Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 5, 2012

Nimeipenda hii,,,Waisilamu kulinda makanisa KenyaHabari NJEMA ya siku toka Afrika Mashariki.
                          IT BRINGS GOD'S GRACE


Kumbe inawezekana dini hizi mbili kubwa kuwa chanzo cha amani na mafanikio au chanzo cha vurugu na vita
Kuna chombo kimoja cha habari hapa  nchini, ntafurahi sana kama watapata nafasi ya kuisoma hii.


VIONGOZI wa Kiislamu nchini Kenya wamekubaliana kuunda makundi ya kutoa ulinzi kulinda makanisa kutokana na mashambulizi kama yaliyotokea Kaskazini mwa Kenya siku ya Jumapili.

Watu 15 waliuawa katika mashambulizi mawili dhidi ya makanisa mawili mjini Garissa karibu na mpaka wa Somalia. Eneo la mpakani mwa Kenya na Somalia limekumbwa na hali ya wasiwasi tangu Kenya ilipopeleka majeshi yake kupambana wanamgambo wa Al-Shabab.

Mkuu wa baraza la waisilamu nchini Kenya, Adan Wachu, aliambia BBC kuwa kitendo cha Jumapili kilikuwa cha ugaidi. Waislamu wanahisi kuwa kwa sababu wakristo ni wachache katika sehemu hiyo hakuna budi kuwalinda.

“Kuna watu huko nje wanaotaka kufanya kila wawezalo kufanya Kenya kama Nigeria.” Alisema bwana Wachu, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la viongozi wa kidini nchini Kenya.”
“Sisi hatutaruhusu kutokea ghasia za kidini nchini humu, yeyote aliye na nia ya kuchochea hali hiyo afahamu kuwa hatafaulu.” aliongeza Wachu.

Alisema kuwa sasa ni juu ya viongozi waisilamu mjini Garissa kupanga namna ambavyo makanisa thelathini yaliyo Garissa yatalindwa. Watu wengi wanaoishi ndani na kando ya mji wa Garissa ni wasomali na ambao ni waisilamu.

Mwezi Oktoba mwaka jana wanajeshi waliingia nchini kupambana dhidi ya al-Shabab wanaotuhumiwa kufanya vitendo kadhaa vya utekaji nyara na kutatanisha usalama kwenye eneo la mpakani.
Lakini tangu hapo Al Shabaab limelaumiwa kwa kufanya msururu wa mashambulizi ya maguruneti katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo. Viongozi wa kundi hilo, hawajajibu shutuma zozote za kufanya mashambulizi ya Garissa.

CHANZO: BBC..http://www.thehabari.com/?p=19805


TOKA DAWATI LA OHAYODA
UTOFAUTI WA DINI USITUFANYE TUDHARAULIANE, TUJIDHARAU, TUONE TUNAFURSA ZAIDI YA WENGINE, TUJIONE NDO WA MAANA KULIKO WENGINE, BALI KILA MTU AHESHIMU UTU WA MTU MWINGINE BILA YA KUJALI DINI YAKE.


RAI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE....
TAFADHALI SANA, MSIRUHUSU WATANZANIA AU WANAAFRIKA MASHARIKI TUTENGANE KWA SABABU ZA UBINAFSI KATIKA DINI ZETU...SISI SOTE NI MALI YA MUNGU, MBIVU NA MBICHI ANAZIJUA YEYE...


                                                                                                                                                                                        Na Nelson Faustin.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda