Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, July 23, 2012

FAHAMU WALICHOPENDEKEZA WANANCHI WA MANYARA KUHUSU KATIBA MPYA.Kama inavyofahamika kuwa, watanzania sasa wapo katika mchakato wa kupata Katiba mpya na kama ulikuwa hufahamu mkoa wa manyara ni moja kati ya mikoa nane ambayo imeteuliwa rasmi na tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya kuwa moja ya mikoa Ambayo wanachi wamepata nafasi ya kutoa maoni juu ya katiba mpya.
Mwishoni mwa wiki hii, wanachi wazalendo katika eneo la Kwaraa’ katika mji wa Babati mkoani manyara walipata fursa ya kuonana uso kwa uso na tume ya katiba mpya. Katika majadiliano yao kuna mambo ya msingi ambayo kwa niaba ya wananchi wa mkkoa wa manyara yaliweza kuwekwa kama mapendekezo ya kuhakikisha kuwa katiba mpya itakidhi maslahi ya taifa letu. Baadhi ya mambo makuu yaliyojitokeza ni pamoja na:-

ARDHI:
Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa wanachi wa mkoa mpya wa manyara kwani wale walio matajiri wanatumia nafasi zao kuwakandamiza wanyonge na kujichukulia maeneo bila wasiwasi wowote. Hivyo wanachi walipendekeza kuwa umiliki wa ardhi ambayo ni mali ya serikali lazima uwekewe utaratibu ulio wazi kwenye katiba ili kuepusha migogoro itakayolisababishia matatizo kama yanayoendelea katika baadhi ya maeneo hapa nchini. Ohayoda inafanya utafiti na tutakuhabarisha zaidi.

MUUNGANO:
Swala la muungano pia lilizungumziwa katika mkutano huo na mwanachi mmoja alipendekeza kuwa muungano ni swala la msingi ila linahitaji zaidi uhiari wa pande zote mbili ili liendelee kuwa la manufaa kwa taifa la Tanzania. Na kipengele hiki kitapewa tena kipaumbele katika mkutano wa pili wa marekebisho ya katiba utakao itishwa na tume kwa mara ya pili kwa mkoa wa manyara na wanachi wamehizwa kutoa hisia zao juu ya swala hili la muungano ambalo kwa namna moja limekuwa tete kidogo.

SERIKALI MOJA NA MADARAKA YA RAISI
Aidha, wananchi wa manyara walishauri kuwa, katiba ijayo ipunguze madaraka ya raisi kwani iliyopo inampa raisi mamlaka makubwa sana. Sambamba na hilo, suala la kuunda serikali moja ya muungano tofauti na ilivyo sasa ni jambo la muhimu sana ili kuweka muungano katika hali nzui zaidi.

MAADILI MEMA KWA JAMII:
Ikumbukwe pia kuwa, manyara ni moja kati ya mikoa michache ambayo bado masuala ya kiutamaduni wa kiafrika unaolinda maadili ya jamii unapewa kipaumbele na bado uchakachuaji wa mila na desturi haujashika kasi kama ilivyo kwa mikoa mingine. Katika hili, wanachi wa Manyara walipaaza sauti zao kuwa katiba mpya isimamie ipasavyo suala la maadili ya jamii kwani hali ilivyo sasa inatisha.

ELIMU BURE
Katika mambo ambayo walijadili, suala la elimu pia liliibua hisia kwani mwananchi mmoja alipendekeza kuwa itakuwa vyema sana kama elimu itaelezwa kwenye katiba kama moja za huduma zitakazotolewa bure kwani wanachi wengi ni masikini na wanaikosa huduma hii muhimu.

Ndugu msomaji, yapo mengi yaliyojiri katka mkutano huo lakini OHAYODA inafurahishwa sana na mwitikio waa wanachi katika kupata hatma ya Tanzania. Mkoa wako utakapopata fursa hii nenda sikiliza na utoe maoni yako ili baadaye pasiwepo malalamiko ya aina yoyote kwani nchi hii ni yetu sote.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA NA DUNIA KWA UJUMLA.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda