Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, July 31, 2012

Karibu katika Makala Mpya Ya "SIKITIKO LANGU Jumanne Hii", Ndani ya OHAYODA.

Na Nelson Faustin.
Nirejee kidogo kwa kunukuu maneno ya Papaa Sam Sasali kwenye makala yake ya Papaa On Tuesday, amesema, "Uliumbwa Kwa Sababu haukuumbwa kama boya, uko duniani kwa makusudi maalum wewe ni Project Manager wa Mungu Duniani, Kuna Kitu Mungu anataka kufanya duniani kupitia wewe", nikakumbuka kuwa, makala hii ya "SIKITIKO LANGU JUMANNE HII", inaweza kuwa moja kati ya projects ambazo Mungu anataka mimi nifanye kwaajili ya jamii kutokana na yale ambayo Mungu atanipa Neema ya kuyadondosha kwenye blog yetu hii ya Ohayoda.

Sikitiko langu ni makala itakayokuwa inatoa taswira halisi juu ya mtu, kitu, au hali fulani ambayo kwa jinsi ilivyo kinaweza kuiathiri au kuigusa jamii kwa namna moja au nyingine. Lengo si tu kusikitisha jamii bali ni kujaribu kuona kama jamii inaweza kujifunza na kufanya kila linalowezekana kuliepuka jambo hilo, mtu huyo au hali hiyo.

Leo, SIKITIKO LANGU Jumanne hii inalenga kwenye anguko la kitaaluma ambalo linaendelea kuitafuna Tanzania yangu ya leo "kwa siri" kutokana na kutokuwepo kwa uwiano kati ya changamoto nyingi za kimaendeleo ambazo zinaikumba dunia na hususani Tanzania na uwezo wa kitaaluma wa kuweza kukabiliana na changamoto hizo.

Si jambo la kuficha kuwa, shule zetu za msingi na sekondari ambazo zinasimamiwa na serikali zipo katika hali ngumu sana ya kitaaluma na hata kimiundombinu, sina wa kumlaumu kwa hili kwani ni janga letu sote. Lakini licha ya kuwa kila mwaka idadi ya wahitimu katika kozi hii ya ualimu kutoka vyuo mbali mbali kama vile UDSM, SAUT, UDOM, TUMAINI na vinginevyo vingi huwa ni kubwa sana  kama asilimia 50 hivi ukilinganisha na kozi nyingine zote, lakini bado matarajio ya elimu yetu kukua ni madogo sana.

source:www.tanzaniagateway.org
Leo hii tunataarifa za mgomo wa walimu,ila kwa mtazamo wangu ni kuwa jamii inapaswa kufungua macho na kutathmini matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne, na kidato cha sita kwa miongo mitatu iliyopita katika shule za serikali ambazo asilimia kubwa ya watanzania ndiko wanakosoma kutokana na hali halisi ya uchumi wetu. Tathmini hii inaweza kutupa sura ya tofauti kuwa, si kwamba wanafunzi wote wanaosoma katika shule hizi hawana akili za kufaulu yani, "they are not tabularasa", na pia haimaanishi kuwa walimu wanaofundisha katika shule hizi hawakufuzu vizuri katika vyuo walivyosoma, na wala haiwezi kumaanisha kuwa utaratibu wa wizara wa kufunga na kufungua shule pamoja na mipangilio ya mitihani haifuatwi...Sasa wewe na mimi tujiulize, hii inamaanisha nini? 

Embu tujiulize; Je, shule binafsi zinanawanafunzi wa aina gani? Je, walimu wanaofundisha katika shule za binafsi wanatumia mbinu gani? Je, wote wanaofeli darasa la saba, kidato cha nne, na kidato cha sita wanakwenda wapi? Je, wengi ni kutoka shule za serikali au shule za binafsi? Je, wanafunzi wengi wanaopata nafasi za kujiunga na vyuo vikuu ni kutoka shule za binafsi au shule za serikali? Je, wanaopata nafasi za kujiunga na shule angalau zinazoonekana bora za serikali kwa masomo ya kidato cha tano wengi ni kutoka shule za serikali au za binafsi? Je, Ualimu ni wito tena kama zamani au ni taaluma ya kujipatia kipato na maisha bora kama zilivyo taaluma nyingine? Je, idadi ya wasomi inaongezeka au inapungua? Je, ukuta kati ya wasomi na wasio wasomi unazidi kujengwa au unavunjika kidogokidogo? Je, tofauti ya uelewa wa dhana ya elimu na taaluma kati ya watanzania waishio Mijini na waishio vijijini inatafsiriwaje? Nani abebe lawama kwa Je hizi zote? Je ...Je, Je, Je,,,,zipo nyingi sana mpenzi msomaji.

For God and My Country.
Swali la msingi linarejea pale pale kuwa, Je Tanzania ya kesho itaweza kukimbizana na dunia ya kesho? Nilibahatika kuwa mwalimu wa sekondari kwa miongo miwili katika shule moja ya binafsi. Mitazamo ya walimu wenzangu niliokuwa nakutana nao hasa wengi kutoka shule za serikali, ilinikatisha tamaa sana sana pale nilijaribu kufikiri kwa undani hatma ya wanafunzi waliopo chini ya uangalizi wa walimu hawa. Kwa kusema hili siwalaumu walimu hawa kwani kwa kuwa wao ni wanadamu basi kuna sababu kuntu za kuwafanya waseme maneno yanayotoka mioyoni mwao kupitia vinywa vyao kama vile, "Elimu ya taifa hili imeuzwa, Watoto wa masikini watabaki kuwa masikini wa mali na taaluma, I am looking for green pastures, Ninatoa 10% na 90% ni maelewano kati ya mwanafunzi na mwalimu, ukiitumikia serikali utakufa masikini, ualimu ni taaluma illiyolaaniwa, ninafanya kazi ya ualimu kwa kuwa sina kazi nyingine, kila mtu abebe msalaba wake kwani hata mimi niliubeba wa kwangu.......na mengine mengi naogopa hata kuyasema nisije nkachapwa viboko mie. Lakini hiyo ndiyo hali halisi.

Kana kwamaba haitoshi, Ualimu umekuwa ni dampo la waliofeli, Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikisikitishwa na kauli za wazazi au walezi ambao bila hiyana huwaambia watoto wao ambao wamefeli kidato cha nne au kidato cha sita kuwa,"umekosa hata ualimu?" Hii inamaanisha nini?????? kwa kauli hii tuna walimu wa ngapi ambao ni matokeo ya kauli kama hizi? Je, kama hakuweza kufanya vizuri atawezaje kumwandaa mtanzania  mwenye viwango vizuri vya taaluma? Mtanisamehe sana walimu ila mimi niliingia katika taaluma hii nikiwa na div. 1 form four na form vi ili kuidhirishia dunia kuwa, "ualimu si kwaajili ya vilaza". Jamii inapaswa ilauumiwe kwa hili.

Twende mbele turudi nyuma, tusijisahau jamani, hatma ya elimu ya taifa letu ipo matatani, tuweke siasa kando tuutazame ukweli ili tujue wapi pa kuanzia, elimu ya taifa hili ni Bomu ndugu yangu, ambalo linajidhirisha katika kujibu maswali yaliyoko katika aya ya sita na ya saba katika makala hii. Kama unaipenda nchi yako utafanya kila liwezekanalo katika kuisaidia jamii, kuanzia ngazi ya familiya,  ukoo, tarafa, kata, kijiji, wilaya, mkoa hadi taifa kwani bomu hili likilipuka madhara yake ni kwetu sote, tusimsubiri mtu atutoe hapa tulipo, wasukuma wanasema "JIONGEZE", tuache siasa, Jamii IJIONGEZE, Serikali IJIONGEZE tena SANA, wadau waelimu amabao ni WALIMU, WAZAZI na WANAFUNZU nao wajiongeze.

Ikumbukwe kuwa, hali ngumu ya maisha inaweza kumfanya mwanadamu akafanya mambo ambayo asingependa kuyafanya, tusiwalaumu walimu (UKIMUULIZA MWALIMU, ANAYAJUA MACHUNGU YA KUWA MWALIMU) bali ninaiomba serikali yangu kwa unyenyekevu mkubwa, kwa kuwa inawezekana basi fanyeni kwa kuwa nmsipofanya mwisho wa siku walimu kama madakatari watarudi kazini. kwa kuwa umeshikilia mpni ma wao wameshikilia makali ila ikumbukwe hata wao ni wanadamu, watafanya kazi lakini kwa shingo upande na athari zake japo mtu anaweza asife kama ilivyokuwa kwa madaktari lakini athari zake ni kubwa na ni za muda mrefu, wakati wewe uliye madarakani sasa hautakuwepo tena madarakani na hili litakuwa tatizo kwa watakao kuwa madarakani kwani litakuwa ni taifa la "MA-MBUMBUMBU" kwani shule ni zaidi ya kuingia madarasani na kumsubiri mwalimu.

Kila mtu akiona na kukaa kimya, Eti anaogopa, Ni Nani atasema?

Hali hii inasikitisha, wewe na mimi Tusikitike ila Tusiishie hapo.....Mimi nimesema wewe utafanya nini? Najua unaiona hii hali ilivyo.

Tuonane Jumanne ijayo katika makala nyingine ya "Sikitiko Langu Jumanne Hii".
UBARIKIWE.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda