopo vijijini ambao mgomo huu unawaathiri kwa asilimia kubwa sana ni Je, hii hali hata lini?  

Tunafanyaje sasa sisi watanzania masikini kwani sasa hali inakuwa mbaya kila uchwao, sifurahii hata kidogo vita hii ya watanzania wachace (serikali) na watanzania wengi (madaktari) dhidi ya watanzania masikini walio wengi sana ambao wanaitazama vita hii iishe ili waokoe maisha yao.

Ingekuwa hiari yangu, ningeomba tuwe na muda wa kusikitika pamoja kwani kama ulikuwa hufahamu, serikali imenena kuwa, katika swala la posho, nyumba, posho ya kuitwa kazini na mshahara wa kuanzia kazi daktari ni mambo makuu ambayo yanasababisha vita hii iendelee kuwa ngumu sana na hata hatma ya sekta hii nyeti ya afya nchini iendelee kuonekana kuwa maelfu kilometa zaidi katika kufikia suluhisho kwani  tumaini halipo tena.

Zaidi ya hapo, mbali na kanuni za kazi kuendelea kusimamiwa na mahakama kuu kitengo cha kazi, silaha katika vita hii zinazidi kuboreshwa na watanzania wanazidi kuangamia sana, kana kwamba hayo hayatoshi, mheshimiwa raisi amsesisitiza kuwa mgomo si halali, na wanaogoma hasa wale madaktari wamazoezi wanahatarisha maisha yao ya ajira ya sasa na ya baadaye kwa kushiriki mgomo ambao ni haramu. Hii imezidi kutuvuruga watanzania masikini.
Kwa  hayo yote, serikali imesisitiza kuwa haina uwezo wa kutekeleza madai yao kama wanavyotaka na anayetaka mshahara mkubwa na posho basi aende anakotaka na serikali kama mwajiri itawatakia kila jema kwani kwa sasa matumizi ya serikali kwa mishahara ni asilimia 48 ambayo inasababisha shughuli nyingine za kimaendeleo kukwama.

Kwa hiyo bado hakuna suluhusho na sidhani kama mgomo  utakoma au utaendelea?........Madaktari ni watu na serikali pia inaundwa na wa wanadamu, Tafadhali embu sote turejee dhamiri zetu kwani kwa kipindi kifupi nguvu kazi ya taifa inapotea na tunaliweka taifa letu rehani kwani matatizo kama ya walimu bado yananukia nukia………kanuni zipo ila zifwatwe kwa kuzingatia pia dhamiri safi zenye utu ndani yake.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mungu tusaidie katika swala hili la vita baina ya madaktari na serikali………………………Na Mtanzania Meku.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda