Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, July 17, 2012

IJUE HAIBA-SURA YA PILI, MELANKOLI (KNOW YOUR PERSONALITY CHAPTER TWO)

SURA YA PILI-MELANKOLI
SEHEMU YA KWANZA.

Maelezo mafupi ya Melankoli.Bila shaka umzima wa afya ndugu yetu wa OHAYODA na unanufaika na maudhui katika blog yetu, kabla sijaendelea naomba sana nitoe baadhi ya mapungufu ya SANGWINI ambayo kwa makusudi niliyaacha ili niyatoe wakati huu, nayo ni:-
 • Masangwini kwa maadili wapo chini sana na ni mrahisi sana kuwayumbisha wengine kwani wana uwezo mkubwa sana wa ushwawishi hasa wakiwa katika nafasi mbalimbali za uongozi,
 • Japo wana uwezo mkubwa wa vipawa, lakini kwa bahati mbaya sana, kwa kuwa hawana kiasi ni wepesi sana kudidimia na kukosa kukua katika vipaji kutokana na tabia yake ya kukosa kiasi,
 • Sangwini hana UMAKINI, they are very careless.
 • Walio wengi ni wachokozi na ni waanzilishi wazuri wa migomo na vurugu japo baadaye hukimbia hii ni kutokana na tabia yao ya kuenenda kihisia zaidi.
 • Si wepesi kustahimili mambo magumu, they like easy things.
 • Hunia mengi na kutimiza machache au hawatimizi kabisa.
 • Ni mwepesi kuendeshwa na matukio na si mipango.
 • Uwezo wao wa kustahimili nafasi za juu ni mdogo sana.
 • Hawapendi kuchukuliwa hatua za kinidhamu pale wanapokosea.
 • Wanalalamika sana hasa pale mambo yanapokuwa ndivyo sivyo.
 • WANAPENDA SANA UCHOCHEZI.
 • Husahau majukumu yao ya msingi.
 • Ni wepesi kutafakari vitu visivyo vya muhimu na kusahau yale ya msingi.
 • Mara nyingine huwa wabinafsi sana.
 • Hukosa hali ya kujiamini na hivyo hunisababishia kujishuku.
Yapo mengi ambayo kwa bahati mbaya tutakuwa tumeyasahau kuhusu SANGWINI, kama mdau mwenzetu katika kuielimisha jamii, usisite kutoa mchango wako kupitia sonnelly06@gmail.com

MELANKOLI
Melankoli ni nani?
Kwanza nisahihishe watu kama MC Pilipili ambao wanasema MOLEKYULI,,,hapana ni MELANKOLI....
Kwaasili wanafahamika kama (wakamilifu) Perfectionists. 

Mungu ni wa pekee sana na alipenda na sisi wanae tuwe wa pekee kama yeye.Melankoli ni mtu anayesemekana kuwa wa tafakari za kina sana hali ambayo kwa kawaida huweza kumsababishia kuwa na mahangaiko pindi mambo yanavyoenda kinyume na mitazamo yake. 

Ni mtu mwenye siri sana na kwa hali ya kipekee kuwa wabunifu wa maswala makubwa na ya maana sana. Tofauti na haiba nyingine, melankoli anasemekana kuwa mtu anayejali sana ubora, hii humfanya awe mtu wa kusahihisha sana.


Mpenzi msomaji, tuyatafakari haya, kipindi kijacho tutajifunza dondoo za SIFA NJEMA ZA SANGWINI ili upate fursa ya kufafanua na kujifahamu zaidi na kuwafahamu wengine.


KUMBUKA:
Mapungufu si kilema wala Sifa njema si kibali cha kukupa kiburi bali kwa vyovyote tulivyo hatuna budi kumshukuru Mungu na kuthaminiana.


                                                             MUNGU AKUTUNZE.
                                                        Na NELSON WA OHAYODA.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda