Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, July 20, 2012

Je, Mandela aliiuza Afrika Kusini kwa ajili ya Tuzo ya Amani ya Nobel?

Ifuatayo ni barua ya wazi  kwa Nelson Mandela iliyoandikwa na kijana mweusi wa Afrika ya Kusini na kuchapishwa katika mitandao mbalimbali wakati mzee Mandela akitimiza miaka 94. Ohayoda imefanyia tafsiri barua hiyo ambayo imefanywa na Amani Paul na Nelson Faustin
Mzee Madiba katika sherehe ya "Birthday" ya Miaka 94


Kwa kuwa leo tarehe 18 Julai 2012 ni siku ya kukumbuka kuzaliwa Nelson R. Mandela, ni vema kuandika barua kwake wakati dunia nzima ikisherehekea siku hiyo pamoja naye. Hii ni barua ya wazi kwa Mandela.Mpendwa Rais Mstaafu Nelson Mandela,
Nilikuwa na umri wa miaka mitano ulipoachiliwa toka kifungoni. Nikiwa mtoto mweusi nimelelewa na kukulia katika familia yenye maisha duni na bibi yangu. Mwaka 1994 Afrika Kusini ilifanya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia; Nakumbuka watu wengi waliokuwa wakinizunguka akiwemo bibi yangu walijawa na shauku ya kukuchagua wewe na chama cha ANC. Bahati mbaya bibi yangu alifariki kabla ya uchaguzi kufanyika April 1994
Ninafahamu kuwa kati ya mwaka 1985 na 1990 ulifanya vikao vingi na P. W. Botha na kujadiliana namna ya kufikia muafaka. Marehemu Rais wa zamani wa ANC Oliver Reginald Tambo akizungumzia vikao vyako na serikali ya kikoloni ya kibaguzi katika miaka ya 1980 alisema "Wafungwa hawawezi kujadili kuhusu uhuru wao" (prisoners can`t negotiate their freedom)

Haya nimeyafahamu kwa mujibu wa maveterani wa ANC kuwa Tambo alionekana kusumbuliwa sana juu ya baadhi ya viongozi waandamizi wa ANC ukiwemo wewe mwenyewe ambao walionekana kuhatarisha chama. Alijawa na swali la "nani wa kumwamini" na kwa mujibu wa maveterani hao ndilo lililopelekea Tambo kupata ugonjwa wa kiharusi (stroke)

Kabla haujaachiliwa mwaka 1990 uliwahakikishia wafuasi wako kuwa migodi, mabenki na madini yangetaifishwa. Imani hii ndiyo ilikuwa msingi wa ANC na kuahifadhiwa katika "Mkataba wa Uhuru" (The Freedom Charter)
"Utajiri wa taifa letu, urithi wa Waafrika Kusini ungerejeshwa kwa watu; utajiri wa madini chini ya ardhi; mabenki na viwanda vitamilikishwa kwa wananchi wote, viwanda vyote na biashara zitakuwa kwa ajili ya manufaa ya wengi" Mkataba huo ndivyo unavyosema
Ikaja kuibuka kuwa wewe na viongozi wengine wa ANC mlikuwa mkitoa "tafsiri" mpya ya "mkataba wa uhuru" kwa ubunifu wa hali ya juu, juu ya utaifishaji ili kuwapooza mabepari weupe waliokuwa wamehodhi (migodi, viwanda na njia za uzalishaji mali)

Jinsi usaliti ulivyofanyika
Wakati mkijadiliana na makaburu, makaburu walinia kuwa na makubaliano yatakayowahakikishia kubaki kwa Afrika Kusini ya Mabepari weupe na itakayochuma faida kutoka kwa weusi wengi huku nguvu ya dola ikibaki kwa mabepari hao kwa kipindi kirefu. Kama alivyosisitiza De Clerk (rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini) "Sina nia ya kujadili kuondoka madarakani". Lakini kinyume chake, majadiliano yalinuia kuzuia ushindi wa weusi wengi. De Clerk aliweka mtego wa kuwanasa weusi ambamo walitumbukia humo  kwa mwongozo wako. Makubaliano yoyote yaliyofanywa na "shetani" kwa namna yoyote ile lazima yatakuwa batili, na mlizidiwa na kushindwa na makaburu katika majadiliano hayo.

Kushindwa kuhamisha mamlaka kutoka kwa weupe kwenda kwa weusi

Majadiliano yalilenga nyanja mbili. Moja kisiasa na pili kiuchumi. Katika majadiliano hayo mlichagua kutenganisha mamlaka ya kisiasa na yale ya kiuchumi. Hilo ndilo lililokuwa kosa kubwa kuliko yote mlilolifanya na la usaliti dhidi ya weusi. Kuhamisha umiliki wa utajiri na ardhi ndicho kiini cha kuhamisha mamlaka kama ilivyooneshwa kwenye Mkataba wa Uhuru lakini mkapuuzia hilo.

Wakati wa majadiliano kila mtu alikuwa makini na majadiliano ya kisiasa. Mlikuwa na hofu kuwa kama majadiliano ya kisiasa hayataenda vizuri kutakuwa na maandamano ya umma. Wengi hawakuwa na haja ya kujua majadiliano ya kiuchumi na hata waliokuwa wakifanya majadiliano ya kiuchumi walileta mrejesho kwa watu, walichukulia kuwa ipo kitaalamu zaidi na hawakuona manufaa. Ulipaswa kutambua kuwa weusi wengi hawakuwa na elimu na hapo ndipo tulipokosa uhuru wetu moja kwa moja na kuuuza  kwa makaburu. 

Kushindwa kwa makubaliano ya kiuchumi na utaifishaji wa Benki Kuu
Ndugu rais mstaafu, ulipewa mamlaka na watu kuhakikisha kuwa makubalino/mkataba wa uhuru unatekelezwa ikiwemo kutaifishwa kwa rasilimali zote za nchi. Lakini kinyume chake ulikuwa ukikutana mara kwa mara na Harry Oppenheimer, aliyekuwa mwenyekiti wa Anglo-American na De Beers, ambao walikuwa alama ya serikali ya kibaguzi ya makaburu

Muda mfupi baada ya uchaguzi wa mwaka 1994, ulifikia hatua ya kukabidhi mpango wa kiuchumi wa ANC kwa Oppenheimer kwa ajili ya uhakiki na kufanyia marekebisho muhimu yaliyokuwa na manufaa kwake au aliyokuwa na wasiwasi nayo pamoja na yale ya mabepari wengine. Aibu yako uliuza madini na ardhi yetu kwa mabeberu.

Matokeo ya mikutano hiyo ni kuwa wewe uwe na mamlaka ya kisiasa lakini dhahabu na almasi vibaki katika mikono ya waliokuwa wanavimiliki hapo kabla. Hivi ulisahau "Mkataba wa Uhuru" ulisema nini?

Udhihirisho wa mabadiliko ya kiuchumi unaoneshwa na umiliki wa benki Kuu ya Afrika Kusini ambacho ndiyo yaasisi yenye nguvu zaidi za kiuchumi nchini. Hatma yake ilielezwa na Vishnu Padaychee, mfanyabiashara wa Durban; Aliyeomba kuandaa makubaliano kwa ajili ya timu ya makubaliano juu ya faida na hasara ya kuwa na Benki Kuu huru, iliyo na uhuru wa kufanya kazi bila kuingiliwa na serikali. Vishnu Padaychee hakuamini alichokisikia, yeye na wenzake waliwasilisha hati iliyokuwa na sera ya kuzuia kuruhu Benki Kuu kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo yake bila kudhibitiwa na serikali.

Baadaye alijulishwa na timu ya majadiliano kuwa "ilitubidi tuliache hili" (la kuzuia Benki Kuu kuwa huru)

Benki Kuu inamilikiwa na watu binafsi na leo hii inawanahisa wapatao 650, Mandela kwa nini uliruhusu Benki Kuu kuchukuliwa na kumilikiwa na mabeberu weupe?

Katika makubaliano ulikubali siyo tu kuwa Benki Kuu itaendeshwa kama chombo huru ndani ya Afrika Kusini ambayo uhuru wake kutunzwa ndani ya katiba ya Afrika Kusini, lakini pia itaongozwa na Chris Stals, mtu yule yule aliyeiongoza chini ya serikali ya kibaguzi. Derek Keyes, kiongozi mwingine katika serikali ya kibaguzi aliendelea kuwa waziri wa Fedha. Mandela imekuwaje hata ukawaruhusu watu waliotukandamiza kumiliki Benki Kuu?

Padayachee alilalamikia kuporwa kwa Benki Kuu, "tutapoteza kila kitu katika mabadiliko ya kiuchumi". Na ndivyo ilivyokuwa baada ya WEWE kuwakabidhi Benki Kuu!!!!
Moja ya kipengele katika mkataba wa uhuru ilizungumzia kugawanya ardhi upya; kipengele ambacho kilifutwa na kuingizwa kipengele kipya cha kulinda mali zote binafsi "protection of all private properties"

Kushindwa kwa dhana ya "nchi ya upinde wa mvua" (rainbow-nation coated myth)

Umekuwa ukihubiri dhana ya nchi ya upinde wa mvua ambayo haipo kiuhalisia isipokuwa kichwani kwako tu. Upatanisho haukuwa na maana yoyote zaidi ya weusi "kuwasamehe" weupe kwa miaka zaidi ya 300 ya ukandamizaji, uporaji wa mali na unyama dhidi ya weusi. Ninapata maumivu kila mara ninapomsikia mweupe (kaburu) iwe dukani, kwenye baa, kwenye radio 720 au katika mijadala ya mitandaoni kuwa "yatupasa kusahau yaliyopita na kuganga yajayo". Ni kama wanatuambia "sahauni maumivu yenu" hasa unaposikia kutoka kwa mtu aliyenufaika sana kutokana na maumivu yetu. Tumenyanyasika sana na wanyanyasaji wetu wakingali kati yetu.

Dhana yenu ya upinde wa mvua, wewe na Desmond Tutu imejengwa juu ya maumivu haya na kuwapa nafuu makaburu. Makaburu hawaoni maumivu na mateso yetu kwa kuwa wanafaidika na maumivu yetu. Lakini wewe ulikuwa na hofu ya kuzamisha mtumbwi kwa kuwalinda weupe. Ndiyo maana unaonekana kuwa na haiba ya usaliti zaidi kwa makaburu kuliko kwa weusi.
Weupe nchini wanaamini kuwa wewe peke yako ndiye mweusi mwenye haiba na heshima na tuliobakia ni mafisadi, wabakaji, walevi, wahalifu na wapumbavu wasio elimika. 

Dhana nyingine ya upinde wa mvua baada ya 1994 ni ile ya Mazingira huru na haki. Weusi hawapo huru (labda kama unatafsiri uhuru kama uhuru wa kupiga kura na kutokubeba kitambulisho masaa 24). Hatuko huru na hakuna haki wala usawa na haya yote ni matunda ya Mandela.

Hali Ilivyo
Je unahabari kuwa Waafrika (weusi) hawana ardhi, hawana chakula, hawana makazi, hawana ajira, hawana uwakilishi wenye uwiano katika nafasi za juu? Huduma za afya na elimu kwa weusi imebaki kama zamani na pengine mbaya zaidi ya hata wakati wa ubaguzi.

Alama za ubaguzi na njia za uchumi za kikoloni, umiliki na udhibiti vimebaki kama zamani pamoja na kuwa na uhuru wa kisiasa ulioupata. Hivi unajua kuwa uhuru wa kisiasa bila kumiliki uchumi hauna maana?
Tatizo la ajira nalo linaakisi ubaguzi wa rangi uliokithiri. Robo ya tatu ya mwaka 2010, 29.80% ya weusi walikuwa hawana ajira ukilinganisha na 22.30% ya machotara, 8.60% ya wahindi huku weupe wasio na ajira wakiwa 5.10% tu. Zaidi ya watu milioni 12 wanaishi chini ya Randi 2.50 kwa siku huku zaidi ya Waafrika Kusini milioni 16 wakipokea misaada ya kijamii (social grants)
MUwiano wa pato kulingana na rangi kwa mwaka 2008 unaonesha kuwa weusi ni 13% ya pato la weupe huku machotara wakiwa 22% la weupe kulingana na 10.90% na 19.3% mwaka 1993. Pengo la kipato baina ya wahindi dhidi ya wazungu likungua kutoka 42% mwaka 1993 hadi 60% mwaka 2008.
Mwaka 1995 wastani wa matumizi (per capita expenditure) ya weusi yalikuwa Randi 333 kwa mwezi dhidi ya R3,443 kwa mwezi kwa weupe. Mwaka 2008 wastani huo wa matumizi kwa waafrika ni R454 kwa mwezi kulinganisha na R5668 kwa mwezi kwa wazungu. Hii ni kwa mujibu wa: [Leibbrandt, M. et al. (2010), "Trends in South African Income Distribution and Poverty since the Fall of Apartheid"]

Uchumi umeshindwa kutengeneza fursa za ajira kulingana na kasi ya kuongezeka kwa ukesefu wa ajira, na mfumo wa elimu umeshindwa kuhakikisha kuwa usawa wa matumizi katika elimu yanaakisi ubereshaji wa elimu kwa watoto maskini wa kiafrika.

Mawazo hitimsho
Demokrasia haijaleta kile kilichoahidiwa, wewe kama raisi wa zamani wa nchi na ANC unawajibika kwa uongozi wenye upotoshaji
Ndugu rais mstaafu, ulichowatendea weusi ni kuwa umepigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza kwa kutuuza ili ufikie ndoto zako za ushindi wa kisiasa. Ndoto zako zimekuwa jinamizi baya zaidi kwetu sisi weusi.

Umetuuza kwa tuzo ya "Amani ya Nobeli" na hii ndo sababu ya migomo inayotokana na utoaji duni wa huduma. Katiba yetu imekuwailiyosifika kuwa moja ya katiba bora duniani lakni inawapendelea wazungu huku ikiwakandamiza waafrika. Mandela tunakushukuru kwa hilo. Ulielewa barabara kuwa makubaliano ya Kempton Park kama suluhisho la uuzaji wa jumla ili kuokoa mtaji wa wazungu na waafrika wachache waliokuwa madarakani na kwa demokrasia hii waafrika wengi wangeendelea kuteseka sana. 

Ninatatizo na watu wanaotoa "Heshima ya Kimasiha kwa Madiba"   (Messianic status to Madiba) kama Yesu mweusi wakati sote tunafahamu dhahiri kuwa uliangusha taifa la watu weusi

Mwanzoni mwa barua hiii, nilikueleza kuhusu bibi yangu aliyefariki kabla ya kukupigia kura. Ukweli ni kuwa ninafuraha kuwa hakuwahi kukupigia kura kwani angekuwa amempigia kura msaliti. Uliyofanya ni muendelezo wa wa serikali ya kibaguzi na kuendelea kutusokomeza katika lindi la umasikini na ukandamizaji.
 
Kabla ya haujamaliza siku zako za kuishi duniani ningepende uwajibike na uombe radhi kwa matendo yako dhidi wa watu weusi. Uliuza ardhi yetu kwa mabeberu, kama ukishindwa kuomba msamaha ukiwa hai, hii itakuwa in maana rahisi tu kuwa wewe ni mshiriki pamoja nao na hivyo wewe ni mwenzao.
Kabla ya haujamaliza siku zako za kuishi duniani ningepende uwajibike na uombe radhi kwa matendo yako dhidi wa watu weusi. 

Na hatimaye utakapofariki na kukutana na  Dr Hendrink Verwoerd na P.W. Botha nakutakia wakati mzuri wa kufurahi na kuchekelea namna ambavyo waafrika wakiendelea kuteseka. Sina mengi zaidi ya chuki kwa yote uliyotutendea.

Ninahitimisha kutoka katika giza nene la ukandamizaji ulilotuingiza
Wako mtiifu

Chipukizi

Barua hii imeandikwa na kijana wa Afrika Kusini na kuchapishwa katika magazeti mbalimbali na Ohayoda imefanya tafsiri kutoka katika mtandao wa http://www.bulawayo24.com/index-id-opinion-sc-columnist-byo-17810-article-How+Mandela+sold+out+blacks+for+a+%27Noble+Peace+Prize%27.html

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda