Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, July 22, 2012

Kanisani Leo: Wakristo Wanaotoka Kanisani kabla ya Ibada Kwisha waonywa

Kanisa Haydom wakati linajengwa miaka ya 1990
Mwinjilisti wa KKKT mtaa wa Haydom Elibariki Momo amewaonya wakristo wenye tabia ya kutoka kabla ibada kumalizika na kuongeza kuwa wanahitaji neema ya Mungu. Mtumishi huyo wa Mungu aliyasema hayo leo katika Ibada ya kwanza kanisani hapo baada ya tabia ya baadhi ya waumini ambao hutoka baada ta kutoa sadaka wakati ibada bado inaendelea.
Mwinjilisti huyo alisisitiza kuwa tabia hiyo si nzuri na waumini wanaofanya hivyo wanaonesha kuwa neema ya Mungu bado haijawafikia kwani wanashindwa kusubiri ibada ambayo inachukua saa moja na nusu tu na pia inaonesha kutokuwaheshimu watumishi wa Mungu ambao wanaongoza ibada hiyo.
Awali akihubiri katika ibada hiyo, mwinjilisti Yakobo Awe alisema kuwa kila kitu tunachokifanya, vyote tulivyonavyo ni kwa neema ya Mungu na wala si kwa matendo yetu bali Mungu katukirimia neema kupitia mwana wake wa pekee Yesu Kristo aliyetufia msalabani.
Mahubiri ya leo yaliongozwa na neno kutoka Injili ya Mathayo 12:9-16

Akaondoka huko, akaingia katika sinagogi lao.
10  Na tazama, yumo mtu mwenye mkono umepooza; wakamwuliza, wakisema, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? Wapate kumshitaki.
11  Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, na yule kondoo ametumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwopoa?
12  Je! Mtu ni bora kuliko kondoo mara ngapi? Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato.
13  Kisha akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, ukawa mzima kama wa pili.
14  Lakini wale Mafarisayo wakatoka wakafanya shauri juu yake jinsi ya kumwangamiza.
15  Naye Yesu hali akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
16  akawakataza wasimdhihirishe;

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na Upendo wa Mungu Baba, na Ushirika wa Roho Mtakatifu uwe nanyi nyote wasomaji wa Ohayoda popote ulimwenguni!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda