Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, July 28, 2012

HEKO MABINGWA WA SOKA, WANA YANGA AFRICA

(Kwa marafiki zangu wote vijana wa kiafrika waipendao Yanga, na wengine wote wenye mapenzi mema)

1. Ishina nane Julai, saa kumi alasiri,
kuna waliojidai, na kujifanya jasiri.
Si jingine nakujuza, kipute cha mafahali,
hatua walomaliza, wakacheza fainali.

2. Ni vijana Afrika, wana Yanga watukuka,
na Azam wasifika, kwamba wameimarika.
Ni jambo kujivunia, kuwa kombe linabaki, 
timu mbili Tanzania, kucheza kindakindaki.

3. Mwamuzi toka Burundi, Si Nkongo ni Nkuruzinza,
wachezaji kawarudi, nidhamu kaitukuza.
Maji ukiyakamia, hautayanywa hakika,
na leo yametimia, Azam yadhihirika.


4. Waliuanza kwa kasi, mchezo kuupania,
wakaleta ukakasi, langoni kwa wenye nia.
Goli lao ni la kusi, kwenye kipindi awali,
njaa huwa halikosi, lazima lifungwe goli.
 
5. Vijana wakatulia, dakika ishina tano,
pasi wakajipigia, bila ya kuwepo Berko.
Mikiki wakaianza, akawa shakani Dida,
kina Chuji na Kiiza, wakampa sana shida.
 
6. Kipute chaendelea, Luhende akitawala,
Niyonzima nae pia, uwanjani hakulala.
Hamisi Diego Kiza, kabla ya pumziko,
hakutaka kuigiza, akatupa pambazuko.

7. Chaja kipindi cha pili, Azam waja kwa shari,
wajifanya pilipili, eti nao majasiri.
Wakaleta ushindani, Bartezi kumpa tabu,
Canavaro na Yondani, hawakuwa mjarabu.

8. Ukasonga Mpambano,Gumbo akapumzika,
akaingia Kijiko, kuungana na Mwasika.
Joshua akatulia, kwa makini akicheza,
Azam kawazuia, hakika ilipendeza.
 
9. Dakika zikayoyoma ,likatandazwa kabumbu,
Salumu na Niyonzima, wakaumana kibubu.
Saidi wa Bahanuzi, za majeruhi dakika,
hakuifanya ajizi, la pili akaandika.
 
10. Ilikuwa ni nderemo, pale mitaa ya Twiga,
Jangwani ni mirindimo, vigeregere wapiga.
Kwenu nyote wana Yanga, tuidumishe amani,
viongozi kuwapinga, haituletei shani.

HEKO MABINGWA WA SOKA, WANA YANGA AFRIKA.

MY SPECIAL AND SINCERE DEDICATION TO ALL YOUNG AFRICAN FANS, IN THIS          
  SPECIAL AND EXTRA ORDINARY DAY!


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda