Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, July 13, 2012

IJUE HAIBA YAKO (know your Personality)-SANGWINI SEHEMU YA TATUNa Nelson Faustin.

MAPUNGUFU YA SANGWINI.

Wapenzi wasomaji wa blog yetu ya OHAYODA, tuendelee na somo letu la kuzifahamu haiba mbali mblali ha hususani haiba ya SANGWINI ambaye tulianza naye.


Katika somo letu,tumeshaona maana ya sangwini na sifa njema za sangwini zinazomfanya awe mtu wa thamani sana kwenye jamii.


Kwakuwa kila binadamu ana mapungufu yake licha ya sifa njema alizonazo, Tafiti zinaonesha kuwa kwa asili sangwini ana mapungufu yafuatayo.


 • Si mtu wa kuaminiwa sana kwani hawezi kutunza siri hasa za mambo ambayo ni nyeti sana.
 • Kwa kawaida si watunza muda.
 • Wana kilema cha kukosa mpangilio kwa jinsi yao ya kufanya kazi.
 • Ni rahisi sana kuongozwa na mihemko katika kufanya maamuzi na si kutafakari kwa kina zaidi kabla ya kuamua jambo lolote.
 • Ni wepesi sana kukasirika na hasira hizi  huleta madhara makubwa sana kwa muda mfupi licha ya kwamba hasira yake inaweza kuisha kwa muda mfupi.
 • Tabia yake ya kuongea sana  husababisha watu kumpuuza hata kama anaongea jambo lenye mshiko.
 • Kwa kukosa mpangilio ni mwepesi sana kusahau na hii inaweza kusababisha hasara kubwa sana.
 • Tabia yake ya kujali sana watu humsababishia mvunjiko wa moyo pindi wale wanaojaliwa wanapokuwa hawaoneshi kuguswa na hali yake, ambapo mwishowe humfanya ajenge uadui na watu kirahisi.
 • Lazima asimamiwe kinyume na hapo kazi haiwezi kufanyika ipasavyo.
 • Tabia yake ya kufanya kazi katika kundi humfanya ashindwe kufanya kazi kwa ufanisi pindi awapo peke yake.
 • Sangwini mi mwoga, mara nyingi ni wepesi sana kuanzisha jambo ila huwa ni vigumu kuliendeleza mpaka mwisho.
 • Ni mwepesi kujiingiza katika matukio mabaya hasa ya starehe za kupita kiasi kama kutumia madawa ya kulevya ili kupata faraja pale inapompasa kuwa mpweke-replacement behaviour.
                                      Itaendelea kipindi kijacho...................................................................


NB: Japo tumeona mapungufu hayo na mengi zaidi tutakayoyaona kipindi kijacho,kama mwanadamu kwa namna moja au nyingine unaweza kujiona wa hasara sana au kama kiumbe dhaifu sana, Nikutie moyo kuwa wewe ni mwanadamu mwenye sura na mfano wa Mungu na una kila sababu ya kumshukuru sana Mungu kwa jinsi ulivyo na kwa kuwa alikuumba bado atakupa njia bora za namna ya kuishi.

Usiache kututumia maoni yako.

                                               MUNGU AENDELEE KUKUTUNZA.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda