Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, July 28, 2012

Kutoka Ukerewe hadi Iramba: Historia, Maisha na Tabia za Wanyiramba na Wanyisanzu.....Sehemu ya Pili

Na Amani Paul, Kidarafa
Mu hali gani wanaOhayoda popote mlipo duniani, leo nipo Kidarafa kijiji kilichopo katika wilaya ya Iramba (sasa Mkalama nadhani) kipo kilometa takriban 10 kutoka Haydom. Kidarafa kunanikumbusha mbali sana, kuna mlima maarufu sana unaitwa "Mlima wa Msalaba", mlima ambao unajiwe refu juu yake na juu ya hilo jiwe kuna msalaba umewekwa. Sijui haswa historia ya huo msalaba na nani aliuweka na kwa nini, lakini Kidarafa inabaki kuwa sehemu muhimu ya maisha yangu ya utotoni. Hapo pia ndipo nilipoweza kufahamiana na kuishi na Wanyiramba na Wanyisanzu na wengi nilisoma nao nilipokuwa Shule ya Msingi Endaharghadatk. 
Tuachane na hizo "story" za utotoni tutazipiga siku nyingine, kama kawa kama dawa, leo tunaendeleza tulipoishia juzi (Alhamisi) kuhusu Historia na Maisha na Tabia za Wanyiramba na Wanyisanzu, makala iliyopita tulipitia Historia yao na Koo mbalimbali na sehemu koo hizo zinakopatikana...ungana nami tuwafahamu hawa rafiki zangu ninapoandika makala hii kutoka Kidarafa pembeni ya "kata upepo"

SURA
Wanyiramba na Wanyisanzu wengi wana;
  • meno mekundu na mafupi (uwekundu kutokana na maji yenye flourine nyingi maeneo mengi ya Iramba)
  • Nywele ngumu za kipilipili
  • Uso wenye aibu na macho yasiyopenda kukabiliana na macho ya mtu mwingine
LUGHA
kama tulivyosema awali Wanyiramba na Wanyisanzu wote ni wabantu na lugha zao zimefanana kwa sehemu kubwa. Kwa mfano neno "twende" Wanyiramba husema "kweini" na Wanyisanzu husema "kweni", Na MAJI Wanyiramba hutamka "Maazi" huku Wanyisanzu wakisema "Mazi"
Aidha zipo herufi za alfabeti za Kiswahili ambazo hazipo katika lugha hizi zote mbili. Mfano herufi "F", "V" na "SH" hivyo maneno yenye hizo herufi hutamkwa kama ifuatavyo
Fimbo hutamkwa Pimbo
Ofisi wao husema Opisi
Viatu kwao ni Biatu
Ushanga wanasema Uchanga

 TABIA
Hapa ndipo tofauti kubwa ilipo baina ya Wanyiramba na Wanyisanzu. Na moja ya tofauti kubwa ni kuwa Wanyisanzu ni moja ya jamii chache za Tanzania ambapo mwanamke ananguvu kuliko mwanaume (Matrilinier society) na mambo mengine kadha wa kadha

Wanyiramba
Wanyisanzu
Wanasalimia kwa sauti ya upole
Wanasalimia kwa sauti ya Ukali
Wanaetoa maelezo ya jambo hadi kieleweke (ni walimu wazuri na wavumilivu)
Hutumia lugha ya ukali kuelekeza jambo na ni kama wanatoa maagizo
Hutumia lugha ya kuomba na unyenyekevu
Hawajui kuomba na hutumia amri
Ni wakweli na hawajui kuficha siri
Ni wasiri sana na hii hupelekea kutokuwa wakweli
Hawapendi vita wala shari na watu wengine
Wanapenda sana ugomvi
Mwanaume ana madaraka ya mwisho katika familia
Mwanamke ndiye mwenye mamlaka ya mwisho katika familia

MIIKO 
Kuna miiko mbalimbali katika jamii za kinyiramba na Kinyisanzu, hizi ni baadhi tu ya miiko yao japo mengi hayapo tena siku hizi za dot com 
  • Huruhusiwi kuonana na mkwe wako hadi baada ya kuzaa watoto wawili na unapoenda huko ukweni maandalizi maalum ya kimila hufanyika.
  • Kama jamii nyingine za Kiafrika, msichana kuzaa nje ya ndoa ni mwiko
  • Kwa waliooa au kuolewa, ni mwiko kuoga mtoni hasa kwa wanawake
  • Wanaume waliooa hawaruhusiwi kuambatana (kuwa na kampani moja) na vijana (mabachela)
  • Kwenye chakula, kuna miiko kadha wa kadha. Mfano wanawake wajawazito hawaruhusiwi kula mayai, watoto katu hawagusi utumbo na vijana hawali bandama. 
MYTH (Imani za "Kufikirika")
Kuna wanyama huwa wanamikosi, kama ukiona paka wanajamiiana utaona au utasikia habari mbaya inayokuhusu, na kama kinyonga au mbweha akikatiza mbele yako wanaamini utasikia habari za kifo au ugonjwa wa ndugu yako


Mpenzi msomaji, naamini leo umepata machache ambayo ulikuwa huyajui kuhusu hawa ndugu zetu ambao wanapatikana katika Mkoa wa Singida hususani wilaya ya Iramba. Bado kuna mengi ya kujuzana kuhusu wao na jamii zingine za huku kwetu, hayo na mengine mengi yanakujia hapa hapa Ohayoda. Mpaka Jumanne ijayo ila usiache kusoma Ohayoda ujue mengi usiyoyajua
Songela Zig Zig

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda