Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, July 30, 2012

Je, Utawezaje kuchukuliana au Kuishi na Mtu mwenye Tabia za kundi la Melankoli? (It is good to Know Your Personality.)

Na Nelson Faustin Nd.
 Wasalaam wapenzi wasomaji wa blog hii ya OHAYODA, na wale ambao ni mara yao ya kwanza kujiunga nasi katika safu hii ya "Ijue Haiba yako" (Know Your Personality).

Ni matumani yetu kuwa mnaendelea kujifunza na kufahamu mengi sana kupitia blog hii, nia na malengo yetu ni kuwasadia wanajamii kwa kuwaelimisha au kwa kuwakumbusha yale masuala ya muhimu ambayo yataifanya jamii yetu iishi bila migogoro na hata kama itakuwepo basi iwe ya kuweza kutafutia suluhisho bila ya kuiweka jamii katika hali ya hatari. Kila mmoja wetu anapaswa kulifahamu hili kuwa, "Kukosekana kwa maelewano katika jamii hutokana na kwamba watu hawajaweza kuzitambua tabia zao za asili na kuweza kuishi na watu vizuri japo kila mtu ana mapungufu yake ndio chanzo cha migogoro isiyoisha kwenye jamii yetu."

 Je, Utawezaje kuchukuliana au Kuishi na Mtu mwenye Tabia za kundi la Melankoliu? Ni kwa kuyafahamu mapungu yake kwanza.
Katika somo letu la leo, tutamaliza kwa kujifunza mapungufu ya mwanadamu mwenye tabia za kundi la Melankoli kwa asili.

 • Huwa si wepesi sana kukasirika. ILA wakikasirika hasira zao hudumu kwa muda mrefu sana.
 • Kutokana na kushindwa kusamehe baada ya kuudhiwa na kukasirika, Melankoli huishia kulipiza kisasi kwa kiwango kile kile alichokasirika.
 • Wakati mwingine, mtu mwenye tabia za kundi la melankoli si mwepesi sana kuendana na Uhalisia bali kwa wao kanuni na sheria ndizo zinatakiwa zifanye kazi katika kila hali hata kama hali halisi hairuhusu. Tabia hii huwafanya waitwe "Radical People".(Never change)
 • Kutokana na Misimamo yao, huifanya dunia kuwaona wabinafsi kwani huona walichonacho ni cha maana zaidi kuliko walichonacho wengine, lakini  pia kwa kuwa wanafahamu wana vipawa vya ajabu huweza kukaa kimya pale wanapohitajika kufanya kitu na hata kama wana kitu kizuri hupenda kuvitumi peke yao. (Egoistic People).
 • Hii ni hatari sana:- Ni Wagumu sana kuomba MSAMAHA, hata kama inawapasa kuomba msamaha hufanya hivyo lakini kwa kuzunguka zunguka sana. Kwa mfano:- Wewe kama unadhani nimekukosea we nisamehe tu, Au kama hutaki kunisamehe basi......nk.
 • Wanapenda sana mambo ya "mahakamani" hata kama kesi yenyewe ni ndogo kiasi gani kwani lengo lao ni kuonekana wpo juu zaidi ya wengine. Ni hatari sana aisee...
 • Ikiwabidi kubadilika kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wao, Huwachukua muda mrefu sana kubadilika kutokana na maswali yao ya Who? Why? When? How? and  Where?
 • Wanajiamini sana kupita kiasi, kiasi kwamba wanadhani hakuna wa kuweza kuwababaisha kwa lolote, hata kama kujiamini kwao si sahihi. Hii huwafanya watu waseme,"Mtu fulani ana majivuno sana na anapenda sana kujisifiasifia".
 • Tatizo likitokea ni wepesi sana kuwatuhumu na kuwahukumu watu wengine (substitution&replacement) kwani wanaamini kuwa wao ni wakamilifu (Perfectionists) na haiwezekani wakosee japo huwa wanakosea.
 • MATENDO kwao ni ya muhimu zaidi kuliko IMANI, watu hawa huenda kwa kuona zaidi na si kwa matendo, Hii huwafanya hata kumpinga Mungu au kuweka mashaka juu ya Utendaji wa Mungu. Matokeo yake, hujenga imani yao katika kile wanachokiona wao kuwa kinafaa. (This is funny..Kuamini kwao bila kuona huwafanya wasiamini kabisa mambo ya ushirikina)
 • Hawapendi sana kupashwa kazi, kutumwa au kulazimishwa kufanya kitu fulani, kwa wao HIARI ni jambo la muhimu sana na si kulazimishana.
 • MASHAKA (unrest) ni sehemu ya maisha yao, huwa hawaishi huishi kwa mashaka mashaka juu ya kazi, afya, au hata watu wengine, hivyo hujiona kuwa lazma wana tatizo fulani. Kwa mfano, ni watu wa kwenda hospitalini kila mara.
 • Fear of The Future,,Swali kwamba, Itakuwaje?... huwasumbua sana kwani wana wasiwasi sana na mambo yajayo, wangewezakujua siri ya mambo yajayo amani yao ingekuwa kubwa sana, kumbuka kuwa hawa ni watu wanaopenda kufahamu na si kuamini tu.
 • Mara kwa mara hupambanana na hali ya kukosa usalama wa ndani hata kama wanajiamini kwani wanaona kuwa jamii haiwaelewi na hivi hujikuta wakiumia pale wanapokataliwa, au kubishiwa, na hata kukosolewa hasa na mtu mwenye tabia za kundi la KOLERIKI. 
Mpenzi msomaji, hadi hapo tumefikia mwisho wa sehemu hii ya kujifunza mapungufu ya Melankoli, Kipindi kijacho tutajifunza namna ya kuishi na Melankoli kwani tumeona namna ambavyo mtu huyu ana mapungufu mengi na magumu, Inahitaji sana kumfahamu vizuri ndo uweze kuishi naye, tayari tumemfahamu, kipindi kijacho tutajifunza namna ya kuweza kuishi naye bila ya kusababisha fujo kwani hawa wajamaa ni wa shari sana.

Ewe MELANKOLI, kama hizi tabia bado unazo, na huna mpango wa kuziacha, ujue wewe ni chanzo cha vurugu kwenye jamii yako. Kipindi kilichopita niliezeza kuwa,.........................

"Kwa namna fulani unaweza kuona kuwa wewe ni MELANKOLI ila kuna baadhi ya dondoo za tabia tumeainisha hapa na wewe hauna,...KATIKA SOMO HILI LA HAIBA TUNAJARIBU KUCHAMBUA TABIA ZA ASILI ZA BINADAMU KATIKA MAKUNDI HAYA MANNE YANI SANGWINI, MELANKOLI, KOLERIKI NA FLEGMATIKI ila kutokana na mabadiliko ambayo mwanadamu anapitia katika mchakato mzima wa kukua na maisha kwa ujumla kama vile kubanwa na sheria za dini, kazi, sheria za nchi, tamaduni nk, au kutokana na majukumu, hali ya maisha, ushawishi utokanao na watu wanaokuzunguka, nafasi yako katika jamii nk..unajikuta unajenga mtu wa tabia fulani kwani kila binadamu anayetazamia mazuri hufanya mazuri ili kupata mazuri na kwa kufanya hivi hujikuta akijenga tabia za aina mbali mbali ambazo ni nzuri zinazokuweka katika hali ya kuonekana huna udhaifu wowote"

NB: OHAYODA kama kioo kitatenga somo maalumu kwaajili yako la kuwagawa wanadamu katika makundi makuu mawili yaani:- BINADAMU WEMA NA WAOVU. Tukumbuke kuwa binadamu wote tunatabia za asili.

BAADA YA SOMO HILI LA HAIBA, TUTAJIFUNZA MASOMO MENGINE KWA KUJIBU MASWALI YAFUATAYO.

 1. Kama mzazi, Kuna Ulazima wa Kufahamu Tabia/Haiba ya Mwanangu? Kama Inatofautiana na yangu Nifanyeje?
 2. Hivi kwa nini baadhi Watu Waliopendana sana huwa Maadui wakubwa sana Baada ya mahusiano yao kuvunjika? (utapata na ushuhuda wangu hapa)
 3. Kwanini Wasichana Wengi WALEO wanakuwa na mawazo ya kukataa kuolewa tangu wakati wakiwa na umri wa miaka 16+?
 4. Je, kuna Uzuri au Ubaya wowote wa mahusiano ya kimapenzi wakati wa UANZAFUNZI wa ngazi yoyote? (Tutapata kuona shuhuda za mahusiano yaliyodumu hadi ndoa na zilizovunjikana na kuleta hasara kubwa sana)
 5. Kwa nini wanaume wengi leo wana Hofu kubwa kuhusu kuoa?
 6. Je, kuna umuhimu wowote wa Msamaha katika jamii?
 7. Itakuwaje kama ndoa ni ya watu wenye haiba za tabia tofauti kwenye makundi tofauti kama vile sangwini na Melankoli, au sangwini na sangwini, au ya flegmatiki na koleriki, nk?Je wanaweza wakaishi pamoja? Na Je, zinadumu?
 8. Tutajaribu pia kuangalia mwanzo na hatma ya "life style ya Usharobaro", na Je, ina sababu zozote za kisaikolojia? Na je walio wa hulka hii Je, ni Masangwini, Makoleriki, Mamelankoli au Maflegmatiki? 
Tunaamini utanufaika sana na safu hii..........

NB: Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo. 

 
Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake yeye mwenyewe.
 
No Body Is Perfect, Who are you to Judge others?


KAMA KAWA,, MUNGU AKUTUNZE....
0753-038005
sonnelly06@gmail.com


Tuonane Jumatano.................................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda