Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, July 6, 2012

Happy Birthday Friends on Friday (FOF)

Leo ndo leo, asiye na mwana aeleke maboga hatimaye Friends on Friday yaani mtoko wa Marafiki ambao hukutana kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi hukutana na kubadilishana mawazo, kuburudika na kujenga mtandao inaadhimisha mwaka moja toka kuanza rasmi mwezi Julai mwaka jana.
Friends on Friday (FOF) ambayo katika kipindi cha mwaka moja imeweza kupata umaarufu mkubwa sana kwa kuwavutia watu wa kada mbalimbali hasa wasomi jijini Dar es Salaam na kuenea katika mikoa ya Mbeya na Arusha hasa vijana wa Kikristo ambao wamekuwa wakikosa "mitoko" ambayo haiathiri imani yao.
Maadhimisho ya leo yanafanyika katika kijiji cha Makumbusho kilichopo Kijitonyama Dar es Salaam kitapambwa na waimbaji kama Miriam Lukindo wa Mauki ambaye atashusha "kwaito la nguvu Ng'ang'ana" (hapa swahiba wangu Neema Isaack atajuta kutokwepo), Sarah Shilah, Steven Wambura, Amani Isaiah na Elandre huku wachekeshaji mahiri nchini wakiongoza na Mc Manu a.k.a pilipili ya shughuli akiwavunja watu mbavu, huku kukiwa na zoezi la kufungua shampaigne zipatazo 20 zoezi zima likiongozwa na Jacque Mndeme.
Ili kuifanya shughuli hii kuwa na mvuto wa kipekee na kutakuwa na FOF Fashion Show ambapo wadau mbalimbali wa FOF watakuwa wakionesha ubunifu wao katika kubuni mitindo ya mavazi na pia kutakuwa na michezo mbalimbali kama vile "actionary" n.k na kama ilivyoada ya FOF lazima kuwe na mtupio yaani "dress code" ya kila event na awamu hii mtupio ni mwekundu (red)
Friends on Friday ilifanyika kwa mara ya kwanza tarehe 1 Julai 2011 katika bustani ya hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam na mtupio wake ulikuwa mwekundu, kisha kufuatiwa na events za mitupio ya njano, traditional, free style, hot pink, puple, gold na white ambapo matukio yote hayo yalifanyika katika Hoteli ya Tamal iliyopo Mwenge.
Mwandishi wa Ohayoda ambaye pia ni moja wa waanzilishi wa FOF tayari yupo jijini Dar es Salaam na atawaletea matukio na habari mbalimbali katika picha ya yatakayojiri katika tukio hili ambalo linazidi kukua kwa kasi sana na pengine kuwa tukio litakalokuwa likifanyika nchi nzima siku zijazo.
FOF MOJA JUU!

1 comment:

  1. kuanzia leo na mimi ni member.......alaaaah

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda