Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, July 4, 2012

Huzuni yangu kwa Bunge Letu.

HUZUNI YANGU KWA BUNGE LETU.

Na  Nelson Faustin
a.k.a Meku Mtanzania.

Wasalaam ndugu wasomaji wa blog yetu ya ohayoda.......Leo naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya vitimbi vinavyoendelea huko bungeni Dodoma, najiuliza je, Bunge letu bado lina hadhi ya kuitwa TUKUFU?

Angalia hapa,,,japo walisema siasa ni mchezo mchafu, kwa hapa kwetu ni mbaya zaidi na tunasahau kuwa siasa ni njia ya kupata uongozi na uongozi ni maisha ya watu sasa kwa nini wabunge wetu mnatuhuzunisha?

Mizaha inayoendelea bungeni ni mingi sana na inanifanya niwe na mtazamo kuwa siasa si utu, si heshima, si upendo, si ufanisi, si elimu,si taaluma, si busara bali ni mchezo tu wa kuigiza halafu mkimaliza muda wenu muondoke,,, kwa kufanya hivi huko kwa Mungu lazima mtalipa nawaambia.......

Ngoja niwaite waheshimiwa kwani nisipofanya hivi mtamwomba spika atoe mwongozo ili mnikamate lakini kama wasimamizi wa serikali mna dhamana kubwa sana na inahitaji kuheshimiwa, mizaha na kejeli mnazofanya huko bungeni inatufanya kwanza tusione faida ya kuwa na ninyi kama wawakilishi wenu, na mara nyingine hatuoni faida ya kufuatilia vikao vya bunge kwani ni kama vile mchezo wa chei chei shangazi kwa kelele na mizaha mnayoifanya. Japo si wote ila baadhi ya wabunge wanasababisha heshima ya chombo hiki muhimu ipotee na sisi tutawaona wababaishaji tu na tutaishia kusema,"imekula kwetu"  wamalize waondoke.


Mbali na viti vingi bungeni kuwa wazi ila hii kwangu ina maanisha kuwa hao wasiohudhuria vikao vya bunge wamechoshwa na MIZAHA hiyo kwa hiyo afadhali walale au wafanye mambo mengine kwani bado mshahara upo pale pale, jamaini MNATUPELEKA WAPI?

Bila shaka, mnafahamu kuwa, Tanzania ya leo ni ya wasomi na mnawaongoza watu wenye akili zao timamu na wanafuatilia sana yale yote mnayoyafanya, natumia nafasi hii kuwaambia kuwa kwa yanayofanywa na baadhi yenu mnatuhuzunisha sana. 

Tafadhali sana, acheni Mizaha, fanyeni kazi kwa dhamana kubwa tuliyowapa kwani bila ya kufanya hivyo damu za watanzania zinalia na zitaendelea sana kulia juu yenu.

Fanyeni mizaha sana ila mjue ya kuwa hilo jengo letu tukufu tulilowaazima kwa muda wa miaka mitano  linabeba dhamana ya watanzania zaidi ya milioni 42 na kwa Mungu mtalipa mpende msipende.

KAMA MKIKASIRIKA NISAMEHENI....HUO NI MTAZAMO WANGU NA NINA  MIAKA 26     TU....FANYIA KAZI.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda