Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, July 2, 2012

Martha Kirika akamatwa na MihadaratiNa Mary Margwe
Simanjiro-Manyara
Mkazi mmoja wa mtaa wa Songambele Mji mdogo wa Mirerani, Wilayani Simanjiro Bi.Martha Kirika (46) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara akidaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya, bangi, mirungi na pombe haramu ya gongo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi Mkoani Manyara, Akili Mpwapwa alisema tukio hilo lilitokea juzi huko katika mtaa wa Songambele  mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Kamanda Mpwapwa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na misokoto 92 ya bangi, na bunda 25 ya mirungi  pamoja na lita moja ya pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo.

Alisema mwanamke huyo alikamatwa, kwenye msako maalum wa kupambana na uhalifu na kuimarisha doria, iliyoongozwa na Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Mrakibu Msaidizi Ally Mohamed Mkalipa, Naftal Mnzava na Sajini Joseph Mirambo.

Aidha alisema kuwa jeshi la Polisi Mkoani hapo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, na pindi upelelezi huo utakapokamilika wanatarajia kumfikisha Mahakamani mtuhumiwa huyo  kwa shauri hilo.

“Zoezi hili ni endelevu na linaendelea sehemu zote za mkoa wetu,ili kuhakikisha kuwa vitendo vya uhalifu ninapungua kama si kwisha kabisa,na ninawapongeza vijana wangu kwa kulifanikisha zoezi hili la kupambana na uhalifu katika mkoa huu,” alisema Kamanda Mpwapwa.   

Kamanda Mpwapwa alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja kwani jeshi lake limejipanga vizuri kupambana na uhalifu wa aina yoyote ile na kuwachukulia hatua kali wale watakaobainika kuhusika na tukio lolote la uhalifu.

Alisema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mahusiano mazuri baina ya jeshi la polisi na raia wema kwani taarifa zao kwa namna moja au nyingine zimefanikisha zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda