Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, July 27, 2012

Je, Unayafahamu Mapungufu ya Mtu Mwenye Tabia za Kundi la Melankoli?...It is Good to Know Your Personality.Kuishi Bila mogoro inawezekana
Na Nelson Faustin-JR Psyc.
Melankoli kama mwanadamu mwingie yeyote japo hufahamika kama mkamilifu yani "Perfectionist" ila ni kundi lenye tabia zenye mapungufu makubwa tu ambapo inahitaji pia neema ya Mungu kuweza kuchukuliana naye kwani kwa tabia yake kidogo ni changamoto.

Baada ya kuona sifa njema (strengths of a Melancholy) ni dhahiri kuwa tunahitaji pia kufahamu na upande wa pili wa shilingi kama tulivyofanya kwa SANGWINI, kwani ni vyema na haki kujifahamu katika pande zote mbili ili uweze kuishi na watu vizuri lakini pia watu waweze kuishi na wewe vizuri.

Narudia tena na tena,, dhamira yetu ni kusaidia kupunguza migogoro katika jamii kwani tuna uhakikaka kuwa, tofauti katika tabia zetu ni sehemu ya maisha na tunahitaji sana ufahamu kuwa, "kutofautiana si dhambi, dhambi ni kuzifanya tofauti hizo zitufarakanishe". Hakuna aliye mkamilifu ila Mungu mwenyewe lakini yeye hutusaidia katika katika udhaifu wetu, kwani kwa Mungu tunapokuwa wadhaifu ndipo tunapokuwa na nguvu na tusisahau yeye anahusika katika uumbaji wetu na hivyo kama kazi ya mikono yake aliuweka udhaifu akiwa na makusudi kamili. Wewe u nani hata umhukumu mwenzako kwa udhaifu wake? Lakini pia wewe u nani hata ujione mkamilifu na wengine wote ni wadhambi? 

Baada ya kupata utangulizi huo, embu sasa tujifunze yale yaliyo mapungufu ya mwanadamu mwenye tabia za kundi hili nyeti la MELANKOLI. Nyingi si nzuri sana lakini kumbuka filosofia yetu ya "umia upone".
Melankoli ni m-bishi acha...
 • Udhaifu wake mkubwa ni kuwa, huwa anajiona kuwa ni mkamilifu sana na hivyo kuwaona watu wote kuwa ni waajabu ajabu hasa MASANGWINI, au wengine ni wadhambi isipokuwa wao tu.
 • Melankoli anangozi nyembamba sana ya moyo na hivyo ni mwepesi sana kukwazika hata kwa jambo dogo, hii huwapelekea kuchoka haraka katika mchakato wa jambo fulani kwa mfano katika nyanja ya mahusiano.
 • Ni mtu ambaye hutaka kufahamu msimamo wa kitu fulani bila ya kubaki njia panda, kwa mfano kama ni ndiyo au hapana anapenda kuhukikishuwa hilo bila maelezo mengi yasiyo na tija, kitu ambacho si rahisi kutokea kwa kila jambo.
 • Si wepesi sana kutia moyo au kuongeza chumvi kwenye jambo fulani kama jambo hilo halijibu maswali yake ya Nini? Kwa nini? Ki vipi? Nani? na Lini? Hii hukatisha tamaa kwa wanaomzunguka.
 • Ni mtu wa kupenda sana sheria na misimamo isiyobadilika mara kwa mara iwe ni sahihi au si sahihi na hata kama akibadilika ni kwa sehemu ndogo sana. {static and not flexible} (Ni wabiashi acha mchezo)
 • Ni mwepesi sana kukosa uvumilivu pale ambapo mambo hayaendi aonavyo yeye na wakati mwingine ni waziraji wazuri hata kama hataonesha nnje kama amezira kwani hawa wana tabia ya ndani yani "introverts".
 • Kuliko aanzishe jambo ambalo anaona kuwa hataweza kulimaliza afadhali asilianzishe, kwa sababu hii tunaona kuwa melankoli ni waoga sana kukwama njiani katika jambo fulani.
 • Kwa kuamini kuwa wao ni maalumu sana, mara nyingine hupenda sana upweke japo si wote. Kwa kukaa pweke hupata nafasi ya kutafakari na kuibuka na mawazo mazuri au majawabu ya maswali magumu japo upweke si mzuri sana.
 • Wakati mwingine hupitwa na mambo mazuri kutokana na tabia yake ya kuchambua sana mambo kutumia maswali yake mengi ya uchambuzi, kwa hili hujikuta wanafanya maamuzi ya kukubali wakati jambo lenyewe linakuwa limeshapiata. Mfano kwenda kwenye sherehe.
 • Si wepesi sana kuchangamkia mambo na kwa hili fursa nyingi huwapita.
 • Hii ndo mbaya:...Ni wagumu sana Kusamehe, hivyo huweka mambo moyoni hasa yale mambo madogomadogo, baadhi yao hupatwa na magonjwa ya moyo hata mtindikio wa ubongo kwa kutunza kumbukumbu mbaya.
 • Na hii ni mbaya pia;....Mara nyingi ni wapinzani wenye mfumo wa maisha ya kupinga mambo na kutoa kasoro, nyingine zinaweza zisiwe na tija kwa sababu tu jambo hili hafahyi yeye. Nyingi ni za kukatisha tamaa,(-ve criticism), akifanya kazi na sangwini embu fikiri itakuwaje.
 • Maisha yao yamegubikwa na shughuli nyingi hata kama hazina tija, hii huwafanya wasiwe na muda na watu wengine hivyo hujijengea kadunia kao ka peke yao.
 • Ni watu wasioweza kudumisha urafiki hata udugu na watu kwa muda mrefu kutokana na vigezo vyao, hii huwafanya kujikuta wanakuwa marafiki wao kwa wao tu bila watu wa tabia nyingine.
 • Cha ajabu kuhusu hawa watu pia ni kwamba, mara nyingi wana "insecurity" sana japo hujiamini; kwa maana hii tunasema kuwa, wanajiamini pasipo kujikubali na hii huwafanya kutumia mabishano ili wakubalike na hadhira. (difensive)
 • Suala la kuridhika kwao na utendaji wa watu wengine ni ngumu sana, hivyo hujikuta wakiishia kufanya wenyewe hata kama baadaye itaonekana mtu wa kwanza alikuwa anafanya vizuri kuliko yeye.
 • Eneo linalohusu utani kwao ni vigumu sana kuweza kuchukuliana nalo. Wakitaniwa huchukulia kweli na kwa hili huwafanya wakasirike sana hata kujenga chuki (this makes them a very complex group     in the community)
Tujifunze kwa Tausi......
Niruhusu niishie hapa kwa leo ili nikupe fursa ya kuyatafakari na kujiona kama wewe unaingia katika kundi hili, na Je utafanyaje sasa ili usiwe kero katika jamii? Nitaendelea kipindi kijacho kakika kumalizia madhaifu haya kabla ya kuangalia namna ya kuishi na melamkoli na Je, wewe kama melankoli uishije na watu?

Kwa namna fulani unaweza kuona kuwa wewe ni MELANKOLI ila kuna baadhi ya dondoo za tabia tumeainisha hapa na wewe hauna,...KATIKA SOMO HILI LA HAIBA TUNAJARIBU KUCHAMBUA TABIA ZA ASILI ZA BINADAMU KATIKA MAKUNDI HAYA MANNE YANI SANGWINI, MELANKOLI, KOLERIKI NA FLEGMATIKI ila kutokana na mabadiliko ambayo mwanadamu anapitia katika mchakato mzima wa kukua na maisha kwa ujumla kama vile kubanwa na sheria za dini, kazi, sheria za nchi, tamaduni nk, au kutokana na majukumu, hali ya maisha, ushawishi utokanao na watu wanaokuzunguka, nafasi yako katika jamii nk..unajikuta unajenga mtu wa tabia fulani kwani kila binadamu anayetazamia mazuri hufanya mazuri ili kupata mazuri na kwa kufanya hivi hujikuta akijenga tabia za aina mbali mbali ambazo ni nzuri zinazokuweka katika hali ya kuonekana huna udhaifu wowote.

NB: OHAYODA kama kioo kitatenga somo maalumu kwaajili yako la kuwagawa wanadamu katika makundi makuu mawili yaani:- BINADAMU WEMA NA WAOVU. Tukumbuke kuwa binadamu wote tunatabia za asili.


BAADA YA SOMO HILI LA HAIBA, TUTAJIFUNZA MASOMO MENGINE KWA KUJIBU MASWALI YAFUATAYO.

 1. Kama mzazi, Kuna Ulazima wa Kufahamu Tabia/Haiba ya Mwanangu? Kama Inatofautiana na yangu Nifanyeje?
 2. Hivi kwa nini baadhi Watu Waliopendana sana huwa Maadui wakubwa sana Baada ya mahusiano yao kuvunjika? (utapata na ushuhuda wangu hapa)
 3. Kwanini Wasichana Wengi WALEO wanakuwa na mawazo ya kukataa kuolewa tangu wakati wakiwa na umri wa miaka 16+?
 4. Je, kuna Uzuri au Ubaya wowote wa mahusiano ya kimapenzi wakati wa UANZAFUNZI wa ngazi yoyote? (Tutapata kuona shuhuda za mahusiano yaliyodumu hadi ndoa na zilizovunjikana na kuleta hasara kubwa sana)
 5. Kwa nini wanaume wengi leo wana Hofu kubwa kuhusu kuoa?
 6. Je, kuna umuhimu wowote wa Msamaha katika jamii?
 7. Itakuwaje kama ndoa ni ya watu wenye haiba za tabia tofauti kwenye makundi tofauti kama vile sangwini na Melankoli, au sangwini na sangwini, au ya flegmatiki na koleriki, nk?Je wanaweza wakaishi pamoja? Na Je, zinadumu?
 8. Tutajaribu pia kuangalia mwanzo na hatma ya "life style ya Usharobaro", na Je, ina sababu zozote za kisaikolojia? Na je walio wa hulka hii Je, ni Masangwini, Makoleriki, Mamelankoli au Maflegmatiki? 
Tunaamini utanufaika sana na safu hii..........

NB: Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo. 
 
Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni KUJITAMBUA katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili ya sifa na utukufu wake yeye mwenyewe.
Enjoy Life ungali HAI HASA KIJANA


 KAMA KAWA MUNGU AKUTUNZE....
0753-038005
sonnelly06@gmail.com

Tuonane Jumatatu.................................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda