Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, July 15, 2012

MCH. GWAJIMA NA SAKATA LA POLISI NA DR.ULIMBOKA.

Na Nelson wa OHAYODAAAA...,,,,

.....Inatokana na taarifa kuwa,"ALIYEMTEKA DR. ULIMBOKA AENDA KWA GWAJIMA KUOMBA TOBA"
Bila ya kuhadithiwa, mimi mwenyewe nilipata fursa ya  kumsikia kwa masikio yangu mawili Mchungaji wa kanisa la ufufuo na Uzima Mch. Josephat Gwajima, jinsi alivyofafanua kwa undani juu ya sakata la mtuhumiwa aliyetangazwa na kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova kuwa alihusika katika kumkamata na kumtesa kinyama Dr. Ulimboka.

Katika hali ya kushangaza sana, wiki hii kumekuwa na tetesi kuwa, mmoja wa aliyehusika katika kumteka  Dr. Ulimboka Stephen amekamatwa na inasemekana alienda kutubu katka kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kawe jijini Dar es salaam maeneo ya Tanganyika Peckers.

Kwa mujibu wa Askofu Gwajima ni kuwa, tangu tarehe 26,27 June 2012,  kuna mtu alijitokeza katika viwanja vya kanisa la Ufufuo na Uzima akitaka kuonana na mchungaji kiongozi lakini walinzi wa kanisa akiwemo mch. Marwa waliamua kumkamata na kumuhoji zaidi baada ya kuona kuwa maelezo yake yamegusa swala la Dr. Ulimboka ambalo linagusa hisia taifa kwa ujumla. Kwa kuzingatia hoja hii kuntu, walinzi waliamua kumpeleka muhusika katika vyombo vya dola  katika kituo cha polisi Kawe na baadaye kituo kikuu cha polisi Osterbay kwa maelezo zaidi.

Katika kumhoji mtuhumiwa huyu mbele ya walinzi wa kanisa la Ufufuo na Uzima, mtuhumiwa alisema kuwa, "Kwa kweli ninaomba sana mnisamehe kwani mimi nina matatizo makubwa kwani kuna liroho ambalo huwa linaniingia na ninaanza kuropoka maneno yasiyo na maana, kwa hili ndugu zangu ninaomba mnisamehe".
Kutokana na hali hii, Polisi pamoja na walinzi wa ufufuo na uzima wakakubaliana yale yoooote yaliyoyokaea yaishie pale pale, lakini kwa kushangaza Polisi kupitia kamanda Kova akatangaza taarifa ile ambayo walikubaliana wasiiseme kwa yeyote kwani halikwa na ukweli wowote bali kuwachanganya watanzania.

TAARIFA KWA UMMA: 
Mchungaji Gwajima alisema kuwa, Kanisa lake halina uhusiano wowote na mtu huyo wala kanisa halina kazi ya kuitetea serikali wala madaktari bali linasimamia ukweli, na hivyo halihusiki na mtu huyo kabisa labda ana mambo yake na Hakuwahi kwenda kutubu katika kanisa hilo.

USHAURI WA ASKOFU GWAJIMA KWA SERIKALI na UMMA wa Tanzania:
 • Kamwe polisi wasitoe taarifa isiyokuwa na ukweli na katika hali yoyote kabla ya kutoa taarifa muhusika afanyiwe uchunguzi kwanza kabla ya kukurupuka.
 • Hemedi Msangi anayetajwa AKAMATWE na kuhojiwa kwa undani kwani itawasaidia kupata taarifa sahihi badala ya kutoa taarifa za kubuni.
 • Suala la kuwafutia madaktari leseni za udaktari ili hali wamewagharamia kwa mabilioni ya shilingi na watu wanaendelea kuangamia na Baya sana na halifai. 
 • Washauri wa Mh. Raisi wajitahidi kumshauri vyema kwani inavyoonekana ana washauri wabaya ili hali yeye ana dhamiri safi na nchi yake.
 • Na kwa kuwa kwa wale wanao tuhumiwa serikali ni mmoja wao kadiri ya hotuba ya Mh. Raisi June 30th basi iteuliwe tume huru ya kulichunguza jambo hili na si serikali kwani na yeye ni muhusika.
 • Serikali, liangalieni swala hili kwa jicho la tofauti laa sivyo Mtapigwa na Bwana.
 • Mwisho, Madkari WAACHE MGOMO NA WARUDI KAZINI KWA JINA LA YESU la sivyo mtapigwa na Bwana.
 Hiyo ndiyo hali halisi,
                                               "Mwenye, Macho haambiwi TAZAMA"

4 comments:

 1. hivi Mh.Rais hua anateuliwa washauri? Si anawateua mwenyewe? Iwapo anateua washauri wabaya kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini ni kosa la nani? Alieteua au alieteuliwa? Sisi tunawezaje kusema kwamaba Mh.Rais ana washauri wabaya kama yeye aliewateua na anaeshauriwa haoni ubaya wao?

  ReplyDelete
  Replies
  1. ASANTE SANA....
   NADHANI NI SWALA LA KUONA KWAMBA ALIYETEULIWA ANAFANYA YALE YANAYOTARAJIWA NA MTEUZIM, SASA KILA BOSI ANA BOSI WAKE, SISI TUNATAZAMIA NINI FROM THE PRESIDENT NA YEYE ANATAZAMIA NINI TOKA KWA WATENDAJI WAKE AMBAO HAO WOTE SIS TUNAWATAZAMA?

   Delete
 2. Serikali inajaribu kujitakasa ili ionekane halina dhambi!Hongera Ngwajima kwa ukweli na kutokulalia upande.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda