Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, July 26, 2012

Nimeiamini TANESCO ila................


TANESCO.....Kwa kauli yenu tumewaamini ILA...........

Ninaishukuru sana TANESCO, shirika ambalo kwa nafasi yake ni sawa na MOYO katika mwili na maisha ya mwanadamu.

Tangu juzi tarehe 25 July 2012 mmekuwa mkitoa matangazo kupitia vyombo vya habari mbalimbali vikiwemo STAR TV na TBC 1, kwa macho yangu nilisoma na kwa masikio yangu nikasikia kuwa TANESCO  inakanusha vikali taarifa zilizotelewa na vyombo vya habari kuwa, kutakuwa na mgao mkali wa umeme siku za usoni.

Nilifurahi sana kupata ufafanuzi kutoka TANESCO Kuwa, HAKUTAKUWA NA MGAO WA UMEME HADI MWAKA HUU UISHE; NA KWA HIYO, HIVYO VYOMBO VYA HABARI VIMEIPOTOSHA JAMII NA WALA TAARIFA HIYO HAIKUFUATA KANUNI NA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI. 

Ila nikajiuliza swali la kawaida, Je, hawa majamaa wamepata wapi ujasiri huu mkubwa kiasi hiki, wakati juzi juzi hapa nilimwona Mh. Waziri Maghembe akiwa kule Mtera na ikaonekana kabisa kiasi cha maji kinazidi kupungua? Na zaidi ya hapo,hizo tetesi za madeni na migogoro ya hapa na pale, lakini bado wameweza kutoa kauli nzito kama hii?......Ohayoda……….Ohayodaaaaaa….mmmmh????????........

Ila nikapata faraja kuwa, “kwa kuwa wametangaza, basi wana uhakika na kile wanachokisema wala hawana wasi wasi kwani wanajua TANESCO kama MOYO WA MWANADAMU SI KITU CHA KUCHEZEA”…

Mimi na wewe tuwe na uhakika kuwa; hakutakuwa na mgao wa umeme KABISA, japo wamesema hadi mwaka huu uishe, labda  mwakani waweza ukawepo. Tuendelee kuwaamini wasimamizi wetu hawa wa nishati hii muhimu.

RAI YA OHAYODA KWA TANESCO: 

Imani yangu pamoja na mamilioni ya watanzania wanaotegemea nishati hii kwaajili ya shughuli zao za kila siku imeimarika na wala hatuna wasiwasi wa kununua majenereta na solar kama tahadhari kwani mmetuhakikishia live bila chenga kuwa MGAO WA UMEME TANZANIA NI NDOTO.

 Hivyo tunawaomba sana, msimamie kauli hii nzito mliyoitoa; kwani lolote ligusalo maslahi ya taifa lazima liwe na mwitikio wa kitaifa. Mjue kauli hiyo ipo vichwani mwetu na TUTAWAKUBUSHA PALE ITAKAPOKUWA NDIVYO SIVYO. 

OHAYODA inasema kuwa, wala vyombo hivyo vya habari havikuwa na lengo la kuichonganisha TANESCO na jamii; kwani nadhani kwa kuitoa taarifa waliyoitoa sasa wamepata kile walichokitamani kutoka kwenu na hii ni kuwa, “HAKUTAKUWA NA MGAO WA UMEME HADI MWISHO MWAKA”.

Na Nelly wa Ohayoda Mtanzania by Calling.NI HILO TU TOKA OHAYODANI……..

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda