Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, July 14, 2012

IJUE HAIBA YAKO-JINSI YA KUISHI NA SANGWINI..

 Na Nelson Faustin.
JINSI YA KUCHUKULIANA NA SANGWINI-How to live along with a sanguine.


Tukirejea mwanzo wa mada yetu, tumejifunza mengi hasa yale yaliyo mapungufu ya sangwini ka asili yake. Katika kumalizia Sura hii ya kwanza ya haiba, tujifunze sasa namna sahihi za kuweza kuishi na masangwini lakini pia tutamshauri sangwini nmna bora ya kuishi na watu wa hulka tofauti na yake.

Ili kumsaidia sangwini aweze kuwa mtu wa thamani katika jamii, watu ambao wanajifahamu kuwa si masangwini na wanaishi na sangwini katika mazingira mbalimbali kama ya kikazi, shuleni, nyumbani, au popote pale katika nyadhifa mbalimbali kama vile viongozi wakubwa, wazazi, walezi, mke, mume,mtoto, rafiki wa karibu, mlezi wa kiroho nakadhalika, unaweza kuishi naye vizuri kwa kuzingatia yafuatayo.


 • Tambua uwepo wake na umwoneshe kuwa unamjali yeye na yale yote aliyonayo hata kama hutafanya anavyotaka yeye.
 • Msaidie kutunza siri hasa pale anapokuwa anaeleza kila kitu kwa kila mtu, tumia hekima katiak kumnyazisha kinyume na hapo utamsababishia mvunjiko wa moyo au anaweza akakudhalilisha.
 • Msaidie kuwa na mpangilio hasa katika kazi kwa kumsaidia kupanga au kumshauri katika upangaji wake kwani kwa kawaida ni warahisi sana kupokea ushauri.
 • Usimwache akupotezee muda au usikubali kumpotezea muda bali msaidie kwa kumkumbusha majukmu yake au kazi zinazomkabili ili asijisahau.
 • Akikosea mpe nafasi ya kujirekebisha kwa upole, USIMLAUMU.
 • Katika maamuzi, usimpe nafasi ya kufanya maamuzi kwa kufuata hisia hasa katika matukio kama michango ya harusi au kutoa misaada kwani wanaweza kutamka mambo ambayo hawana uwezo nayo, bali muulize maswali yatakayo mfanya afikiri kabla ya kuamua.
 • Tumia mbinu yoyote katika kumsimamia hata kama haupo kwa kumwekea kazi zote kwa mpangilio na uhakikishe kuwa unafuatilia kila hatua japo tunaamini anaweza kufanya mambo vizuri ila akisimamiwa anafanya vyema zaidi.
 • Katika mvunjiko wa moyo, mshauri na umpe nafasi ya kusema, kulia au kucheka sana ili kuondoa yaliyojaa moyoni.
 • Kwa kuwa hawapendi kuwa smart, msaidie kwa kumpangia nguo zake vyema ila mfundishe kujithamini hasa pindi anapotakiwa kwenda kwaajili ya matukio ya muhimu.
 • Tabia yake ya kupenda sana tafrija inaweza kudhibitiwa kwa kumpa sababu za kwa nini kila siku si siku ya starehe, na si kila tafrija lazima ahudhurie.
Kwa ufupi hizo ni mbinu za kuishi na sangwini.

SANGWINI UNAWEZAJE KUISHI NA WATU VIZURI?
Rejea ushauri wangu wa kwanza kwamba kila mwanadamu kaumbwa kwa sura na mfano wa Mungua na ulivyo ni sababu ya kumtukuza Mungu, hakuna aliyeumbwa kuwa KERO  ila baraka kwa wengine, hivyo basi kuyafahamu mapungufu ni hatua ya kwanza ila kuyafanyia kazi mapungufu ni hatua ya pili na ya muhimu sana itakayokufanya uishi katika baraka, amani na mafanikion zaidi.


Sasa mimi sangwini niishije?
 • Usifanye maamuzi ukiwa na mihemko, tulia kwanza, tathmini ndo utende, uruhusu ubongo utafakati kwanza.
 • Jitahidi kuhesabu maneno yako wakati wa maongezi hasa katika vikao vya muhimu.
 • Ukibahatika kuwa kiongozi mahali popote, soma alama za nyakati, usijizuie kufurahi ila jitahidi kuwa na kiasi katiaka mambo yote.
 • Jitahidi kuheshimu muda.
 • Fanya kila kitu kwa wakati wake.
 • Weka kila kitu mahali pake, jitahidi sana kuwa na mpangilio.
 • Tafuta mtu wa kukusaidia katika kuweka kumbukumbu hasa ya maswala nyeti.
 • Jiweke smart hasa katika muonekano wako.
 • Amini kuwa, hata ukiwa peke yako unaweza kufanya mambo na si lazima katikati ya kundi la watu.
 • Usimwambie kila mtu mambo yako, jaribu kuwa msiri.
 • Si kila atakayekupinga hakupendi.
Itaendelea.................................................

Baada ya sehemu hii, tutaendelea na HAIBA SURA YA PILI ambayo ni KOLERIKI.

                                                ENDELELA KUBARIKIWA.

1 comment:

 1. ebhana daah., ni kweli kabisa kaka kuna watu nawafahamu yani karibu kila ulichosema kinawahusu yani ni masangwini pure. endelea kutuelimisha kaka Nelson.
  .....Kenny Onney

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda