Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, July 21, 2012

Matukio ya Harusi ya kidatooga katika picha

Wadatooga kama ilivyo kwa jamii nyingine huwa na sherehe za harusi pale ambapo vijana wawili (wa kiume na kike) wanapoamua kufunga ndoa na kuishi pamoja. Lakini tofauti na jamii zingine, sherehe za harusi huhudhuriwa na wanawake tu hata bwana harusi hatakiwi kuonekana katika eneo la shughuli na hata bibi harusi anakuwa amefichwa porini hadi baada ya ndugu zake (waliohudhuria harusi watakapoondoka).
Ohayoda ilipata fursa ya kujua yanayojiri katika shughuli hiyo ambapo mama wa binti hupewa zawadi nyingi hasa nyama na damu iliyokaangwa na kupakwa mafuta ya ng`ombe mwili mzima kama heshima ya kuwaletea mke (mzaa chema).
Yapo mengi sana ambayo hujiri katika shughuli nzima na mengi ohayoda iliyaeleza katika moja ya makala huko nyuma kuhusu harusi za wadatooga. Hapa tunakuletea sehemu tu ya matukio yaliyojiri katika moja ya harusi chache za kimila huku kwetu, haikuwa kazi rahisi lakini shukrani za dhati kwa Janeth John na Herman Malleyeck na familia nzima ya Ungo kwa kutupa idhini kuchukua picha.
Kina mama wa Kidatooga katika shamrashamra za harusi

Kina dada wakiimba na mwali


Janeth akiwa na huyu mama sijui anaitwa qamata nani

Mjini mwali hupewa vyombo mbalimbali, hata huku kwetu mwali hupewa vipeyu (pichani) tayari kwa ajili ya familia mpya

Huu ni ugali uliopikwa kwa mafuta (siagi) ya ng`ombe, kina mama wa pande zote mbili hula pamoja kama ishara ya kuunganisha koo na kuunda udugu

Mama wa mwali pamoja na ndugu wa kike wa mwali huwekewa mafuta (siagi) kichwani kama heshima ya kumtunza binti hadi kuolewa kwa heshima


Kina mama wakiwa wamebeba vyakula kwenye vipeyu, kila mtu hujitegemea kwa chakula katika kipindi cha harusi

5 comments:

 1. Wow.. Its a wonderful experience kuwafahamu hawa watu, i never thought kuwa such kind of people with such unique customs exists. How about Gospel, are they getting Born Again there!? I mean is the Gospel of Salvation preached to them..!Do they have/go to churches? and which church has reached them!?
  Thank you so much
  Bro. Tony Asukile.
  Mbezi Beach
  Dar es salaam

  ReplyDelete
 2. HAHAHAAA.... NIMEPENDA VIPEYUUU
  SANDE SANA MUWAHA

  ReplyDelete
 3. it's good. but bibi Harusi wala bwana harusi sijawaona

  ReplyDelete
  Replies
  1. Bibi arusi angekuwa muhimu kuonyeshwa.

   Delete
 4. Oh! Ni ajabu kweli kweli - duniani kuna mambo

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda